HOJA Uchunguzi ufanyike kuhusu mifumo ya Chuo cha Mwalimu Nyerere pale Kigamboni, vijana wangu wamefutiwa matokeo

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Nina vijana wangu sita wanaosoma katika Chuo cha Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wameathirika baada ya kufutiwa matokeo yao na kuambiwa kuwa walighushi matokeo.

Kwa maelezo tuliyoyapata, si watoto wangu pekee waliokumbwa na hali hii, bali kuna wanafunzi zaidi ya 200 ambao wote ni wa mwaka wa tatu na walikuwa wanatarajia kuhitimu, lakini sasa wamejikuta wakiwa katika hali ya kutokuwa na uhakika wa hatma yao ya masomo.

Kinachotupa maswali ni kwamba wanafunzi hao wameambiwa wameghushi matokeo, lakini kuna wanaodai kuwa huenda tatizo limetokana na changamoto za mifumo ya chuo ambayo wakati mwingine imekuwa ikipata matatizo ya kiufundi. Hivyo, tunaomba suala hili lichunguzwe kwa kina ili kubaini kama kweli wanafunzi hao walifanya udanganyifu au kama kuna tatizo jingine la kimfumo.

Kama mzazi, naomba mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Elimu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), pamoja na wadau wengine wa elimu, wafuatilie jambo hili kwa haki na uwazi.

Lengo si kupinga taratibu za chuo, bali kuhakikisha wanafunzi ambao wamewekeza muda na fedha zao hawapati madhara kutokana na makosa ambayo huenda hayakutokana na wao.

Tunaiomba serikali na uongozi wa chuo kusikiliza kilio hiki, kufanya uchunguzi huru na kutoa majibu yatakayosaidia kujua ukweli wa jambo hili ili wanafunzi waweze kupata haki yao na hatma yao ya kuhitimu iwe wazi.
 
Hivi naomba kuuliza kitu hivi hili ni jambo la kitaifa ambalo linahitaji hadi serikali itoe tamko?
Kwa nini wazazi msiungane mkaenda kuwaface hao walimu wao ana kwa ana mpate majibu sahihi yenye ushahidi na wakikosa ushahidi muwe wakali ikiwezekana kuwashitaki kwa njia mnazojua nyinyi.
Hata serikali ikiingilia kati kesi yake inaweza ikachukua miaka 3 kukamilika utakuwa umepoteza muda mwingi sana.
 
Watoto 6 wote mwaka wa 3 mhhh SEMA TU zupo wanafunzi 6 WA MNM atuelewi hatma yetu matokeo yafutwa tumeambiwa twagushi
 
Hivi naomba kuuliza kitu hivi hili ni jambo la kitaifa ambalo linahitaji hadi serikali itoe tamko?
Kwa nini wazazi msiungane mkaenda kuwaface hao walimu wao ana kwa ana mpate majibu sahihi yenye ushahidi na wakikosa ushahidi muwe wakali ikiwezekana kuwashitaki kwa njia mnazojua nyinyi.
Hata serikali ikiingilia kati kesi yake inaweza ikachukua miaka 3 kukamilika utakuwa umepoteza muda mwingi sana.
Wala hili si suala la wazazi kuingilia kati. Ni suala la wanafunzi wenyewe kupambana ili kujua hatima Yao. Mtoto yupo mwaka wa tatu chuoni bado hana uwezo wa kujipambania mwenyewe? Kama Hawezi basi hakupata maarifa yoyote hapo chuoni,alipoteza muda tu.
 
Uko sahihi.
Labda kwa vile siku hizi wanaingia chuo wakiwa bado wadogo wanakosa ile confidence ya kuongea kiutu uzima
 
Nina vijana wangu sita wanaosoma katika Chuo cha Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wameathirika baada ya kufutiwa matokeo yao na kuambiwa kuwa walighushi matokeo.

Kwa maelezo tuliyoyapata, si watoto wangu pekee waliokumbwa na hali hii, bali kuna wanafunzi zaidi ya 200 ambao wote ni wa mwaka wa tatu na walikuwa wanatarajia kuhitimu, lakini sasa wamejikuta wakiwa katika hali ya kutokuwa na uhakika wa hatma yao ya masomo.

Kinachotupa maswali ni kwamba wanafunzi hao wameambiwa wameghushi matokeo, lakini kuna wanaodai kuwa huenda tatizo limetokana na changamoto za mifumo ya chuo ambayo wakati mwingine imekuwa ikipata matatizo ya kiufundi. Hivyo, tunaomba suala hili lichunguzwe kwa kina ili kubaini kama kweli wanafunzi hao walifanya udanganyifu au kama kuna tatizo jingine la kimfumo.

Kama mzazi, naomba mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Elimu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), pamoja na wadau wengine wa elimu, wafuatilie jambo hili kwa haki na uwazi.

Lengo si kupinga taratibu za chuo, bali kuhakikisha wanafunzi ambao wamewekeza muda na fedha zao hawapati madhara kutokana na makosa ambayo huenda hayakutokana na wao.

Tunaiomba serikali na uongozi wa chuo kusikiliza kilio hiki, kufanya uchunguzi huru na kutoa majibu yatakayosaidia kujua ukweli wa jambo hili ili wanafunzi waweze kupata haki yao na hatma yao ya kuhitimu iwe wazi.
Ndugu
 
Ndugu yangu wewe ni mzazi na watoto wako wote 6 wapo Mwalimu Nyerere.Ongea na hao watoto wako 6,wamekudanganya kwamba wanaonewa ilhali wamefanya makosa dhahiri.Kama kweli wamehusika sheria itasema.Sheria,taratibu na kanuni haziangalii hata kama umebakiza mwezi mmoja kuhitimu.Nenda Chuo wasiliana na watu wa mitihani na uongozi kwa ujumla UTAYAJUA MENGI JUU YA WATOTO WAKO 6
 
Back
Top Bottom