Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

Kushuka kwa bei ya mchele ni kilio kwa mkulima. The world is unfair
Hiyo ni kweli mkuu,

Gharama za uzalishaj zmekua kubwa sn msimu huu.

Hakuna pembejeo wala mbolea za ruzuku,

Vipuri vya Trekta viliongezewa kodi, Service ya trekta imekua mwiba mkubwa.

Riba kwenye mabenki zimekua juu sana.

YAAN NI KAMA VILE SEREKALI IMEWATELEKEZA WAKULIMA.

HUU UCHUMI UNAOKUA KWA KUWAUMIZA ZAIDI YA 85% YA WATANZANIA WENZETU(wakulima)

SIDHANI KAMA UNA TIJA YOYOTE KWETU.
 
Ninavyoelewa mimi, kushuka kwa mazao ni maumivu kwa mkulima. Kwahiyo hii ndio kusema kuwa uchumi unakuwa kwa mkulima kuzidi kuwa masikini?!
 
Kuna ukweli flani kwenye hii taarifa. Japo hiyo bei imeshushwa sana. Bei ambayo ipo sokoni kwa sasa kwa masoko ya DSM ni wastani wa Tag 1450-1800 unategemea na quality ya mbele wenyewe.

Kweli baada ya week mbili hizo bei za 1300 zitakuwepo sokoni tena kwa mchele mzuri kabisa.

Mavuno kwa msimu huu ni mengi. Kuanzia Sengerema, Shinyanga kwa maana ya Shinyanga yenyewe,kahama, igunga.

Huko mpanda, Mbeya wilaya zote zinazolima mpunga. Kilombero na Ulanga kote huko ni neema kwa walaji ila ni maumivu kwa mkulima. Mchele utauzwa mpaka 1000.
 
Kudhibitiwa kwa walanguzi na madalali waliokuwa wananunua mazao kabla hsyajavunwa ni sababu mojawapo ya bei za nafaka katika ujumla wake kushuka!
Kwa wachumi wa kilimo kushuka kwa bei wakati wa mavuno ni kitu cha kawaida, na hili ndio kubwa hapo na sijaona analysis ya ziada inayoweza kukuruhusu wewe kusema uchumi umekuwa. Data yako very likely imetolewa na reliable source lakini interpretation yako sidhani kama iko sahihi.
 
Huyu ndugu yetu ni wa kumuhurumia bure tu.

Ndo maana kuna mdau humu alisema kua

Inawezekana huyu jamaa ni kula kulala kwa shemeji.

Kazi yake ni kutumwa tu supermarket.

WATU KM HAWA HATA HAWAJUI UCHUMI UNAKUAJE.
Mbona umepanic!
 
Mnaoshangilia hili basi mjue, mkulima ndiye anae umia.

Na lait mkulima angegoma,sijui hivi vibesi mngevitoa wapi.
 
Ni msimu wa mavuno mkuu
 
Wewe ni mbumbumbu au Tutusa maana unajua kabisa huu ni msimu wa mavuno na mchele ni mwingi na kushuka ni kukosa wanunuaji
 
  • Mkuu unazungumzia bei ya chenga za mchele au mchele wenyewe?.
  • Je kama mchele wenyewe una uhakika na ubora wake?
  • Kilo Tsh 1300 kwa kilo moja?
Mkuu pia ukiona mchele unauzwa kilo sh 1300 tambua kundi kubwa la wakulima wameumia wa zao hilo.
Tambua KUPUNGUZA IDADI YA WATU HAIMANISHI KUUA WALIO HAI LAHASHA BALI KUZUIA WATU WASIZALIANE OVYO. Namanisha huwezi kupima kukua kwa uchumi kwa kukandamiza wakulima ili bei dogo ya mazao kiashiria cha uchumi kupanda.
Unakumbuka baazi imeukwa kilo sh 200 je uchumi umepanda mkuu?
 
Wewe ni mbumbumbu au Tutusa maana unajua kabisa huu ni msimu wa mavuno na mchele ni mwingi na kushuka ni kukosa wanunuaji
Kwani miaka mingine haukosi wanunuaji?...wale wakenya na wazambia waliokuwa wananunua mazao kabla ya kuvuna wamejificha Ufipani?!!
 
Nenda Tandale utajua kama ni chenga au bismark!
 
Kwani miaka mingine haukosi wanunuaji?...wale wakenya na wazambia waliokuwa wananunua mazao kabla ya kuvuna wamejificha Ufipani?!!
Wewe si umezoea kula kwenu hujui kinachoendelea.
Wakenya hata mahindi sasa wananunua Zambia na Brazil bei ya mahindi hifai tena.
Mchele wanaonunua wametemana nao vikwazo ni vingi kuliko kuagiza kutoka Asia wameachana nao
 
Wewe si umezoea kula kwenu hujui kinachoendelea.
Wakenya hata mahindi sasa wananunua Zambia na Brazil bei ya mahindi hifai tena.
Mchele wanaonunua wametemana nao vikwazo ni vingi kuliko kuagiza kutoka Asia wameachana nao
Mkuu mimi huwa nakula kwa mkeo labda kanidanganya!
 
Nimegundua watanzania wengi ni wagonjwa wa akili!Yaani mtu kusema mchele umepungua bei unamtolea matusi makubwa jinsi hii?Ndio,nipo Kahama,mchele unaporomoka bei kiasi kwamba wiki iliyopita uliuzwa 2000 kwa kilo,na leo ninapoandika hapa unauzwa kwa 1300 kwa kilo.Na kuna watu wanatembeza mitaani wanauza hadi 1200!Kama wasiporuhusu wanunuzi toka Rwanda na Uganda,bei itaporomoka hadi 1000 kwa kilo au chini ya hapo.
Maana matajiri wa Uganda na Rwanda wanaweka stock kwa ajili ya kuuza wakati wa upungufu.
Hali hii inatokana na kuwepo mvua za kutosha ingawa historia inaonesha miaka inayofuata huwa na njaa.
 
bei hazijapungua mchele maharage ,mafuta yavkula sukari mafut ya petrol zote zina panda wasitudanganye...sisi tupo mtaani tunavitumia kila siku dar es salaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…