kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kunyonga wahujumu uchumi ni nyenzo muhimu sana ya uchumi wa kujitegemea. Hakuna mtu wala taasisi inayotakiwa kuwa juu ya sheria, kila mtu lazima aitumikie sheria.
Huko tunakoelekea hakutakuwa na misaada isiyokuwa na madhara kwetu maana kila nchi itakuwa inalalamikiwa na raia wake kuhusu hali za maisha yao. Hivyo, misaafa nafuu na isiyokuwa na mitego itapungua sana, hivyo tunachotakiwa sasa ni kuanza mkakati kabambe wa kuimarisha utawala wa sheria kwa kuanzia na katiba bora na bora na uwezo wa mahakama zetu kwenye kutoa haki.
Tuwe na katiba ambayo kila mtu anashitakika kwa mujibu wa makosa yake aliyoyafanya. Tuanze kukuza na kutumia uwezo wetu katika kujiletea maendelea, na hili halitawekana bila kuwa na serikali za majimbo, maana jimbo lina uwezo mkubwa wa kuzitambua na kuzitumia kikamilifu rasilimali zake zote zilizomo ndani ya jimbo kwa maendeleo ya wanajimbo na taifa kuliko hii ya sasa ya nchi yote kutawaliwa kutoka Dodoma.
Namna ilivyo sasa kuna watu wanatuibia sana lakini hatuna cha kuwafanya, wana kinga madhubuti ya kutoshitakiwa na wengine ni wezi tu lakini sheria iko "mifukoni" mwao.