Nimegundua watanzania wengi ni wagonjwa wa akili!Yaani mtu kusema mchele umepungua bei unamtolea matusi makubwa jinsi hii?Ndio,nipo Kahama,mchele unaporomoka bei kiasi kwamba wiki iliyopita uliuzwa 2000 kwa kilo,na leo ninapoandika hapa unauzwa kwa 1300 kwa kilo.Na kuna watu wanatembeza mitaani wanauza hadi 1200!Kama wasiporuhusu wanunuzi toka Rwanda na Uganda,bei itaporomoka hadi 1000 kwa kilo au chini ya hapo.
Maana matajiri wa Uganda na Rwanda wanaweka stock kwa ajili ya kuuza wakati wa upungufu.
Hali hii inatokana na kuwepo mvua za kutosha ingawa historia inaonesha miaka inayofuata huwa na njaa.
It means ni mavuno yameongezeka na wala siyo uchumi umepanda! Shule nyingine wanafunzi hupita tu kuhesabu madarasa na wala siyo elimu bora!