“Uchuuzi” Biashara zinazowalemaza Watanzania

Kuhusu mzawa kua na kiwanda nitawapa mkasa wangu Kwa kifupi gharama za uzalishaji upatikanaji malighafi msururu wa Kodi na WAKUBWA KUTAKA POSHO na bado hujaenda shindana sokoni ni HATARI KAMA ULIKOPA HELA KAMA MIMI UTALALA NA VIATU
Tupe ushuhuda kaka.
Ulifungua kiwanda cha nini?.

Na kaka Yangu alitaka kufungua kiwanda cha Rangi, Tanga pale Mkisi. Ila kiwanda kilikuwa mbali na akaambiwa kupeleka umeme na kuweka trasformer hadi kiwandani atoe 30 Mill. 😊😊😊😊.
Na idea ya kiwanda ikafa pale pale.
 
Uzalishaji unataka moyo sana, hata mimi nilikuwa na mentality kama yako ila kwa sasa nimebadili gia angani, nimeanza kufanya uchuuzi ili kukuza mtaji then nikikua nijenge majengo kwenye maeneo potential niweke viwanda vidogo vitakavyowasaidia wanangu kuendeleza kuwa na viwanda vya kati na vikubwa kama wataamua, wakitaka kuuza na wauze tu
 
Kuhusu mzawa kua na kiwanda nitawapa mkasa wangu Kwa kifupi gharama za uzalishaji upatikanaji malighafi msururu wa Kodi na WAKUBWA KUTAKA POSHO na bado hujaenda shindana sokoni ni HATARI KAMA ULIKOPA HELA KAMA MIMI UTALALA NA VIATU
Umeongea ukweli mtupu kuna jamaa yangu anafanya vzr n project yake. Cha kushangaa mkuu w kituo ndani y wilaya ilipo project anataka posho ya kila wiki anapewa bila sababu y msingi. Mpk huruma hii nchi kiongozi. Mtoa mada raha y ngoma ingia ucheze.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Natamani nikukutanishe na mama yangu mkubwa yupo uko morogoro town akuambie kiundani kwani amefunga kakiwanda kakae kadogo kakutengeneza mishumaa,mikate,cake,sabuni tena apo 90% maligafi niza apa ndani kasoro mashine tu (osha,tra na kuna watu wa ofisi nyingine walikua wanataka posho) miongoni mwa mazingaumbwe aliokutana nayo ni kukuta sabuni na mishumaa yake ipo sokoni wakati yeye amefunga kiwanda miez 6 sasa
 
Acha kabisa mkuu mimi ilibaki kidogo nipagawe bank unadaiwa production imesimama bank wanataka uza dhamana
 
Uzalishaji mgumu maana hakuna wakukulinda hatakama unamkataba na tenda (tazama mzabuni wa simba jaylut anavyopambana,tazama wamiliki wa viwanda vya pombe kali za GIN wanalalama kua wao wanatengeneza mzigo org kwa garama,kodi ila kuna watu wana viwanda bubu wanatengeneza bidhaa zenye nembo zao tena fake.
 
Acha kabisa mkuu mimi ilibaki kidogo nipagawe bank unadaiwa production imesimama bank wanataka uza dhamana
Lakini pia ukiacha sarakasi zote za ukiritimba wa taasisi za serikali, pia kuna suala la product kukubalika sokoni. Wateja wakijua bidhaa hii unazalisha wewe kapuku mwenzao waanza kukupiga majungu na kuiona product yako haifai. Yalishanikuta kwenye sembe.
 
Tafuta historia za hao wenye viwanda... wengi walianza kama traders, hata baby yake Mo huko Singida alianza kama trader, baba yake ndio akawa importer/exporter... yeye anafanya vyote + viwanda
Ni kweli usemacho, uchuuzi kwa kuanzia sio kitu kibaya na hakikwepeki maana unasaidia kujenga misuli ya kiuchumi na pia kulijua soko kiundani na undani wake ila kuufanya uchuuzi kuwa ndio maisha yetu yote hii inatuharibu, tunageuka kuwa watumwa wa wachina na wazungu
 
Mimi naona hawa wasomi viongozi wa mamlaka and the likes hawana uelewa sana juu ya Msoto uliopo mtu kurun kiwanda hasa Kwa wazawa mpaka aanze kupata faida wao Wana dhana kwamba ukisema tu huyu ana KIWANDA basi akili moja Kwa moja wanasema huyu ana HELA bila kujua mchakato mzima mpaka upate hela inaumiza sana kila siku Nissan zinakuja nipe hiki nipe kile mimi ni kiongoz Fulani
 
Hii sio sababu kubwa maana wapo vijana wengi wanazalisha wana viwanda vidogo vidogo wanategemea umeme huu huu wa Tanesco.
 
M
Mleta mada natamani kujua wewe binafsi umeanzisha nini au unafanya biashara gani? Ndo nianze kucomment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…