Uchunguzi dhidi ya Rushwa katika Qatar kuandaa World Cup 2022: Rais wa zamani wa UEFA, Michel Platini akamatwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Amekamatwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea dhidi ya madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika uamuzi wa kukubali michuano ya Soka ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022, kufanyika Qatar

Amekamatwa mapema leo na kuwekwa kizuizini huko Nanterre, Paris, nchini Ufaransa

Platini, aliyeongoza UEFA tangu mwaka 2007 hadi 2015, kwa sasa atumikia zuio la kutojihusisha na soka kwa miaka minne baada ya kukutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwa Rais wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter

Katika hali inayodaiwa kuwa ni ya kushangaza mnamo Desemba 2010, Qatar ilishinda na kupewa idhini ya kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022


====

Former UEFA president Michel Platini has been arrested as part of an investigation into alleged corruption relating to the decision to award Qatar the 2022 World Cup, according to reports.

He was taken into custody in Nanterre, Paris, on Tuesday morning.

Platini, who was UEFA president between 2007 and 2015, is currently serving a four-year ban from football after he was found guilty of receiving a "disloyal payment" from ex-FIFA president Sepp Blatter.

Qatar controversially won the rights to host the 2022 World Cup nearly a decade ago, in December 2010
 
Wenzetu wako makini sana masuala ya ufatiliaji. Tangu 2010 mtu kaja kukamatwa leo 2019..
 
Kitendo cha WC 2022 kwenda uarabuni wanzungu kimewauma sana inavyoonekana ,Maana hili sakata ndio hata Blater lilimtoa
 
Mwarabu anapigwa vita sana asiandae michuano
 
Hii rushwa haikuanza Leo Kama kweli walikuwa wanachukia rushwa wangeanza uchunguzi kipindi kile wajerumani wanapewa uenyeji wa kombe la dunia pale rushwai ilukuwa waziwazi
 
Unadhani wanamkomoa au wanatekeleza wajibu wao kupambana na rushwa?
Wanatekeleza wajibu wao ,ujue mchakato wa uandaaji WC toka ile 2006 German ,2010 SA na 2018 Russia na 2022 Qatar kuna tuhuma nyingi za rushwa

Km unakumbuka SA alivyokosa uandaaji wa 2006 akapewa German kuna mjumbe hakupiga kura kwa makusudi ( kwa mtazamo wangu yule alikula rushwa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…