“Uchuuzi” Biashara zinazowalemaza Watanzania

“Uchuuzi” Biashara zinazowalemaza Watanzania

Natamani nikukutanishe na mama yangu mkubwa yupo uko morogoro town akuambie kiundani kwani amefunga kakiwanda kakae kadogo kakutengeneza mishumaa,mikate,cake,sabuni tena apo 90% maligafi niza apa ndani kasoro mashine tu (osha,tra na kuna watu wa ofisi nyingine walikua wanataka posho) miongoni mwa mazingaumbwe aliokutana nayo ni kukuta sabuni na mishumaa yake ipo sokoni wakati yeye amefunga kiwanda miez 6 sasa
Yaani hapo anapambana na maadui wawili.
1.Mafisadi/Wala rushwa
2.Pirates/Maharamia wamepiga copy bidhaa zake wanapiga hela kupitia brand yake
 
Uzi mzuri sana.
Changamoto kubwa kwenye hili ni uongozi. Maafisa wa Halmashauri wakikaa tu ofisini wakiwa hawana hela wanasema aah twende kiwandani na wakija lazima uwape hela.
Na unakua kama utararibu kila baada ya muda wanakuja, apo hadi mkuu wa kituo cha polisi wamo.
Ila sio kwamba haiwezekani inawezekana sana ila inahitaji msuli.
 
Tupe technical know-how mkuu. Masuala ya kodi, rushwa, shida ya umeme na maji n.k tunaweza kukabiliana nayo vipi
Umeme na maji ni kukabiliana navyo tuu na kufanya massive production pale vinapopatikana na maji ni kuhifadhi ya kutosha kulingana na uzalishaji wako.

Swala la kodi, rushwa na mengine yanayohusu urasimishaji kwa bongo serekali ina loophole nyingi sana hakuna system ya kukamata watu kirahisi labda uwe unatengeneza bidhaa haramu.

Na kiuhalisia huna haja ya kuikwepa serekali maana gharama zao ni ndogo sana hao tbs ni ndogo sana wao ni kuja kuchukua sample na kwenda nayo maabara malipo kidogo sana, tra cha muhimu uwe na mashine ya risiti na tunajua kuwa bidhaa nyingi tunanunua mtaani na risiti hatupewi japo wanazo.

Katika nchi rahisi kuanzia biashara na kufanikiwa ni bongo.

Nimekuwa kwenye packaging and plastic industries mda mrefu nina andika from expirience and exposure.

Sio mtu hata brender la juice hajawahi miliki anajiropokea.

Mfano wa mjasiriamali mdogo nimeuona na nimeufanya.
Kuna mtu kwa mtaji wa 12m alinunua mashine sido za kukoboa na kusaga mahindi mwaka jana yuko mlandizi sahivi anasema changamoto kubwa ni kuzidiwa na wateja na wala sio serekali, umeme wala maji.
 
Vipi wazee wa kuchapisha copy za bidhaa za watu mkuu. Hawa unaweza ukapambana nao vipi. Kuna comments uko juu nimeona wanaotengeneza pombe kali wanalalamika mtaani kuna vinywaji feki vyenye stika zao.
 
Hapo huzungumzii viwanda vidogo vidogo tena, yani hadi ifike stage watu watengeneze vitu kwa brand yako wewe sio mmiliki wa kiwanda kidogo tena.
 
Lakini pia ukiacha sarakasi zote za ukiritimba wa taasisi za serikali, pia kuna suala la product kukubalika sokoni. Wateja wakijua bidhaa hii unazalisha wewe kapuku mwenzao waanza kukupiga majungu na kuiona product yako haifai. Yalishanikuta kwenye sembe.
Usirudie kufanya hivi. Kuna jamaa Kariakoo wanaagiza vifaa vya simu kama cover, protector, charger na USB cable. Wameweka majina ya Kichina au ya Kizungu kwenye bidhaa zao wanafyatua kule China wanakuja kuuza Kariakoo kwa jumla.

Kuna wadada nawajua walitengeneza formula ya vipodozi wakaenda kutengeneza China na kuja kuuza bongo. Huku wanajifanya ni mawakala kwamba hiyo bidhaa inauzika nchi kadhaa ila wao ni wakala wa hapa.

Sasa hizo zote mtu ajichanganye aseme eti "Mwajuma Skin Care" uone.
 
Hii sio sababu kubwa maana wapo vijana wengi wanazalisha wana viwanda vidogo vidogo wanategemea umeme huu huu wa Tanesco.
Sasa mtu anazalisha maziwa unasema sio sababu kubwa umeme kukata?

Mtu yeyote anayezungumzia viwanda alafu anaona umeme kukata ni jambo la kawaida basi hajui anachojadili.
Reliable and cheap energy ni mojawapo ya vichochezi vya viwanda.

Hao unaosema "wapo vijana" ndio hao sasa wanazalisha kwa gharama kubwa. Mafuta yenyewe lita 4,000+. Mchina akizalisha kule kwao, akasafirisha, akalipa ushuru, akalipia godown anauza bei nafuu kuliko hao vijana wako wanaozalisha na huu umeme wa masimango.
 
Bongo kuna urasimu sana Rushall na kukwamishana just imagine was on the process ya kufungua kampuni ata kazi hujapata ndo unajitafuta uko kwa registration watu wanataka gawio na uwapi usajili unakwama unajikomboaje kwa mifumo ya ivi
 
Kikwazo kikubwa kwenye ufunguzi wa biashara ni ukiritimba uliojaa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kuna mfano mzuri wa Dangote na uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata mafuta nchini kwake Nigeria. Kama unaanzisha kiwanda unatakiwa uwe na namna nyingine ya kumudu gharama za maisha maana misukosuko yake hadi utoboe sio midogo.
 
kutwa kucha wanasifia kuwa awamu ya sita imewezesha kufungua biashara elfu 10 kadhaa. Kumbe kwenye uhalisia viwanda vidogo vinateseka.

Ngumu sana hii
 
Back
Top Bottom