Visiwa vya Madagascar, Seychelles, Maldives, Reunion na Zanzibar ni visiwa viliopo kwenye bahari ya Hindi. Uchumi wa visiwa hivi umefanana vinategemea utalii na kilimo. Kipato cha wastani (per capita income)wa visiwa hivi ni kama ifatavyo:
Reunion $ 23,000 kwa mwaka
Maldives $ 18,600 kwa mwaka
Seychelles $ 16,000 kwa mwaka
Madagascar $ 1900 kwa mwaka
Zanzibar $ 460 kwa mwaka
Kwa kuzingatia takwimu hizi ni dhahiri Zanzibar hoi kiuchumi ukilinganisha na uchumi wa visiwa vengine vya bahari ya Hindi. Hivi nini chanzo cha umaskini wa Zanzibar?