“Uchuuzi” Biashara zinazowalemaza Watanzania

Tupe ushuhuda kaka.
Ulifungua kiwanda cha nini?.

Na kaka Yangu alitaka kufungua kiwanda cha Rangi, Tanga pale Mkisi. Ila kiwanda kilikuwa mbali na akaambiwa kupeleka umeme na kuweka trasformer hadi kiwandani atoe 30 Mill. 😊😊😊😊.
Na idea ya kiwanda ikafa pale pale.
Daah. Pole yake...yaani wanaotakiwa kumpa support ndio wanammaliza na kumdidimiza. Waafrika tuna roho mbaya sana.
 
Nimesoma comments Nyingi zimesema changamoto kubwa ni Urasimu ikiwepo Rushwa. Hivi ni kweli hatuwezi pambana na Urasimu na Rushwa?
Unajua Kwa mawazo yangu Watanzania wengi tunapenda kufanya vitu kwa upungufu unaacha Loophole ya Warasimu wengine kukutumia.

Mfano wewe hujakamilika kwenye ABC akija mtu wa mamlaka fulani. Ku deal na wewe badala ya kumwambia sawa narekebisha kosa kubwa tunafanya nikuandaa mazingira ya kumuomba afunike kombe ( Rushwa).

ukishampa mtu rushwa siku ya kwanza jua haitakoma utaendelea kuwa mtumwa wake Milele atautumia udhaifu huo kukuumiza hata kama utakuwa sawa atatafuta udhaifu kukuonesha haupo sawa umpe rushwa.

Nakumbuka kipindi fulani nikimiliki Gari Ndogo za Usafirishaji wa abiria. Siku kadhaa nilikiwa natoka naingia barabarani kama dereva. Sasa kulikuwa na Mfumo wa Trafic polisi kuwa gari inajiunga na kifurushi cha Tsh 5000 kwa siku kupita barabara husika. Ukitoa hio basi unapiga trip siku nzima free bila cheti wao waliita yani faini hii haikujali unakosa ama huna. Na usipo jiunga utatafutiwa kosa uchapwe vyeti (faini).

Mimi nikasema “nikiwa nna gari hii kama dereva mimi haiwezekani” sitatoa hiko kifurushi. Siku moja nimeanza tu kazi asubuhi nikapigwa mkono alipokuja polisi akasema hatujaiona hii gari leo kwenye kifurushi, nikamwambia nikiwa na gari ndugu sitoi pesa yeyote ya Rushwa kwakuwa gari ina vibali vyote. kagua gari nipige faini kulingana na kosa langu. Akaomba leseni, akakagua stika zote zipo sawa, akaangalia matairi nk nk akasema nenda. Kumbe kaweka kinyongo Moyoni.

Ikawa Nikiwa nayo mimi ile gari wanaipotezea siku dereva akiishika wanasema hatutaki kifurushi chako boss wako anakiburi wanamchapa faini za kutosha

Kufupisha maelezo siku moja niliondoka na dereva na faini waoizompiga mpaka kituo cha polisi nikawaeleza nimechoka na nnajua hili suala ni kwasababu ABC nikamwambia Mkuu wa kituo usipolitatua leo liishe kesho napanda ngazi za juu zaidi. Akanitishia kuniweka ndani kuww nafanya fujo pale. nikamwambia unachelewa ungeshaniweka hata sasa( akatishika kidogo). Daima kuna watu wazuri maishani mama mmoja polisi mtu mzima akatafuta namna akaniambia kazia hapohapo. Nikakaza sana Nilichanel lile suala mpaka ngazi za juu kiasi hatimae barabara ile vifurushi vikafa tukaishi huru.

Je ni kweli bila kusimamia haki zetu na msingi ya kweli iwe kikwazo cha kujijenga? Kwa imani yangu be bold simamia ukweli na uwe mkweli hakika warasimu watakupa Njia upite na utakuwa umeshinda dunia inataka uwe FIT to Survive dont give excuses
Umeongea vizuri mkuu sema sheria wanazotunga chama cha ccm sio rafiki kwa mwananchi wa kawaida fikiria hiyo miushuru iliyowekwa kwenye kusafirisha mazao, fikiria hizo tozo zilizopo kwenye biashara unakuta ndio kwanza unataka kuanza biashara unatakiwa ulipie leseni na tozo za TRA wakati hata faida hujui utapataje

Mfanyabiashara anatozwa tozo ya frem kama yeye ndio mwenye nyumba kwa namna hiyo wanatengeneza mazingira ya rushwa kwa ulazima maana hayo matozo hayalipiki
 
Ntafanya mchakato wa kiwanda cha mafuta ya mgando Tanzania ukitaka kuanzisha hapa SA ni mwezi tu documents zote unazo ila huko kazi kweli nilijaribu kufatilia naona kuingiza mzigo ni rahisi kuliko kufungua kiwanda na hakuna uhusiano wa ofisi hii na ingine na wote uwaone aisee..
Hiyo kazi labda umpe mtu afatilie ukitaka ufanye mwenyewe utakatishwa tamaa maana huku ni rahisi na eneo wanakupa wao hata ukitaka kwa mkopo warehouse za kutosha..
Chemicals unatoa Durban na Iran..
 
Ntafanya mchakato wa kiwanda cha mafuta ya mgando Tanzania ukitaka kuanzisha hapa SA ni mwezi tu documents zote unazo ila huko kazi kweli nilijaribu kufatilia naona kuingiza mzigo ni rahisi kuliko kufungua kiwanda na hakuna uhusiano wa ofisi hii na ingine na wote uwaone aisee..
Hiyo kazi labda umpe mtu afatilie ukitaka ufanye mwenyewe urakatishwa tamaa maana huku ni rahisi na eneo wanakupa wao hata ukitaka kwa mkopo warehouse za kutosha..
Chemical unatoa Durban na Iran..
Asante sana mzes wa South.....vp kiwanda kama hiko cha mafuta ya mgando kinaweza kufika sh ngap kwa maaba ya kununua???
 
Sijafanya tafiti kwa sasa hivi naona kitakua kinahitaji hela nyingi tofauti na miaka ya nyuma hicho ikifika wakati ntafatilia vizuri maana chemicals zinatoka bado Iran wanashushia Msumbiji na Durban..
Mitambo ipo tofauti kutokana na kitu unachotaka kutengeneza kuanzia polisher,mafuta yenyewe na vitu vingine
 
Nimesoma comments Nyingi zimesema changamoto kubwa ni Urasimu ikiwepo Rushwa. Hivi ni kweli hatuwezi pambana na Urasimu na Rushwa?
Unajua Kwa mawazo yangu Watanzania wengi tunapenda kufanya vitu kwa upungufu unaacha Loophole ya Warasimu wengine kukutumia.

Mfano wewe hujakamilika kwenye ABC akija mtu wa mamlaka fulani. Ku deal na wewe badala ya kumwambia sawa narekebisha kosa kubwa tunafanya nikuandaa mazingira ya kumuomba afunike kombe ( Rushwa).

ukishampa mtu rushwa siku ya kwanza jua haitakoma utaendelea kuwa mtumwa wake Milele atautumia udhaifu huo kukuumiza hata kama utakuwa sawa atatafuta udhaifu kukuonesha haupo sawa umpe rushwa.

Nakumbuka kipindi fulani nikimiliki Gari Ndogo za Usafirishaji wa abiria. Siku kadhaa nilikiwa natoka naingia barabarani kama dereva. Sasa kulikuwa na Mfumo wa Trafic polisi kuwa gari inajiunga na kifurushi cha Tsh 5000 kwa siku kupita barabara husika. Ukitoa hio basi unapiga trip siku nzima free bila cheti wao waliita yani faini hii haikujali unakosa ama huna. Na usipo jiunga utatafutiwa kosa uchapwe vyeti (faini).

Mimi nikasema “nikiwa nna gari hii kama dereva mimi haiwezekani” sitatoa hiko kifurushi. Siku moja nimeanza tu kazi asubuhi nikapigwa mkono alipokuja polisi akasema hatujaiona hii gari leo kwenye kifurushi, nikamwambia nikiwa na gari ndugu sitoi pesa yeyote ya Rushwa kwakuwa gari ina vibali vyote. kagua gari nipige faini kulingana na kosa langu. Akaomba leseni, akakagua stika zote zipo sawa, akaangalia matairi nk nk akasema nenda. Kumbe kaweka kinyongo Moyoni.

Ikawa Nikiwa nayo mimi ile gari wanaipotezea siku dereva akiishika wanasema hatutaki kifurushi chako boss wako anakiburi wanamchapa faini za kutosha

Kufupisha maelezo siku moja niliondoka na dereva na faini waoizompiga mpaka kituo cha polisi nikawaeleza nimechoka na nnajua hili suala ni kwasababu ABC nikamwambia Mkuu wa kituo usipolitatua leo liishe kesho napanda ngazi za juu zaidi. Akanitishia kuniweka ndani kuww nafanya fujo pale. nikamwambia unachelewa ungeshaniweka hata sasa( akatishika kidogo). Daima kuna watu wazuri maishani mama mmoja polisi mtu mzima akatafuta namna akaniambia kazia hapohapo. Nikakaza sana Nilichanel lile suala mpaka ngazi za juu kiasi hatimae barabara ile vifurushi vikafa tukaishi huru.

Je ni kweli bila kusimamia haki zetu na msingi ya kweli iwe kikwazo cha kujijenga? Kwa imani yangu be bold simamia ukweli na uwe mkweli hakika warasimu watakupa Njia upite na utakuwa umeshinda dunia inataka uwe FIT to Survive dont give excuses
Sasa angalia muda uliopoteza kudeal na hao wala rushwa kufanya kazi ambayo sio jukumu lako.
Huo muda uliopoteza hapo ulitakiwa uwe kwenye kazi zako za uzalishaji,ni kazi ambazo ilitakiwa hao wakubwa wa polisi wawe tayari wameshafanya na kuandaa mfumo mzuri.
Na hapo wewe ulideal na kituo kimoja tu cha polisi sasa jiulize nchi nzima kuna vituo vingapi vya polisi?
Ndio maana wadau wengi kwenye comment wameelezea mifumo mibovu ndio kikwazo ni si kwamba fursa hawazioni.
Nimepitia comment zote kwa umakini naona bado mtoa mada ameshindwa kuleta ushawishi in a practical sense.
Na uzuri wapo wadau kwenye comment wametoa mifano ya wazi kwamba walishawahi kufanya hizo harakati wakapata hasara utawashawishi vipi kuingiza tena pesa zao kwa matatizo ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi hadi leo
 
Daima usiogope vikwazo keep pushing in the hardest way kwakuwa njia ngumu ndiyo pia ukwepwa na watu wengi
 
Nimeipenda hii na hongera kwa hatua uliyochukua japo nina swali moja, kuna mahali umesema gari ulipokuwa unaeendesha wewe askari walikuwa hawakupigi fine kwa sababu gari halikuwa na shida na kila kitu kilikuwa sawa kuanzia sticker mpaka matairi, lakini pale alipoendesha dereva wako alikuwa anakutana na fine! Nachotaka kujifunza hapa ni kwamba kwanini dereva wako alipokuwa akiendesha alikuwa anapigwa fine ilihali gari lilikuwa sawa kwenye kila kitu kuanzia vibali mpaka sticker? Au tatizo lilikuwa kwa dereva? Kama tatizo lilikuwa kwa dereva kwanini hukumuelekeza dereva kujirekebisha na yeye ili aache kupigwa fine akiwa na gari lako?
Nyingi tu Mara 3 bomba, wakati mwingine kazidisha watu hadi kwenye buti. Kupita kwenye 50 speed.😁 Nakumbuka kuna siku alikuwa na makosa matatu kwa pamoja elfu 90, kwanza moja alisimamishwa akapitiliza kwa madai ya polisi alafu mbele alipofika kituo cha gari hakuingia ndani kupanga folen kusubiri zamu akachora juu kwa juu
 
Watu wanaogopa bureaucracy, sera mbovu za kulinda viwanda vya ndani na gharama kubwa za uzalishaji. Mara umeme umekatika washa jenereta, mara mamlaka hii inataka hiki.

Unazalisha bidhaa kwa gharama kubwa ghafla Mchina anafanya dumping ya bidhaa zake sokoni.
Jibu sahihi hili.
 
Nilichojifunza ili uwe na uwezo wakuzalisha bidhaa kwa ukubwa hata wakutosheleza kata tatu au nne kwanza tafuta mtaji mnono 100m+,ingia siasani chama tawala na uwe mzito uko au uwe mfadhili wa wanasiasa,omba jina la mtu kigogo au mtu ambae yupo sokon tayar,alafu tafuta eneo ndio ufungue kakiwanda kako (ila kumbuka figisu,vikwazo na hujuma hazitokata)
 
Ntafanya mchakato wa kiwanda cha mafuta ya mgando Tanzania ukitaka kuanzisha hapa SA ni mwezi tu documents zote unazo ila huko kazi kweli nilijaribu kufatilia naona kuingiza mzigo ni rahisi kuliko kufungua kiwanda na hakuna uhusiano wa ofisi hii na ingine na wote uwaone aisee..
Hiyo kazi labda umpe mtu afatilie ukitaka ufanye mwenyewe urakatishwa tamaa maana huku ni rahisi na eneo wanakupa wao hata ukitaka kwa mkopo warehouse za kutosha..
Chemical unatoa Durban na Iran..

Mafuta ya kujipaka, hasa haya ya kina Dada ni biashara nzuri.

Unafungua kiwanda chako.
Unatafuta ambassodor wako wawili watatu. Wawe wanakutangazia.

Target wale Middle na High class woman. Wanaofanya kazi maofisini
wanawake wanapenda urembo na wakiyapenda mafuta fulani wanakuwa royal nayo sana.
Wao wenyewe kwa wenyewe wanakufanyia market.

Cha Muhimu ni uwe na Bidhaa bora , package nzuri na inavutia, maelezo mazuri na yanayoeleweka kwenye ingredients na yawe affordable.
 
Daima usiogope vikwazo keep pushing in the hardest way kwakuwa njia ngumu ndiyo pia ukwepwa na watu wengi
Vikwazo inatakiwa viwe Technical barriers na sio personal barriers vya kusababishwa na watu hivi havitabiriki ni ngumu kuvitengenezea kanuni maana hujui atakuja nani na muda gani na atahitaji kiasi gani huoni hii itakuwa inakuvurugia bajeti zako kila siku.
 
Sasa angalia muda uliopoteza kudeal na hao wala rushwa kufanya kazi ambayo sio jukumu lako.
Huo muda uliopoteza hapo ulitakiwa uwe kwenye kazi zako za uzalishaji,ni kazi ambazo ilitakiwa hao wakubwa wa polisi wawe tayari wameshafanya na kuandaa mfumo mzuri.
Na hapo wewe ulideal na kituo kimoja tu cha polisi sasa jiulize nchi nzima kuna vituo vingapi vya polisi?
Ndio maana wadau wengi kwenye comment wameelezea mifumo mibovu ndio kikwazo ni si kwamba fursa hawazioni.
Nimepitia comment zote kwa umakini naona bado mtoa mada ameshindwa kuleta ushawishi in a practical sense.
Na uzuri wapo wadau kwenye comment wametoa mifano ya wazi kwamba walishawahi kufanya hizo harakati wakapata hasara utawashawishi vipi kuingiza tena pesa zao kwa matatizo ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi hadi leo
Hiyo Nchi ni kama wamerogwa bidhaa hazina usumbufu kuleta kuliko mitambo niliwahi kuleta Log mashine walisumbua kama wiki hivi kila mtu anaongea lake kwenye kulipia mara wanataka usajiri wa blue kadi kama gari unawaambia hii ni Yellow mashine SA haziruhusiwi kupita kwenye bara bara zao inatakiwa ibebwe kitu chenye usajiri ni kinachopita road mashine ya kubeba mbao porini huku mnasajiri wao hawasajiri hata mitambo ya kutengeneza bara bara daah watapiga simu huku na huko ili mradi wakusumbue tu.
 
Nilichojifunza ili uwe na uwezo wakuzalisha bidhaa kwa ukubwa hata wakutosheleza kata tatu au nne kwanza tafuta mtaji mnono 100m+,ingia siasani chama tawala na uwe mzito uko au uwe mfadhili wa wanasiasa,omba jina la mtu kigogo au mtu ambae yupo sokon tayar,alafu tafuta eneo ndio ufungue kakiwanda kako (ila kumbuka figisu,vikwazo na hujuma hazitokata)

Mm nadhan huku mbali sana Mkuu.

Ni kiwanda gan unataka kufungua?.
Mradi umeshauandika chini?.

Fuata procedure na anza kwa kiwango kidogo.
Jipe hata mwaka wa kufanya maandalizi kabla hujazalisha products zako.
Na ukianza unaanza uzalishaji kidogo kidogo.

100m ni nyingi. Na huo ukiritimba unaouongelea sio lazima ufanyike.
 
Mafuta ya kujipaka, hasa haya ya kina Dada ni biashara nzuri.

Unafungua kiwanda chako.
Unatafuta ambassodor wako wawili watatu. Wawe wanakutangazia.

Target wale Middle na High class woman. Wanaofanya kazi maofisini
wanawake wanapenda urembo na wakiyapenda mafuta fulani wanakuwa royal nayo sana.
Wao wenyewe kwa wenyewe wanakufanyia market.

Cha Muhimu ni uwe na Bidhaa bora , package nzuri na inavutia, maelezo mazuri na yanayoeleweka kwenye ingredients na yawe affordable.
Hivi vilishafanyika tayari na changamoto zinarudi palepale kwenye umeme na malighafi zingine sasa ukishazalisha ukipiga hesabu utajikuta chupa moja ya mafuta hadi kukamilika imekugharimu elfu 20 wakati chupa moja ya mafuta kama hayo kutoka china yanauzwa elfu 7 na wamekuzidi kwenye ubora hapa ndio changamoto ilipo wabongo wanapenda vitu vya bei cheap.
 
Hiyo Nchi ni kama wamerogwa bidhaa hazina usumbufu kuleta kuliko mitambo niliwahi kuleta Log mashine walisumbua kama wiki hivi kila mtu anaongea lake kwenye kulipia mara wanataka usajiri wa blue kadi kama gari unawaambia hii ni Yellow mashine SA haziruhusiwi kupita kwenye bara bara zao inatakiwa ibebwe kitu chenye usajiri ni kinachopita road mashine ya kubeba mbao porini huku mnasajiri wao hawasajiri hata mitambo ya kutengeneza bara bara daah watapiga simu huku na huko ili mradi wakusumbue tu.
Ndio hivyo mkuu yaani unaweza ukaplan kufanya jambo la kimaendeleo lakini baadae inakutokea puani hadi unajuta kwa nini ulifanya yaani unapata usumbufu utadhani mtuhumiwa wa kesi fulani
 
Hivi vilishafanyika tayari na changamoto zinarudi palepale kwenye umeme na malighafi zingine sasa ukishazalisha ukipiga hesabu utajikuta chupa moja ya mafuta hadi kukamilika imekugharimu elfu 20 wakati chupa moja ya mafuta kama hayo kutoka china yanauzwa elfu 7 na wamekuzidi kwenye ubora hapa ndio changamoto ilipo wabongo wanapenda vitu vya bei cheap.

Kwanza, kwenye Biashara kila mtu ana mteja wake. Kwahiyo Tusiogope bidhaa kutoka China, yeye atauza na ww utauza.

Pili, nadhan mfano wako hauko realistic, 20k vs 7k ni parefu sana.
Hebu tolea mfano halisi wa bidhaa gani ili tuone by how far kuna diff in cost of production.

Umeme Sikuhizi sio kama zaman.
Pia unaweza kuwa na Generator dogo kwenye hizo hours ambazo umeme hauko.

Malighafi inaweza ikawa shida.
Hasa kama ni chemical.
Ila wapo waigizaji wa Chemical wenye Leseni wengi maeneo ya mandela road. Unaweza ongea nao . Ili wakiwa wana import chemical zao wakaadd na zako.

All in all.
Vikwazo viko, ila Kuviruka inawezekana.
Penye Nia pana Njia.
 
Unamaanisha bei ya umeme imeshuka?Unit moja tunauziwa kwa 300 unasema imeshuka?
Mkuu tafuta wanaozalisha products Tanzania kisha linganisha na bei za kutoka nje kama zinafanana mbona vitu viko wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom