Uchumi wetu hauwezi kukua kwa kuwanyonya masikini

Uchumi wetu hauwezi kukua kwa kuwanyonya masikini

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Kuna kiongozi mmoja mkubwa aliwahi kusema kwamba hata yeye hajui kwa nini wananchi ni maskini! Ni masikini kwa sababu wananyonywa! Huwezi kuwa na tax rate kubwa kwenye income tax, kwenye Vat, kwenye import duty na bado hao wananchi watajirike. Watatajirika vipi wakati marginal propensity to save is small.

Ili wananchi watajirike inabidi wafanye investments which is equal to savings. Sasa kama wananchi hawana savings rate ya kutosha, inamaana hawawezi kuinvest. Na hivyo Nurkes vicious poverty cycle itaendelea kuwala wananchi na taifa kwa ujumla haliwezi kunufaika. Tubadilike kwa manufaaa ya wananchi na nchi yetu!

Some working Outs!
Kwa hali ilivyo sasa hivi, kila asilimia hamsini ya pato la mfanyakazi inapotelea kwenye kodi. Chukua mshahara wa milioni moja utakatwa hapo karibu laki mbili na nusu kodi, huyo mfanya kazi ataondoka na laki saba unusu. Atanunua Petroli ambayo nayo imekatwa kodi, let say kwa mwezi kanunua mafuta ya laki mbili na nusu, kodi hapo ni karibu laki nzima, pia atanunua umeme ambao nao ataulipia kodi, atanunua nguo kutoka China ambayo nayo itkuwa imelipiwa mikodi kibao, atanunua simu ambayo nayo itakuwa imekatwa kodi. Kwa hiyo hapo kitu kinachojitokeza kanakuwa double taxing... Hivyo unakutak kama mtu alilipwa milioni moja, karibu laki tano nzima itaishia kwenye kodi , na laki tano nyingine ndio itanunua huduma.
 
Back
Top Bottom