Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

Nashukuru mbwiga wa msimbazi center umekiri ni kweli mchele wa Morogoro umeshuka bei, haya wajulishe na mbwiga wengine hapo Ufipa!
 
Mamamayo,, Shinyanga kwenyewe kwa wakulima maarufu wa mpunga tunauza 1700 -1800/= sasa wewe makalio utasemaje 1,300? Harafu usituambie eti uchumi umepaa wakati wakulima hatuna pa kuuzia mpunga wetu!!
Mkuu mbona huku Kahama siku ya jana nimechukua kwa 1,200/= mashineni
 
Ufipa wamebanwa kila kona mkuu!
 
Sina hakika huyo mtu ana taaluma gani,ila ni msimu wa mavuno ya mpunga,and mahidi ni mengi na mengine yanavunwa,aache unaa huyo mtu
 
Mamamayo,, Shinyanga kwenyewe kwa wakulima maarufu wa mpunga tunauza 1700 -1800/= sasa wewe makalio utasemaje 1,300? Harafu usituambie eti uchumi umepaa wakati wakulima hatuna pa kuuzia mpunga wetu!!
Hahaaa
 
Kwahiyo ulipoona kilo ya mchele imeshuka uka conclude uchumi umepanda, tuna safari ndefu sana, lazima utakuwa imesoma shule za serikali una qualify kupewa mkopo.
Ndiyo uchumi unakuwa kwa kuwa na bidhaa nyingi ambazo utauza kwenye masoko ya nje!! Wewe kila kitu kubisha tuuuu??
 
Umepotosha....

Hiki ni kipindi cha mavuno....supply kubwa kuliko mahitaji....haina uhusiano na kukua kwa uchumi...
 
ukiona unakula kwa bei nafuu ujue mkulima anauawa
 
Kipindi unapanda hadi iyo 2600 hukuwai kuja na post humu ukisema uchumi waporomoka.
 
Bw Juma kahamisha magoli JF na mijadala ya sasa unaweza lia sijui members wanakaribia kudata au wamevamia vichaa na mods wamewekewa bastola shingoni na hawajitambui.

Sasa bora siku ziende tu!
 
Gharama za kuzalisha huo mpunga nazo zimeshuka au hilo lipo nje ya kibarua chako.
 
Kumbe ccm wana maduka yao na Ufipa wana maduka yao? Hilo nilikuwa silijui.
Tatizo lenu mnakariri sana maafisa masoko wamesema mchele umeshuka bei Ufipa mnabisha!....Jana Mbowe naye amekariri lazima mfungwa atokee mlango ule ule alioingilia....hajiongezi kuwa mambo hubadilika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…