Uchumi wa Frame Tanzania

Uchumi wa Frame Tanzania

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Uchumi wa Frame unashika kasi sana Tanzania, ni Frame juu ya Frame, ni frame ukikata kona ni frame ukinyosha ni frame.

Hii nchi na hisi uwezo wa wetu wa kufikiria nahisi usha fikia tamati yake, nchi kwa sasa iko kwenye uchumia wa frame, si Jeshi la Police, Si Jeshi la Wananchi, Si makanisa yaani wote wanawaza Frame, Frame zinaoteshwa kama uyoga, miji imejaaa frame. Halimshauri, ni frame, Majiji ni Frema, Manisapaa zinawaza Frame.

Sasa wameona mjini hakutoshi, Frame zimehamia hadi kwenye makambi ya jeshi, Vituo vya Police, Mitaani maeneo ambayo ni kwa ajili ya Makazi kumejaaa Frame.

Tunako elekea Frame zitakuwa nyingi kuliko watu kama speed itakuwa ni hii hii ya sasa.

Je, hatuna Idea zingine nje ya Uchumi wa Frame?

Tunaandaa frame za kusapoti uchumi wa China make asilimia 99 ya hizo frame lazima ukutane na products za China.
 
Nimejikuta nacheka tu nimepita mtaa fulani hivi mazingira ya eneo lile ni tulivu sana nyumba nyingi zina fensi ila kuna mtu alinunua eneo kubwa mwaka jana kapiga frem zaidi ya 15 tangu mwaka jana mpaka leo ni frame mbili tu ndio zinawapangaji sijui boss aliwaza nini ukiangalia eneo lenyewe haieleweki wateja wanatoka wapi maeneo yapo kimya.
 
Nchi hii Watanzania wanapenda kuigana pia fremu ni ujinga na kipimo duni, mie kilichonichosha zaidi Hadi jwtz Lugala walikata ile miti mingi wakajenga frem hii ni aibu hivi jeshi kweli ubunifu umeishia kujenga frem tu wakati Kwa wenzetu majeshi huongoza ubunifu na hizo frem wanazojenga vipi ma jasusi wa nchi jirani wakikodi Kwa masilahi ya uchunguzi.

In short nchi hii watu wanatumia asilimia Moja ya ubongo kufikiria.
 
Nimejikuta nacheka tu nimepita mtaa fulani hivi mazingira ya eneo lile ni tulivu sana nyumba nyingi zina fensi ila kuna mtu alinunua eneo kubwa mwaka jana kapiga frem zaidi ya 15 tangu mwaka jana mpaka leo ni frame mbili tu ndio zinawapangaji sijui boss aliwaza nini ukiangalia eneo lenyewe haieleweki wateja wanatoka wapi maeneo yapo kimya
Watanzania tunapenda kuigana vipi Sheria za mipango Miji maana sikuhizi huwezi jua soko ni lipi na makazi ya watu ni yepi
 
Nchi hii watanzania wanapenda kuigana pia fremu ni ujinga na kipimo duni, mie kilichonichosha zaidi Hadi jwtz Lugala walikata ile miti mingi wakajenga frem hii ni aibu hivi jeshi kweli ubunifu umeishia kujenga frem tu wakati Kwa wenzetu majeshi huongoza ubunifu na hizo frem wanazojenga vipi ma jasusi wa nchi jirani wakikodi Kwa masilahi ya uchunguzi.
In short nchi hii watu wanatumia asilimia Moja ya ubongo kufikiria
Umewaza km Mimi kila nikipita pale nasema mhhh these people are not serious taasisi nyeti km hiii wanavutia muingiliano wa watu manake nimeona hadi pub pale ni hatari Sana hata ni kujikwamua au kujiongezea njia nyngne ya kipato hpn aisee
 
Kali kuliko Yote ni kitendo cha JW kuachana na project za kutunza mazingira na wao wa kubebwa na muhemuko ya Uchumi wa Fremu , wamepafyeka pale Lugalo kama mtu aliyetoka kusafisha sehemu zake za siri, pamebaki pameachama tu pakisubiri wapangaji wakapange ili waendeleze Uchuni wa Fremu.
 
Back
Top Bottom