Uchumi wa Tanzania kuwa hivi walaumiwe wataalamu wa uchumi wa Kitanzania

Uchumi wa Tanzania kuwa hivi walaumiwe wataalamu wa uchumi wa Kitanzania

Ntiley

Senior Member
Joined
Oct 23, 2017
Posts
196
Reaction score
250
Habari za Kazi wana JF,

Kama somo linavyojieleza nimekaa na kutafakari sana juu ya uchumi wa Nchi yetu Tanzania. Baada ya kupata Uhuru Mwl Nyerere alijitahidi sana kupambana kuiweka Nchi yetu katika uchumi wa viwanda.

Alipeleka vijana wa kitanzania zaidi ya 140 Nchini India kwenda kujifunza mambo yahusuyo viwanda Na kuja Nchini Na ujuzi WA kutosha wa kuanzisha Na kusimamia viwanda Nchini

Uchumi wa Nchi yetu uliimarika hadi Nchi yetu ikamudu kujenga viwanda vingi Nchini , Na kuzalirisha bidhaa mbali mbali tulizalisha mwenyewe Na kuziuza Nchini Na Nje ya Nchi

Kipindi hicho Nchi ilikuwa Na wataalam wachache mno lakini Nchi ilifanikiwa Sana hadi kuweza kuwalipia Elimu bure wanafunzi, madaftari ,kalamu ,nauli nk vyote serikali ilimudu kuhudumia

Tanzania ya leo tumempata rais Mwenye maono makubwa sana tena zaidi ya rais wa awamu ya kwanza tumekalia mambo ya kiutawala tu na hao wanasiasa wasio wazalendo wanatuletea hoja za ovyo humu kwenye mitandao tumeshindwa kutumia fursa hii.

Tanzania ya leo inao wachumi wenye Elimu Na ujuzi Mkubwa sana lakini sijui wamelogwa? Hakuna wanachoweza kufanya hata kuweza kusaidia Nchi yetu tukafanikiwa katika Sera yetu ya viwanda?

Hakuna mijadala humu jukwaani ya maana sana hata watanzania walio wengi wamekalia kupost Picha za ajabu ajabu ,kuanzisha mada za kisiasa tu,je hatuna watanzania walio Na siasa za kiuchumi wakasaidia kuelemisha jamii ya kitanzania kutumia fursa hii?

Naomba maoni ushauri tuelekeze kwa Serikali yetu pendwa jamani Nchi ni yetu wote tuijenge Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom