Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Wanasiasa wasiojua Kushindwa hawastahili kushinda. Kuelekea Uchaguzi Mkuu tutaona na kusikia mengi; tutaona watakaocheka na watakaonuna, watakaolia na watakaochukia, Watakaokenua na watakaokimbia.
Vigogo wataanguka na kupigwa na butwaa, vijana wataibuka na watu wakashangaa, tutaona na kinyume chake; vijana wataangushwa na wazee na manjemba wakibwagwa na kina dada!
Tuwapime Hawa wanaoangushwa na kukataliwa, wanaitikia vipi. Tusiwatengenezee njia ya kuwabeba. Walioshindwa waachwe wanuse na walambe ladha chungu ya Kushindwa! Tutajua wametengenezwa kwa udongo gani...
#kurazamaonizisimame2020