Uchumi wa Kenya wazidi kuelekea kaburini kwa kasi

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Taarifa ya Benki kuu ya Kenya inaonyesha kwamba, Kenya inapoteza nguvu ya kupambana katika biashara katika EAC kutokana na gharama kubwa za uzalishaji nchini, hii imesababisha Kenya kuwa mnunuzi zaidi wa bidhaa kutoka Kenya na Tanzania, kuliko kuwa muuzaji.

Hii inaonyesha ni jinsi gani " Manufacturing sector" ya Kenya inavyoporomoka ukilinganisha na zile za Kenya na Tanzania, ambazo kwa sasa zinakua kwa kasi kubwa kutokana na kutumia tehnolojia ya kisasa ambayo inapunguza gharama za uzalishaji.

Ikumbukwe kwamba, Kenya ilikua nchi ya kwanza kupata maendeleo ya viwanda katika ukanda huu, pale ilipoamua kuegemea wazungu na kuwasaliti waafrika katika kipindi cha vuguvugu la ukombozi wa Africa, lakini baada ya uwanja wa biashara kuwekwa sawa kwa nchi zote za EAC, imeonekana wazi kwamba manufacturing sector ya Kenya haina uwezo wa kupambana na zile za Tanzania.
 
Kwa hiyo ripoti Kenya inaauza bidhaa mingi Tanzania kuliko venue inanunua,lakinini kwa kueneza propaganda hujamboo wewe kichaa
Kenya exports to Tanzania-15bn
Kenya imports from Tanzania-13bn
Kenya export to Uganda- 30bn
Kenya imports fro Uganda-13bn
Bado Kenya ni king wa east Africa
 
Kwa hiyo ripoti Kenya inaauza bidhaa mingi Tanzania kuliko venue inanunua,lakinini kwa kueneza propaganda hujamboo wewe kichaa
aliyeelewa huu mwandiko anisaidie kunielewesha kilichoandikwa
 
Joto hii report haiongei kuhusu T.Z inaongea kuhusu Africa. Usiingize T.Z kwa kila kitu
 
Kichaa wewe, inamaana hiyo article inayolalamika kwamba export ya Kenya inazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka kwako haina maana?. Sasa hivi Kenya inanunua zaidi kuliko inavyouza nchi za nje, hiyo ni dalili kwamba uchumi unasambaratika, wewe hilo huoni kama ni muhimu eti kwasababu bado inauza zaidi kwa Tanzania.
 
Joto hii report haiongei kuhusu T.Z inaongea kuhusu Africa. Usiingize T.Z kwa kila kitu
Mimi nimesema uchumi wa Kenya unapoeomoka kwasababu sasa hivi Kenya inanunua zaidi kuliko inayouza ndani ya Africa. Ripoti hii imezitaja Tanzania na Uganda kuonyesha kwamba, sasa hivi Manufacturing sectors za Tanzania na Uganda zinazidi kufanya vizuri kushinda ile ya Kenya kutokana na gharama za uzalishaji za Kenya kuwa juu, hivyo kufanya bidhaa za Kenya kushindwa kupambana na bidhaa za Uganda na Tanzania.
 
Mwenzako kakujibu freshy...hii habari haihusianibna tanzania...manake tukiileta afrika mashariki bado mko chini
 
Lkn bado mna import vitu vingi kutoka kenya kuliko mnavyo export
 
Mwenzako kakujibu freshy...hii habari haihusianibna tanzania...manake tukiileta afrika mashariki bado mko chini
Tanzania imetajwa Mara 3 katika hii ripoti, kama Tanzania haihusiki kwanini mnaitaja kila Mara, hasa pale Kenya inapofanya vibaya?, tena ripoti inaonyesha kwamba, Tanzania manufacturing sector inafanya vizuri kuliko ile ya Kenya, kwamba hiyo ni miongoni mwa sababu kubwa ya Kenya kupoteza" competitive advantage' hivyo kushindwa kuuza kwa wingi bidhaa zake, na kupoteza ajira za viwandani.
 
Lkn bado mna import vitu vingi kutoka kenya kuliko mnavyo export
Sababu nimekuambia, ninyi mlikua mnabebwa na wazungu kuanzia 1963 hadi1990s. Katika kipindi hiki, Kenya ilipokea mitaji mikubwa kutoka nchi za kibepari iliyowezesha mjenge viwanda Vingi, pia bidhaa zenu zilipata soko zuri huko kwao baada ya Kenya kuchagua kuwaunga mkono wakoloni waendelee kuwatawala na kuwakandamiza waafrika.

Tanzania tulitengwa na kuwekewa vikwazo na nchi tajiri za wazungu, bidhaa zetu za KILIMO walizisusia kama njia ya kutulazimisha kuachana na juhudi za kuwakomboa waafrika.

Kuanzia 1990s, hali ya siasa ya duniani imebadilika na kuweka uwanja wa biashara katika "level" sawa, matokeo yake ni ile tofauti ya Kenya na Tanzania katika manufacturing sector inakwisha kwa kasi sana. Mlitegemea kubebwa na wazungu, sasa hivi wazungu hawapo mbaporomoka kwa kasi wakati sisi tunapanda kwa kasi.
 

Incase haukusoma vizuri, hivi ndo ripoti ulioileta inasema kuhusu Tanzania na Uganda.


Orders from Kampala have dropped to Sh30.77 billion in the January-June 2019 from recent highs of Sh34.51 billion in 2013, the statistics kept by the CBK shows.
Half-year exports to Tanzania have dipped to Sh15.79 billion this year from Sh21.73 billion five years ago, while those from DRC have dipped to Sh6.86 billion from Sh10.12 billion.
Imports from Uganda, on the other hand, have doubled to Sh13.95 billion in June 2019 from Sh5.14 billion in 2014, while Tanzania’s has grown to Sh12.95 billion from Sh8.34 billion.



--------------------------------------

So Uganda exported 15.95B and imported 30.77B from Kenya
Tanzania exported 12.95B and imported 15.79B from Kenya.

Kwahivyo wewe mtanzania uache kujiingiza kwa hoja ambayo hata haikulengi, mwanzo sababu ya exports za Kenya kuja huko Tanzania kupungua si kwasababu ya viwanda vinavyojengwa huko, export zimepungua kwasababu rais wenu alianza ku apply protectionist measures kama kuzulia maziwa, pipi, biskuti na mengineyo, kama ingekua mmefungua soko huru kama vile kitambo ingekua tumejaza bidhaa zetu huko. Angalau Uganda tunajua ni kwamba viwanda vyao ndo vimeongezeka manake wako na soko huru ambalo linaruhusu bidhaa za kenya kuingia bila shida lakini licha ya hivyo, bado eports zetu zinashuka kwasababu zilebidhaa tulikua tukiwauzia sasa wanaweza kujitengenezea wenyewe..

Kule ambako kuna competition kwa Kenya hapa Africa ni ndani ya soko huru la COMESA ambapo Egypt anazidi kutuchapa game, kila kitu ambacho tuna manufacture hao wana uwezo wa ku manufacture mara mbili zaidi tena kwa bei ya chini zaidi.... Juzi baada ya kusoma nyuma ya Tv yangu vizuri nilihuzunika kidogo baada ya kugundua Tv yangu ya LG imeandikwa "Made in Egypt" si eti kwamba nilikua nawaonea dhiki, lakini nilikua najiuliza kama wanaweza kutengeneza products za LG inamaanisha wameanza ku replace China , kwanini pia sisi tusifanye hivyo??

Mbali na wachina wanaojaza bidhaa zao za bei ya kutupa huku Africa kusababisha bidhaa zetu ziwe hazinunuliki, Hao kina Egypt ndo Nchi za Africa zinazo sababisha intra Africa exports yetu ya Kenya izidi kushuka, Usijarubu kuingiza Tanzania kwa huo mjadala..

Ndani ya Comesa members, Egypt exports $2.4B followed by Kenya $1.6B



Taarifa ulioileta kutoka kwa business daily inasema total exports za Kenya za first 6 months ilikua sh107B kumaanisha in 12 months itakua amngalau sh200B.. Ukiangalia hio screenshot hapo inaonyesha mwaka jana biashara ndani ya COMESA, Kenya ili export sh160B to comesa countries, kumaanisha only sh40B was exported by Kenya outside of Comesa.... So its inside COMESA region where It really matters to Kenya cause this is where 80% of our exports to Africa go to! Usihusishe Tanzania na haya mambo!
 
Sidhani kama atarudi huku mleta mada
 
Hahahaha, sasa kama Uganda ambao manufacturing sector yao inakua kwa taratibu sana ukilinganisha na Tanzania, wameweza kuzuia bidhaa za Kenya kuingia Uganda kutokana na kuzalisha bidhaa zao wenyewe, vipi kuhusu Tanzania ambayo Manufacturing sector yake ni the fastest growing in the EAC?.https://www.tanzaniainvest.com/industry/manufacturing-growth
Tunawapiga kutoka kila pande, lazima mkubaliane na hali halisi.
 
Umesoma content kweli? Ama we umesoma tu heading ukamua ukimbie nayo huku?
 
Sidhani kama atarudi huku mleta mada
Jamaa mnatapatapa tu, lakini hiyo article imezungumza kila kitu kuhusu kushuka kwa manufacturing yenu na kupanda kwa Tanzania na Uganda. Ukweli mwengine ndio huu ninakuwekea.

Gharama za uzalishaji Kenya zipo juu sana, bidhaa zenu haziwezi kuhimili kushindana. Baada ya miaka kadhaa, kampuni zote za Kenya zitaamua kufunga uzalishaji na kuhamia Tanzania au Uganda, kama walivyofanya makampuni ya USA kuhamia China, hadi Trump alipoanzisha ugomvi wa kibiashara na China ili kuzuia makampuni na mitaji kukimbilia China. Sasa hivi zaidi ya makampuni ya Kenya 500 yapo Tanzania, ikifika mwishoni mwa 2020, hii idadi inakadiriwa kuzidi 1000.
 
Nowadays your threads are turning back on you.
 
We still sell more to you, you only sell to us raw materials as we sell to you manufactured goods.
Which manufactured goods do you sell to Tanzania?
We sell to you
1) Tiles
2) Konyagi
3) Energy drink
4)Wines (Dompo)
5) Cooking gas
6)White dent toothpaste
7)Iron sheet
8)Fruit juices
9)Safari &Kilimanjaro beer
10)Electric transformers
11)Electric poles
Just few to mention................
 
Sasa unafurahia sana kuona nyumba kubwa ya jirani ikiungua kwa moto mkali sana si ndio? Wewe mwenyekiti wa kamati ya roho mbaya utakufa kutokana na wivu siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…