Uchumi wetu upo kwenye hatua ipi?Recovering,Recession,Peak ama Depression?

Uchumi wetu upo kwenye hatua ipi?Recovering,Recession,Peak ama Depression?

Imma Saro

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
394
Reaction score
197
Uchumi wetu upo kwenye hatua ipi?Recovering,Recession,Peak ama Depression?

Leo humu mtandaoni nimeona matangazo ya kampuni moja kubwa ya simenti na benki moja zikitangaza hasara huku jana niliambiwa kuwa kuna benki moja imetangaza kufunga baadhi ya matawi yake ikilitangaza tawi la Wilaya ya Babati!.

Nadhani wachumi mlitakiwa kutupa ufafanuzi kuhusu uchumi wetu,"cycle" yake ipo wapi kwenye dhana ya "economic cycle" na je kesho yake ni njema?na tahadhari zipi zinatakiwa zichukuliwe na mtu mmoja mmoja pamoja na wawekezaji wakubwa?

Je hatua tuliyo nayo sasa kwenye mzunguko wa kiuchumi,nini kinashauriwa kichumi? "Kusave" sana?kutumia sana ama kuwekeza sana/kuingiza pesa nyingi kwenye uwekezaji!.

Huu ni wakati wa kuona maandiko,mijadala na hoja za kutosha kutoka kwa wachumi wetu,wao ndiyo vyanzo sahihi(credible),sasa mkituacha sisi vyanzo vya kawaida vinavyoguswa na mzunguko huu aa uchumi(reliable),tunachambua mambo,tutachambua kwa kadri tunavyoona mifuko yao,na mkiwaacha serikali (Authoritative)wachambue wao tu,wao watachambua kwa kujilinda.

Ndiyo maana sijafurahishwa sana na matumizi ya sheria ya takwimu ta mwaka 2016,inatia hofu watafiti!.


by
D:Bulendu.
 
IMG-20171103-WA0034.jpg
IMG-20171103-WA0033.jpg
IMG-20171103-WA0032.jpg
IMG-20171103-WA0031.jpg
 
Vyakula vipo vya kutosha na kuzaliana watoto kume stawi sana hivyo uchumi wetu umeongezeka sana
 
kuna makosa huko kwenye Mitandao, kwa usahihi tazama mtandao wa BOT
Wewe ndio utakua na matatizo, angalia real time exchange rate, kama hutaki endelea kuangalia BOT
 
Pia hali ya shilingi yetu kila siku inashuka hii inawaatiri sana watu wanaonunua bidhaa toka nje nk wachumi ongeeni kwakweli tujue moja
6b990984362e825a065715c81feaf699.jpg
 
Kwi kwi kwi kwi kwi soon tutaanza kutoa mikopo kwa mataifa madogo duniani na mataifa makubwa.

Uchumi unakua kwa kasi ya kupaa. Tukisema tofauti sheria ya takwimu itatuhusu. Uchumi uko kwenye peak kwasasa had mataifa ya nje yanatuonea wivu
 
a82e0e817831aa61831b953e8bb1c73d.jpg

2200[emoji654]2500[emoji31][emoji30][emoji24][emoji24] ni hatari
Yan nlichokuwa nanunua nje kwa shilingi 2200,000/= now bila 2500,000 sipati......Mijitu itaendelea kupiga makofi kulinda maslahi yao...Hakuna nchi tena hapa umbumbumbu UNATUMALIZA...#ANG'OLEWE
 
Back
Top Bottom