Uchumi wa Tanzania unaelekea shimoni

Uchumi wa Tanzania unaelekea shimoni

uswaa

Member
Joined
Mar 4, 2014
Posts
55
Reaction score
20
Duuu inasikitisha na kufadhaisha leo hii
KWA TREND HII YA BOT; UCHUMI WA TANZANIA ULALE MAHALI PEMA PEPONI.!

Siungi mkono hoja ya Benki kuu (BOT) kufuta noti ya Sh.500/= na kuifanya sarafu. Huu ni wendawazimu mkubwa katika sekta ya uchumi "the most unpleasant economic decision" kwa sababu zifuatazo;

MOSI; fedha yoyote inapobadilishwa kuwa sarafu kutoka shillingi ni kuishusha thamani. Hii ni kwa sababu kiuchumi inabadilika matumizi na kuanza kutumika zaidi ktk sekta ya uchumi mdogo km wa wauza njugu mtaani, mama lishe, na maeneo mengine yasiyozalisha sana kiuchumi (less productive sector).

Maeneo yenye uzalishaji mkubwa (lead productive sector) yatashindwa kuitumia fedha hii kwa kuwa tu ni ya sarafu. Kw mfano kuanzia sasa haitakua rahisi kukuta sarafu hizi za 500/= maeneo kama Airport, Migodini au Supermarket.

Hiki ni kiashiria cha kushuka kwa thamani kwa fedha hiyo. (Indicator for currency devaluation).

Hivi hatujiulizi kwanini Marekani hadi dollar moja ni ya noti sisi 500/= tunaweka sarafu?? Dollar moja ina single digit lakini ipo kwenye noti, sisi tunalazimisha kuweka 500 kwny sarafu wakati ina tripple digit. Tunaforce Galloping inflation.

PILI; unapotengeneza sarafu ya pesa kubwa ina maana sarafu zinapotea na kujiondoa ktk mzunguko wa fedha. So tutegemee siku si nyingi sarafu za sh.100/= na sh 200/= hazitakuwepo tena mtaani.

Ikifikia hatua hii ujue nchi imeanza kuyumba kiuchumi na mfumko wa bei umevuka kiwango cha kawaida (extention from Moderate inflation to Galloping inflation).

Wenzetu Kenya hadi sarafu ya sh.10 inatumika. Ukienda Nairobi, Mombasa au maeneo mengine ya Kenya utata watoto wakinunua madafu, ice cream au matunda kwa sh.10.

Hapa kwetu sarafu ya sh.10 ilikufa na Nyerere. Ya sh.5 ikaenda na Sokoine. Ya sh.20 na 50 zimemfuata Kawawa. Sasa benki kuu wanalazimisha sarafu ya sh.100 na ya sh.200 zikamfuate Karume mahali pema peponi. Noti ya sh.1,000/= nayo inakaribia kwenda ahera maana BOT wameleta sarafu ya sh.1,500/=.

TATU; BOT kuwa wametoa hoja mufilisi kuwa wamefuta noti ya Sh.500/= na kuireplace kwa sarafu baada ya kugundua noti hiyo inachakaa haraka sn na inadumu kwa muda mfupi mno kwenye mzunguko.

Hoja hii ni mufilisi kwa sababu solution ya noti kuchakaa mapema si kureplace sarafu bali ni kuimarisha noti hiyo kwa kuitengeneza kwa material imara zaidi.

Hivi noti ya 10,000/= nayo ikichakaa mapema BOT wataleta sarafu instead?? Huu ni wendawazimu.

Mojawapo ya sifa za fedha imara ni uwezo wa kukaa kwny mzunguko muda mrefu (durability). Sasa fedha inapopoteza durability dawa sio kubadili muundo wake (changing of currency format is not a solution for impermanency)

Lakini hata hivyo BOT wameonesha hawakufanya utafiti wa kina kabla ya kuleta sarafu ya 500/=. Wanasema zinachakaa haraka ukilinganisha na noti nyingine. Hii ni hoja dhaifu sana kutolewa na mtu anayejiita Profesa wa uchumi Benno Ndullu.

Yani Profesa Ndulu anataka noti ya 500/= na ya 10,000/= zidumu kwenye mzunguko kwa muda sawa?? Yani 10,000/= ikidumu miaka miwili, 500/= nayo idumu miaka miwili. Bila shaka hapo ndo ataona noti ya 500/= haichakai haraka.

Hii ni "akili ndogo kujaribu kutawala akili kubwa". Noti ya 500 haiwezi kulinganishwa na noti nyingine kwenye mzunguko kwa sababu ina frequent circulation. Yani ktk uchumi noti yenye thamani ndogo huwa inazunguka zaidi kuliko ya thamani kubwa.

Hivyo noti ya 500/= inaweza kupita kwenye mikono ya watu 2000 ndani ya mwezi mmoja wakati ile ya 10,000/= imepita kwenye mikono 20 tu kwa mwezi.

Hii ni kwa sababu mzunguko wa noti hizi hutegemea matumizi. Ya 500/= itazunguka kwny daladala, wauza magazeti, vijiwe vya kahawa etc, wakati ile ya 10,000/= itazunguka Supermarket, Airport, hoteli kubwakubwa etc.

Hivyo ni dhahiri kuwa noti ya 500/= itaanza kuchakaa mapema kuliko noti ya 10,000/= au ya 5,000/= au noti nyinhine kubwa. Sasa cha ajabu Profesa Beno Ndulu hajui hili na badala yake ameona solution ni kuleta sarafu. Aibu gani hii kwa mtu anayejiita Profesa wa uchumi kushindwa kujua vitu common km hivi ambavyo hata muuza machungwa wa Keko anavijua??

Mama lishe wa Tandale "kwa tumbo" anajua kuwa noti ya 500/= inachakaa haraka kuliko ya 10,000/= kwa sababu ina mzunguko mkubwa. Yeye anaweza kushika noti za 500/= hata mia kwa siku kwenye mauzo yake lakini asione hata noti moja ya 10,000/=.

Cha ajabu Profesa Ndulu hajui hili. Yeye amekerwa na noti ya 500/= kuchakaa haraka na ameona dawa ni kueeplace sarafu.

Naumia kuiona Tanzania ikiangamizwa na watu tuliowaamini, tuliowaheshimu, tukawapa madaraka, kwa kuamini ni wasomi watatusaidia. So sad, uchumi wa Tanzania ulale mahali pema peponi..!!

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.
|| Your Partner in Critical thinking.!!
 
kweli kabisa noti ya 500 hata uhifadhi wake ni wa hali ya chini kwenye vidosho vigundo vya khanga ila 10000 kwenye pochi atm kwenye mabunda hivyo haiwezi kuhimili mikiki mikiki lazima ichakae kwa haraka
 
Hizi takwimu za mwaka gani jitahidi kuwa makini kwenye data zako leo umetia aibu kweli.
 
mkuu unao utaalamu hata kidogo wa uchumi,banking au finance? Naona kama umetoa mawazo yako tu ambayo hayajawa based on facts.
 
Dah, inasikitisha sana, ila thread kama hii haiwezi pata wachangiaji wengi, mleta maada ungeleta thread ya Siasa ingeisha pata coment 100, ila ukweli kufuta not ya 500 maana yake sh 500 inawekwa kwenye kundi la pesa ndogo ndogo ambapo hutaweza tena kuzipata kwenye maduka ya kubadilishia pesa ya nchi zingine, Hutaweza ipate sh 500 nchini Kenya au Uganda, Wakati Tanzania kwenye maduka ya pesa unapata mwisho Sh 50 not ya kenya ila ni tofauti kabisa Ukienda kenya, kwa sasa utaanza kupata sh 1000/
 
Mbona uchumi wetu ulishaporomoka siku nyingi! Hizi zilizo baki ni propoganda tu, hakuna cha uchumi kukua hapa bali mdororo wa uchumi na kuanguka kwa kasi ya ajabu kwa shilingi yetu.
 
Mkuu yani ukizungumzia swala la uchumi wa tz ni kutiana hasira tuu ktk kila sekta. Waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali zetu wanajiamini sana ktk kufanya maamuzi ya hovyo wakijua wabongo wengi hawawezi kufanya lolote zaidi ya kulalamika tu vijiweni wakishiba wanasaau. Ndio maana saivi waboongo wengi imefikia hatua wakipata fursa tu (ya kuiba au rushwa) wanaitumia vilivyo. Very sad kwa kweli
 
Back
Top Bottom