Uchumi wa Tanzania unaibiwa mchana kweupe

Uchumi wa Tanzania unaibiwa mchana kweupe

Col FEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
327
Reaction score
460
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa kweli inasikitisha kuona taasisi zetu mbali mbali, kama vile Uhamiaji, SUMATRA, TRA n.k zikiwa zimekaa kimya wakati Tanzania tunaibiwa mchana kweupe. Naomba nitoe mfano mmoja ili kuonyesha ni jinsi gani tulivyo lala na wakoloni wakiendelea kuneemeka.

Mola ametujaalia kuwa na Bandari ambayo imekaa eneo zuri sana na hivyo kuwa ni rahisi kwa nchi majirani kuitumia. Hivyo mizigo mingi ya Majirani zetu inapitia hapa Bandari ya DAR! JE MOLA ALIFANYA MAKOSA KUTUPA BANDARI HII?

Hivi sasa kumezuka wimbi la wageni wengi kuja hapa Dar Wahindi, Wachina, na Wazungu ambao wanafungua vikampuni vidogo vidogo kwa ajili ya kudaka mizigo yote unayopitia hapa Dar (Clearing & Forwarding na Cargo Consolidation) ieleweke kuwa hii mizigo inayo kuja na kupitia hapa inaanzia huko kwao hivyo kufanya raisi kwa wao kupata habari mapema ya ujio ya mizigo husika hivyo basi kupelekea kazi nyingi za mizigo inayo kuja hapa TZ hufanywa na wao wageni huku sisi Watanzania tukibakia kuwa vibarua tu. Kwa njia hii Pesa nyingi ambazo zingebakia hapa Tanzania kwa biashara ya Bandari yetu 80% ya kipato hiki kinarejeshwa kwa wakoloni wakati sisi tumelala.

Hivyo basi naziomba sana taasisi zetu ziamke kutoka usingizini na kuanza mara moja kufanya uchunguzi wa kampuni zote Wakala wa Mizigo ili kuhakikisha zinamilikiwa kwa 100% na Watanzania wenyewe tena ikibidi tuwe Watanzania weusi. Haiwezekani Wazungu watoke kwao huko kuja hapa kufanya kazi ya ukarani tu wa mizigo na kuondoka na Dola zetu, tusione haya kutetea uchumi wetu ili kuhakikisha unanufaisha Taifa letu kwa 100%.

Mola ametupa Bandari ili itunufaishe sisi Watanzania wazawa. Vita ya Uchumi ni vita ngumu sana kwani vibaraka wa Wakoloni wapo wengi. LAZIMA TULINDE RASILIMALI ZETU KWA NGUVU ZOTE NA BANDARI NI RASILIMALI KUBWA AMBAYO TUMEIZARAU. TUAMKE NA TUPAMBANE KULINDA UCHUMI WETU.

Je tujiulize Wakala wa Mizigo na Meli kunaulazima gani ya kuwa na Mtaalam wa kigeni? Jamani hadi kazi ya Ukarani tunahitaji Mzungu aje kutusimamia? Tumelala Jamani tunaibiwaa kweupe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua uchumi wa soko huria una faida na changamoto zake.Swali hapo ni je hao wageni wanafanya kazi ki uhalali ??wanalipa kodi ??

Kama vyote hivyo viko sawa then tujiulize kwa nini hatujachangamkia fursa hii ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasema weusi kwasababu kuna wenzetu weupe wengi ni vibaraka na wamekuwa wakitorosha uchumi wa nchi hii kwa kisingizio cha kuwa na wao ni wazawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhubiri 9:11,14
[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
Mkuu colfen, unachosema ni sahihi, na siyo kwa bandari tu. Ukiangalia Kariakoo, kuna maduka mengi ya rejareja na jumla yanamilikiwa na wachina. Unakuta mwenye kiwanda huko China, anamiliki duka la jumla na la rejareja Kariakoo.. Mfumo wa biashara wa aina hii unawaweka kwenye hali ngumu wamiliki wa maduka wazawa kwenye ushindani wa kibiashara.

Kulikuwa na taasisi ya Kitanzania inaitwa Fair Competition, sijui kama bado ipo na kama majukumu yake ni yapi.

Siyo rahisi M-tz aende china au india aishi na kufanya biashara ya maana kule.

Kimsingi hii nchi imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu ambacho yeyote ananyoa akijisikia. Ni ajabu kuwa wageni hawawekewi mipaka, au kama ipo ni kwenye makaratasi tu!
 
Mkuu colfen, unachosema ni sahihi, na siyo kwa bandari tu. Ukiangalia Kariakoo, kuna maduka mengi ya rejareja na jumla yanamilikiwa na wachina. Unakuta mwenye kiwanda huko China, anamiliki duka la jumla na la rejareja Kariakoo.. Mfumo wa biashara wa aina hii unawaweka kwenye hali ngumu wamiliki wa maduka wazawa kwenye ushindani wa kibiashara.

Kulikuwa na taasisi ya Kitanzania inaitwa Fair Competition, sijui kama bado ipo na kama majukumu yake ni yapi.

Siyo rahisi M-tz aende china au india aishi na kufanya biashara ya maana kule.

Kimsingi hii nchi imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu ambacho yeyote ananyoa akijisikia. Ni ajabu kuwa wageni hawawekewi mipaka, au kama ipo ni kwenye makaratasi tu!
 
hapo ndo kwenye shida..kwann tulalamike tunaibiwa na ni sisi wenyew tumezubaa!!!!watu wameona tumelala wao wakachangamkia fursa jambo la maana ni serikali kuhamasisha wanachi wake juu ya fursa zilizopo kwe nchi yetu tusikomalie mambo magum na makubwa wakati haya madogo yanatushinda
 
hapa ndo mahala ambapo state media kama TBC wangekuwa wanaandaa vipindi kwa kushirikiana na wataalamu wa hayo mambo ili kuwaongezea watanzania exposure ya mambo mbalimbali ambayo bado tupo nyuma
 
Jamani wa TZ tuamke toka usingizini na tuhakikishe Serikali ina wawezesha wazawa wazalendo kwa makusudi kumiliki uchumi pia inazuia kwa makusudi na nguvu zote kwa wageni kujitajirisha kupitia rasilimali zetu kwa ujumla wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom