Uchungu

Ruth Benson

Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
9
Reaction score
2
Naomba kujua jamani, kipi kinaanza mwanamke akitaka kujifungua kati ya uchungu au maji yanayotoka au damu? Au vyote huanza kwa pamoja?
 
cha kwanza ni uchungu unaomfanya mtoto azidi kusogea chini kuingia kwenye nyonga kuelekea kwenye uke,ule mfuko wenye maji anamokaa mtoto hata kuwa na uhuru wa kucheza(amniotic fluid sac) hupasuka hapo ndo maji mengi hutoka, hapo utasikia wanasema chupa imepasuka(rupture of membrane)

wamama wengi chupa ikipasuka hawachelewi kujifungua hasa uchungu ukiwa umekazana kwa maana chupa isipopasuka mtoto hawezi toka maana anakuwa yumo ndani ya huo mfuko wenye maji,na maji hayo ndo amniotic fluid, lakini wengine waweza chelewa baada ya hayo maji ni kiumbe kutoka ndo damu hufuata kisha kondo la nyuma likisha toka damu nyingi hutoka.
 
A very simple task,

yaaa msaidie asiogope na kazi yenyewe ni kunya kwa nguvu badala ya kutoka mavi hutoka mtoto shida ni pale mtu anaenda kujifungua huku hajajisaidia lazima mzigo wa kinyeshi utoke ndo mtoto atoke ni rahisi kama unakunywa uji wenye sukari hahahahaha
 
Kabla ya kuzaa, mama mjamzito hupata uchungu kutokana na kutanuka kwa nyonga, kufunguka mlango wa uzazi na msukumo wa mfuko wa uzazi “uterine contractions”.

Baada ya hapo majimaji ya uchungu"amniotic fluid" na damu nyepesi vitatoka “rupture of membrane”. Chupa ikipasuka ndipo mtoto anapotoka.

Mtoto anaweza kutoka kwa kutanguliza kichwa “cephalic presentation” au akatanguliza matak.o “breech presentation” au mtoto anaweza kutanguliza mikono au miguu au uso,lakini yote haya hurekebishwa wakati wa kujifungua.
 
Naomba kujua jamani, kipi kinaanza mwanamke akitaka kujifungua kati ya au maji yanayotoka au damu? Au vyote huanza kwa pamoja?

Ruth unakaribia nini? Usiogope...! Kinachofanyika ni hicho wachangiaji wamekueleza! Kila lakheri kama ni mtarajiwa.
 
Unaanza uchungu aisee ndugu hapo utashuhudia mwenyewe maji yakianza kutoka mtoto hachelewi akianza kutoa kichwa ni vizur zaid
 
Mh hiki kikombe siwez kukiepuka hata nfanyaje,asanten kwa kutujuza haya!
 

Did >5 deliveries ambazo mtoto alitoka akiwa ndani ya mfuko wake.
 
kwa kauzoefu kangu kamiaka kadha kwenye field hii sijaona mtoto akitoka akiwa kwenye mfuko wake kwenye SVD,ladba iko siku nitaona.

mi mwenyewe nilikuwa siamini initially lakini my first observation ilikuwa mnh enzi hizo nipo chuo. Hui inategemea na size ya mtoto na speed ya cervical dilatation. Kuna mwingine anakuja yuko fully na membranes zimebulge, unapojiandaa kupasua unakutana na mtoto anatoka.
 

Mmmh! Makubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…