SoC02 Uchumi wa Tanzania 2022

SoC02 Uchumi wa Tanzania 2022

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 18, 2022
Posts
11
Reaction score
4
Uchumi unaweza kuelezwa kwa namna mbalimbali. Uchumi ni jumla au mjumuisho wa shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji katika nyanja zote za maisha ya jamii au taifa husika. Uchumi ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali zinazokubalika katika jamii husika.

Mara nyingi uchumi hutazamwa kwenye ngazi za mtu mmoja mmoja, eneo, kijiji, taifa au dunia kwa ujumla. Uchumi huendeshwa na mfumo wa uchumi husika uliochaguliwa na kukubalika na jamii husika. Kuna aina mbalimbali za mifumo ya uchumi kama vile uchumi wa kijamaa (socialist economy), uchumi wa kibepari (capitalist economy), na uchumi mchanganyiko (mixed economy) kama huu ambao unatumika hapa Tanzania.

Tangu kupatikana kwa uhuru toka kwa wakoloni wa kiingereza, nchi ya Tanzania imepitia katika hali tofauti tofauti za uchumi ambayo imepelekea mabadiliko makubwa katika nyanja za uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa na huduma mbalimbali. Si hivyo tu, uchumi wa Tanzania umeathiriwa pia na mabadiliko katika mifumo ya uchumi wa nchi nyingine ambazo zinashirikiana pamoja kwa namna moja au nyingine. Hii ni kwa dhana ya kwamba Tanzania sio kisiwa kwamba ijitenge na isishirikiane na nchi nyingine katika nyanja mbalimbali za maisha.

Mabadiliko katika sekta za sayansi, teknolojia, utawala, biashara, kilimo na elimu yamepelekea uchumi wa Tanzania kupitia hali mbalimbali ikiwemo kupanda na kushuka. Hii inathibitishwa katika nyanja za ajira, mifumuko ya bei za bidhaa, viwango vya fedha, sera na miongozo mbalimbali inayoongoza taifa. Kuendana na hayo yote hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa katika kuchochea mabadiliko kwenye nyanja muhimu na nyeti ya uchumi katika wakati huu wa sasa. Kwa lengo la kuhakikisha kukua na kuendelea kwa uchumi wetu.

Mosi; Kutumia fursa ya uwepo wa uchumi wa kidijitali (digital economy) na utandawazi. Uchumi wa kidijitali ni mtandao wa kimataifa wa shughuli za kiuchumi, miamala ya kibiashara na mwingiliano wa kitaalamu unaowezeshwa na teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT).

Uchumi wa kidijitali huangazia fursa na hitaji la mashirika na watu binafsi kutumia teknolojia kutekeleza majukumu yao vyema, haraka na mara nyingi tofauti na hapo awali (Daily News, 2022). Tupo katika karne ya 21 inayoongozwa na mapinduzi na maboresho ya kisayansi na teknolojia katika nyanja zote za kimaisha kama vile kijamii, kiuchumi,kisiasa na katika nyanja zote muhimu za kimaisha. Pia utandwazi umeongezea kiwango kikubwa cha muingiliano wa jamii na jamii taifa na taifa jingine.

Ni wakati sasa kutumia mapinduzi haya kwa mlengo wa kukuza na kuendeleza uchumi wa Tanzania. Dunia kwa sasa inaelekea katika ulimwengu wa kidijitali zaidi hivyo sisi kama watanzania tusiwe nyuma katika fursa hii kwa kuufanya uchumi wetu uwe wa kidijitali. Hii ni kwa nyanja na sekta zote muhimu katika kukuza na kuendeleza taifa letu pendwa la Tanzania. Japokuwa mapinduzi na maboresho haya yamekuja kwa faida na athari zake, tahadhari zinapaswa zichukuliwe ili yasilete athari hasi katika shughuli zetu za kiuchumi, kijasiriamali na kibiashara.

Pili, kuongeza jitihada na maarifa katika kufanya kazi. Ukweli ukibainisha kuwa, hakuna nchi yoyote iliyoendelea kiuchumi kwa wananchi wake kutofanya kazi kwa jitihada na maarifa yenye malengo ya juu. Shime watanzania ni wakati sasa wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na taifa kwa ujumla.

Pia ni wakati sasa watanzania tubadilike kwa kuachana na tabia au mienendo inayokwamisha maendeleo yetu na taifa letu kwa ujumla. Ingawa ugumu upo katika mazingira ya kufanya kazi, ni wakati sasa wa kutafuta namna bora ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Pia, watanzania tupunguze tabia ya kuilalamikia serikali , uvivu na kukatishana tamaa badala yake tutumie majukwaa yaliyopo kutatua changamoto zinazotukumba kwa juhudi za awali zinazowezekana. Iwe katika ajira rasmi au kazi zingine ambazo sio ajira za moja kwa moja kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo. Hii iendane pia kudai haki kwa taratibu na misingi iliyowekwa na kukubalika.

Tatu, taasisi zinazotoa huduma za kifedha, kibiashara na ujasiriamali zipunguze riba na masharti mengine yanayokwamisha kukua kwa mazingira ya kibiashara hapa nchini. Imekuwa ni kawaida kupata ugumu kwenye kupata huduma hizi ambazo ni moja kati ya misingi muhimu katika kukuza na kuendeleza uchumi. Ni vyema taasisi hizi ziangalie namna mpya na bora zaidi kwa kutoa huduma zake kwa wanachi hasa wananchi wa chini ambao ni wengi na wana uhitaji mkubwa wa huduma izo kwa shughuli. Mathalani, taasisi za kifedha kama vile benki zipunguze riba na kulegeza masharti ya kupata mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Hii itasaidia wengi kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza au kuanzisha biashara na shughuli nyinginezo za kiuchumi.

Nne, ni wakati sasa kwa serikali kupitia watendaji wake na taasisi zake kutengeneza mazingira bora na wezeshi ya kukuza na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kibiashara. Hii inajumuisha kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kupata ajira na kujiajiri, kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi, kupunguza utitiri wa kodi, tozo na ushuru wa aina mbalimbali zinazoumiza au kukwamisha maendeleo kwa wananchi. Kukaribisha wawekezaji wengi zaidi kuwekeza nchini kwetu kwa manufaa mapana ya uchumi wetu hii iendane na kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa hao wawekezaji.

Mwisho kabisa lakini sio kwa umuhimu, serikali iwekeze katika miradi mbalimbali ili kuhakikisha taifa la Tanzania linajitegemea kwa asilimia kubwa. Hii ni kwa nyanja zote za maisha kama taifa lililojipatia uhuru wake kamili. Mfano mzuri unaweza kurejewa kipindi cha janga la UVIKO-19 na wakati huu wa mgogoro kati ya Urusi na Ukraine ambavyo vyote kwa pamoja athari zake zimeonekana kwenye uchumi wetu kama taifa kama vile mifumuko ya bei za bidhaa mbalimbali, kuongezeka kwa gharama za usafirishaji.

Hitimisho: Makala hii inahitimisha kwa kusisitiza kila upande na ngazi zote iwe kwa mtu mmoja mmoja, taasisi binafsi na za kiserikali pamoja na serikali kwa ujumla kutimiza wajibu wake kwa ubunifu, ubora na kiwango kwa lengo moja ambalo ni kuhakikisha uchumi wetu unakua na kuendelea licha ya changamoto mbalimbali zilizopo. Shime watanzania, ujenzi wa taifa letu ni wetu wenyewe na sio mtu kutoka nje. Tuanze kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja, katika jamii zetu na hatimaye kwa taifa.
 
Upvote 2
Hili ni shindano la uandishi kwa kutumia akili zako siyo Ku copy kutoka google, pia binafsi Mimi sijakuelewa andiko lako linasifia au lina maanisha nini, point zako za kuunga unga hazieleweki zina base wapi.
 
Hili ni shindano la uandishi kwa kutumia akili zako siyo Ku copy kutoka google, pia binafsi Mimi sijakuelewa andiko lako linasifia au lina maanisha nini, point zako za kuunga unga hazieleweki zina base wapi.
Ya
Hili ni shindano la uandishi kwa kutumia akili zako siyo Ku copy kutoka google, pia binafsi Mimi sijakuelewa andiko lako linasifia au lina maanisha nini, point zako za kuunga unga hazieleweki zina base wapi.
1.Sijakopi google ila baadhi ya idea nimejifunza huko 2.andiko linahusu mabadiliko chanya katika uchumi wa Tanzania
 
Kwa mujibu wa takwimu za Nguvukazi na soko la ajira Tanzania (Bara na Visiwani) mwaka 2021/2022 lipo jambo ambalo tunapaswa angalau kuona jitihada na kulisema kwani ni hatua ya kuonesha jitihada za makusudi kufikia lengo.

Takwimu zinaonesha umasikini Nchini Tanzania ulishuka kutoka asilimia (34%) mwaka 2007 hadi asilimia (26%) mwaka 2018 kiwango hicho kilihesabika kuwa ni kidogo ukilingnisha na nchi nyingine jirani kama vile; Burundi(65%), Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (64%), Kenya (36%), Malawi (52%), Msumbiji (46%), Rwanda(38%), na Zambia (54%) isipokuwa nchi ya Uganda ndiyo iliyokuwa na asilimia (21%). Jambo hili Kwa hakika tunapaswa kuona jitihada na kusema licha ya uwepo wa changamoto nyingine nyingi Kwa sababu umasikini ni moja ya maadui wakubwa watatu wa Taifa hili lakini pamoja na hayo bado tunahitaji jitihada za makusudi kuendelea na mapambano dhidi ya umasikini na madhila yake.

Pamoja na hayo takwimu zinaonesha bado hatufanyi vizuri kama Taifa katika meneo mengi ambayo yanaweza kuruhusu adui ( umasikini kujipanga upya). Baadhi ya maeneo hayo ni biashara za mipakani Tanzania inashika nafasi ya 182, ulipaji Kodi nafasi ya 165, Uanzishaji biashara nafasi ya 162, Vikwazo kwenye Uutoaji wa vibali n nafasi ya 149, Ukuzaji wa raslimali watu (Human Development Index (HDI) nafasi ya 163 kati ya 189 mwaka 2020.

Kinachotupa matumaini ni jitihada zinazochukuliwa na Serikali iliyopo madarakani. Hili linatupa hamsa kuwa takwimu zijazo tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom