Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

Nimegundua watanzania wengi ni wagonjwa wa akili!Yaani mtu kusema mchele umepungua bei unamtolea matusi makubwa jinsi hii?Ndio,nipo Kahama,mchele unaporomoka bei kiasi kwamba wiki iliyopita uliuzwa 2000 kwa kilo,na leo ninapoandika hapa unauzwa kwa 1300 kwa kilo.Na kuna watu wanatembeza mitaani wanauza hadi 1200!Kama wasiporuhusu wanunuzi toka Rwanda na Uganda,bei itaporomoka hadi 1000 kwa kilo au chini ya hapo.
Maana matajiri wa Uganda na Rwanda wanaweka stock kwa ajili ya kuuza wakati wa upungufu.
Hali hii inatokana na kuwepo mvua za kutosha ingawa historia inaonesha miaka inayofuata huwa na njaa.

It means ni mavuno yameongezeka na wala siyo uchumi umepanda! Shule nyingine wanafunzi hupita tu kuhesabu madarasa na wala siyo elimu bora!
 
Njoo vijiji vya kata ya Mwamala wilaya ya Nzega mkoani Tabora gunia ni 36,000 mwisho 45,000 na bado wanavuna hapo.

Duru zinadai kilo itafika hata 800 huko lakini hii wala siyo ishara ya uchumi kuimarika,Kuna watu wataumia.
Hata Mahindi bei iko chini sana na bado khali ni ngumu
 
Umeshuka kidogo coz supply imeongezeka maana huu ni msimu wa mavuno na mwaka huu mavuno hasa mpunga yameongezeka,hata mafuta huku Sumbawanga bei hazikupanda kama huko keingine
Sasa hivi ni masika sio mavuno
 
Unamaanisha uchumi au mfumuko wa bei? Unasemaje kuhusu mafuta ya kula ambayo sasa hivi lita 20 inauzwa kati ya sh. 64,000 hadi 70,000/=, kutoka 50,000/=?! Bei ya bidhaa moja ndiyo imeimarisha uchumi?
Kwahiyo kumkomoa mkulima ndiounaita uchumi kukua yeye bidhaa zake zinashuka mafuta yavyombo vyamoto na vifaa vya ujenzi vipojuu kuliko pia nauli na gharama za usafirishaji vipo juu hapa sisi wakulima hatuna letu nchii ikiwa tunashangilia mkulima kukabwa namaisha nihatari sana
 
Imeelezwa na maafisa masoko wa jiji la Dsm kuwa bei ya mchele imeshuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo na itaendelea kushuka hadi kufikia sh.1000 kwa kilo. Hali kadhalika bidhaa nyingine muhimu za chakula bei zimeendelea kushuka ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa uchumi. Source Eatv habari!
Hata mbaazi, dengu na choroko vimeshuka bei. Uchumi hoyeee!
 
Nimegundua watanzania wengi ni wagonjwa wa akili!Yaani mtu kusema mchele umepungua bei unamtolea matusi makubwa jinsi hii?Ndio,nipo Kahama,mchele unaporomoka bei kiasi kwamba wiki iliyopita uliuzwa 2000 kwa kilo,na leo ninapoandika hapa unauzwa kwa 1300 kwa kilo.Na kuna watu wanatembeza mitaani wanauza hadi 1200!Kama wasiporuhusu wanunuzi toka Rwanda na Uganda,bei itaporomoka hadi 1000 kwa kilo au chini ya hapo.
Maana matajiri wa Uganda na Rwanda wanaweka stock kwa ajili ya kuuza wakati wa upungufu.
Hali hii inatokana na kuwepo mvua za kutosha ingawa historia inaonesha miaka inayofuata huwa na njaa.
Sasa hapo Uchumi umeimarika kwa vigezo vya huyo mteja wako unaemtetea asinyeshewe matusi
 
Vijana wa lumumba fanyeni kazi za akili acheni propaganda za kindezi muda unwatupa mkono
 
kwa huyo bei wakulima watabaki kuwa maskini wa kutupwa.wenye faida watakuwa wale wale big exporters.
 
Njoo vijiji vya kata ya Mwamala wilaya ya Nzega mkoani Tabora gunia ni 36,000 mwisho 45,000 na bado wanavuna hapo.

Duru zinadai kilo itafika hata 800 huko lakini hii wala siyo ishara ya uchumi kuimarika,Kuna watu wataumia.
Hii bei wala si ngeni kipindi cha mavuno.. Ukizingatia kipindi hiki mvua zimenyesha kwa muda mrefu na kupelekea kuharibu barabara hivyo wengi wa wanunuzi ni humohumo kijijini wanaonunu gunia 20-100
 
Huku kwetu ni 950 kwa kilo
Toka walivyo zuia mchele kuuzwa nje ya nchi,waganda wakarudi makwao kwa sasa ni 950 kwa kilo[emoji1321]
 
Imeelezwa na maafisa masoko wa jiji la Dsm kuwa bei ya mchele imeshuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo na itaendelea kushuka hadi kufikia sh.1000 kwa kilo. Hali kadhalika bidhaa nyingine muhimu za chakula bei zimeendelea kushuka ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa uchumi. Source Eatv habari!
Hivi bei ya mbaazi ilivyoshuka kwa asilimia 90 kutoka 2000 hadi 200 maana yake uchumi uliimarika? Watu hawana pesa, hivyo wanalazimika kununua kidogo kidogo sasa mzigo unabaki mkubwa kwa mkulima au muuzaji inabidi auze kwa bei ndogo ili afidie gharama za shambani na kulipa mkopo. Wakulima wanaumia sana miezi hii. Mimi sijaamini kama nimeuza debe la mahindi elfu tatu. Yani mwaka jana ilikua 13000 sasa nilikua na mzigo mkubwa na sina pa kupeleka.
 
naona mtoa uzi kaandika ili apongezwe ila ukweli ni kwamba mchele haujashuka hata senti labda unauziwa mpungaa mkuu kutoka shambani na sii dukani

Mkuu naandika sasa hivi MWANZA BEI YA MCHELE NI 950 KWA KILO
FIKA MABATINI UJIONEE,TUNASHKURU KWA MUNGU BEI HII KUSHUKA KUTOKANA NA MFUNGO WA RAMADHANI TUNAO JIANDAA NAO WIKI IJAYO[emoji1321]
 
Back
Top Bottom