Nimesoma comments Nyingi zimesema changamoto kubwa ni Urasimu ikiwepo Rushwa. Hivi ni kweli hatuwezi pambana na Urasimu na Rushwa?
Unajua Kwa mawazo yangu Watanzania wengi tunapenda kufanya vitu kwa upungufu unaacha Loophole ya Warasimu wengine kukutumia.
Mfano wewe hujakamilika kwenye ABC akija mtu wa mamlaka fulani. Ku deal na wewe badala ya kumwambia sawa narekebisha kosa kubwa tunafanya nikuandaa mazingira ya kumuomba afunike kombe ( Rushwa).
ukishampa mtu rushwa siku ya kwanza jua haitakoma utaendelea kuwa mtumwa wake Milele atautumia udhaifu huo kukuumiza hata kama utakuwa sawa atatafuta udhaifu kukuonesha haupo sawa umpe rushwa.
Nakumbuka kipindi fulani nikimiliki Gari Ndogo za Usafirishaji wa abiria. Siku kadhaa nilikiwa natoka naingia barabarani kama dereva. Sasa kulikuwa na Mfumo wa Trafic polisi kuwa gari inajiunga na kifurushi cha Tsh 5000 kwa siku kupita barabara husika. Ukitoa hio basi unapiga trip siku nzima free bila cheti wao waliita yani faini hii haikujali unakosa ama huna. Na usipo jiunga utatafutiwa kosa uchapwe vyeti (faini).
Mimi nikasema “nikiwa nna gari hii kama dereva mimi haiwezekani” sitatoa hiko kifurushi. Siku moja nimeanza tu kazi asubuhi nikapigwa mkono alipokuja polisi akasema hatujaiona hii gari leo kwenye kifurushi, nikamwambia nikiwa na gari ndugu sitoi pesa yeyote ya Rushwa kwakuwa gari ina vibali vyote. kagua gari nipige faini kulingana na kosa langu. Akaomba leseni, akakagua stika zote zipo sawa, akaangalia matairi nk nk akasema nenda. Kumbe kaweka kinyongo Moyoni.
Ikawa Nikiwa nayo mimi ile gari wanaipotezea siku dereva akiishika wanasema hatutaki kifurushi chako boss wako anakiburi wanamchapa faini za kutosha
Kufupisha maelezo siku moja niliondoka na dereva na faini waoizompiga mpaka kituo cha polisi nikawaeleza nimechoka na nnajua hili suala ni kwasababu ABC nikamwambia Mkuu wa kituo usipolitatua leo liishe kesho napanda ngazi za juu zaidi. Akanitishia kuniweka ndani kuww nafanya fujo pale. nikamwambia unachelewa ungeshaniweka hata sasa( akatishika kidogo). Daima kuna watu wazuri maishani mama mmoja polisi mtu mzima akatafuta namna akaniambia kazia hapohapo. Nikakaza sana Nilichanel lile suala mpaka ngazi za juu kiasi hatimae barabara ile vifurushi vikafa tukaishi huru.
Je ni kweli bila kusimamia haki zetu na msingi ya kweli iwe kikwazo cha kujijenga? Kwa imani yangu be bold simamia ukweli na uwe mkweli hakika warasimu watakupa Njia upite na utakuwa umeshinda dunia inataka uwe FIT to Survive dont give excuses