Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

Kweli neno uchumi limetumika vibaya kwenye mjadala huu! Sasa sijui isemeke tu neema imepanda kwa walaji? Maana kwa wakati huohuo mkulima anaumia kimtindo mpaka hapo soko litakapokaukiwa mchele....
Cc: maafisa masoko!
 
Nielekeze soko gani kuna bei hiyo niufuate kesho asb mkuu!
 
Swali, Serikali inamlinda vipi mkulima kuondakana na adha ya kuyumba kwa bei ya mazao?
 
Njoo vijiji vya kata ya Mwamala wilaya ya Nzega mkoani Tabora gunia ni 36,000 mwisho 45,000 na bado wanavuna hapo.

Duru zinadai kilo itafika hata 800 huko lakini hii wala siyo ishara ya uchumi kuimarika,Kuna watu wataumia.
Aisee kama mwamala bei hiyo sijui mambali,mbutu,nkindwa watauzaje
 
Kwa bei hiyo Naskia harufu ya shehena za Mchele wa plastic
 
Niliagza mtu akanichukulia huko Geita, kwa 900, nikautuma kwenda musoma jamaa wameniuzia huko kwa bei ya 1600, ni kweli umeshuka sana baadh ya sehemu wakuu
Hata Hiyo 900 kama ulichukua kilo nyingi Jamaa alipata hata miamia. Nimelima huko geita gunia eflu40 hadi najiuliza utapanda kweli? Hadi nafikilia kuuza shamba lenyewe. Wakulima tuna umia kweli
 
Hata Hiyo 900 kama ulichukua kilo nyingi Jamaa alipata hata miamia. Nimelima huko geita gunia eflu40 hadi najiuliza utapanda kweli? Hadi nafikilia kuuza shamba lenyewe. Wakulima tuna umia kweli
Kweli ndgu hali ni ngumu sana kwa mkulima wa kawaida
 
Ngoja nibane m.a.p umbu maharage yasishuke bei....maana yakishuka tu basi nitakula hasara ambayo sikuwahi kukumbana nayo.
 
Niliagza mtu akanichukulia huko Geita, kwa 900, nikautuma kwenda musoma jamaa wameniuzia huko kwa bei ya 1600, ni kweli umeshuka sana baadh ya sehemu wakuu
Hata Hiyo 900 kama ulichukua kilo nyingi Jamaa alipata hata miamia. Nimelima huko geita gunia eflu40 hadi najiuliza utapanda kweli? Hadi nafikilia kuuza shamba lenyewe. Wakulima tuna umia kweli
 
Duh 50% price sway ni zaidi ya lazy sway to weary blues.Mungu mnusuru mkulima.
 
Mpunga
Ngoja nibane m.a.p umbu maharage yasishuke bei....maana yakishuka tu basi nitakula hasara ambayo sikuwahi kukumbana nayo.
Mpunga imebidi niweke ghalani gunia elfu40 wata tumaliza ghalama za palizi dah, sielewi isee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…