Uchunguzi wa mapacha njiti waliochunwa ngozi ya uso wakamilika. Wanne kufikishwa Mahakamani kwa Uvunaji wa Viungo vya Binadamu

Uchunguzi wa mapacha njiti waliochunwa ngozi ya uso wakamilika. Wanne kufikishwa Mahakamani kwa Uvunaji wa Viungo vya Binadamu

Wauguzi wanne katika mkoa wa Tabora Magharibi nchini Tanzania watafikishwa Mahakamani kwa kosa la kuvuna viungo vya watoto mapacha, afisa wa mkoa amesema.

Kamati iliyoundwa kuchunguza tukio hilo iligundua kuwa miili ya mapacha hao waliozaliwa kabla ya wakati wao ilikuwa imeharibika baada ya kufariki.

Mama huyo alikuta macho ya watoto wake yametobolewa na sehemu ya ngozi yao ikiwa imetoka kwenye paji la uso.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Batilda Buriani alisema wauguzi hao ambao wako chini ya ulinzi wamesimamishwa kazi.

Alisema uvunaji wa viungo hivyo unahusishwa na uchawi.

Wauguzi hao waliipotosha kamati ya uchunguzi kwa madai ya uwongo kwamba miili hiyo ilihifadhiwa katika wadi ya wazazi wakati, ilipatikana katika chumba cha wauguzi, Bi Buriani aliongeza.

Wauguzi hao bado hawajazungumzia madai hayo.

Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa pacha hao walifariki dunia kutokana na kukosa huduma za watoto wachanga ambazo hazikupatikana katika kituo walichozaliwa.
Mie nilicho sikia ni kwamba mtoto mmoja Hana jicho na ametolewa ngozi kwenye paji la uso hizi hospital zetu isije kua ni panya Mana mie kunandugu wa mke wangu huko mikoani walishakuta marehem Hana jicho na baadhi ya vidole vimetafunwa na panya
 
Kingine hizi hospital za serikali kuna Mapaka, yaan sijui ni Paka sijui misukule.

Ilikua Songea kuna mtoto mdogo wa week 3 alikutwa kafa huku mwili umetafunwa na paka.

Tena huwa yanazurura, afu mabishi na makavu balaa, hayaogopi watu
 
Tukipiga vita mnasema maslahi madogo ndio chanzo. Peleka jela hao
 
Wauguzi wanne katika mkoa wa Tabora Magharibi nchini Tanzania watafikishwa Mahakamani kwa kosa la kuvuna viungo vya watoto mapacha, afisa wa mkoa amesema.

Kamati iliyoundwa kuchunguza tukio hilo iligundua kuwa miili ya mapacha hao waliozaliwa kabla ya wakati wao ilikuwa imeharibika baada ya kufariki.

Mama huyo alikuta macho ya watoto wake yametobolewa na sehemu ya ngozi yao ikiwa imetoka kwenye paji la uso.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Batilda Buriani alisema wauguzi hao ambao wako chini ya ulinzi wamesimamishwa kazi. Alisema uvunaji wa viungo hivyo unahusishwa na uchawi.

Wauguzi hao waliipotosha kamati ya uchunguzi kwa madai ya uwongo kwamba miili hiyo ilihifadhiwa katika wadi ya wazazi wakati, ilipatikana katika chumba cha wauguzi, Bi Buriani aliongeza.

Wauguzi hao bado hawajazungumzia madai hayo.

Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa pacha hao walifariki dunia kutokana na kukosa huduma za watoto wachanga ambazo hazikupatikana katika kituo walichozaliwa.
Hii lugha ya kuita Uvunaji nafikiri haipo sawa...binadamu anahitaji kuheshimiwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian @batilda.burian amesema jalada la uchunguzi wa tukio tata la Watoto pacha waliozaliwa kabla ya muda katika Kituo cha Afya Kaliua na mmoja wao kunyofolewa jicho la kulia na ngozi ya paji la uso, limekamilika na Watumishi wanne wa Kituo hicho watafikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Akiongea na CG FM Dkt. Batilda amesema uchunguzi umebaini miili ya Watoto hao ilitunzwa katika chumba cha Wauguzi na sio katika wodi ya Wazazi kama ilivyosemwa awali na Wauguzi hao.

RC Batilda amewataja Wauguzi hao kuwa ni Theresia Kakiziba, Asha Magidi, Paulo James na Benson Maikase na kwamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kuwasimamisha kazi Wauguzi wengine wawili walioongezwa katika kesi hiyo.

Itakumbukwa tukio hilo lilitokea May 9, 2023 katika Kituo cha Afya Kaliua ambapo inadaiwa Mtoto mmoja kati ya wawili pacha waliozaliwa kabla ya muda na kufariki alinyofolewa jicho na kuondolewa ngozi ya paji la uso hali iliyozua taharuki iliyopelekea Familia ya Isaka Rafael kugoma kuzika miili ya Watoto hao hadi leo.

Pia soma:
Ili kurudisha Imani ya umma kwa watumishi wa afya, ni vyema Kesi hii ikaendeshwa mfululizo mwanzo hadi mwisho.Ikiwezekana ikamilike ndani ya mwezi mmoja tu kuanzia hapo itakapofikishwa Mahakamani, iend3shwe kwa utaratibu wa "fast track" ili watu wengi zaidi wasiendelee kupoteza Imani dhidi ya manesi na madaktari.
 
Mie nilicho sikia ni kwamba mtoto mmoja Hana jicho na ametolewa ngozi kwenye paji la uso hizi hospital zetu isije kua ni panya Mana mie kunandugu wa mke wangu huko mikoani walishakuta marehem Hana jicho na baadhi ya vidole vimetafunwa na panya
Sio kwa watoto waliokuwa chini ya uangalizi,
Watoto walitunzwa wapi mda huo make walikaa mda mrefu wakati ilibidi wawahishwe hospitali
Ilikuwaje wakawafunga moja kwa moja kwenye mabox?
Ni ushirikina
 
Halafu utasikia mtu anaponda kwamba tumeacha tamaduni zetu tumefuata za wayahudi na waarabu...sasa madhara ya upagani ndio kama haya!
 
Hii hatari sana Hawa watoto huenda waliuliwa makusudi,manake jamaa alikuja na usafiri wakagoma kumpa hao watoto
 
Kwa ufupi hapa serikali imepata sehemu ya kukimbia lawama pia... Inakuwaje zahanati inakosa mafuta ya gari la dharura.. kutoa cha afya cha karibu kitakosaje standby ambulance?! DMO ahusishwe kwenye hii case kuachana na hao washirikina wapo ambao wanatakiwa kuwajibishwa ?! Ummy anakwamnia hospitali zetu zina kila kitu .. pumbavu?? Wilaya inakosa standby ambulance?!
 
Hivi Sasa kwaiyo watashtakiwa Kwa kesi ya mauaji ya kukusudua na watakwenda jela Maisha
 
Back
Top Bottom