Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Watanzanka kwa ku exaggerate mambo hamjambo. Takwimu za kula mlo mmoja kwa sababu za uchumi mmbaya umezitoa wapi? Umapima vipi mdororo wa uchumi wa Tanzania?Sasa ni dhahiri kwamba maisha ya Watanzania yamekuwa magumu kuliko awamu zote zilizopita , familia nyingi sasa zinakula mlo mmoja tu , huku Maharage yakiwa Chakula Muhimu kabisa .
Ni kweli kwamba Mambo ya Utekaji , kuokota viroba vya maiti baharini na kwingineko na ubambikaji kesi za uongo , zilizoitwa za uhujumu uchumi na Utakatishaji fedha kwa sasa yamepungua (Hayajaisha) , lakini maisha ya Raia yamekuwa kizungumkuti , hali ni mbaya mno ! Mzunguko wa pesa ni kama hakuna , watu wamekuwa masikini mno ! Chakula Kikuu kimekuwa Mihogo na Maharage .
Hata sisi tuliobarikiwa kidogo ni kama tuko matatani , tunapigwa mno mizinga na wenye uhitaji kuliko kipindi chochote kile , shida ya nchi hii ni nini ?
Sasa katika hali kama hii ya sasa nchini Tanzania ni Nani alaumiwe , Ni Rais wa Nchi au Waziri wa Fedha ?
Mimi binafs naona mabdidiliko chanya toka Rais Samia amechukua nchi kama ifuatavyo;
Watu masokoni wanajaa kununua vyakula, petrol station magari yanaingia na petrol station zinaendelea kujengwa, mabasi ya mikoani yanajaza abiria wanaokwenda na wanao rudi. Kariakoo sasa hivi hakuna matangazo ya "Fremu inapangishwa". Mitaani sijaona mtanzania anakufa kwa njaa. Ujenzi wa Nyumba na magorofa kwa Dar es Salaam unaendelea kila mahali na ukienda Benki unakutana na angalao wateja wanne wako foleni.
Hali ya uchumi ni nzuri sana wakati huu wa Samia kuliko wakati wa Dikteta