UDA imebinafsishwa ili iingie Biashara na DART - Siri ya kuuzwa Bei Chee

ni hatari zaidi ya hatari yenyewe, hiyo ni UDA tu inayoonekana kwenye macho ya watanzania hawa maskini, ni mangapi mazito zaidi ya hayo yaliyojificha kwenye mashirika ya umma na mikataba mingine yenye utata ambayo maskini hawa walipa kodi hawaijui?

 
Ninashangaa wabunge na mawaziri wanalumbana.
Rais wa JMT aliapa kwa kutumia katiba kulinda mali na watu wa JMT.

UDA ni mali ya watu. Kuna vitu viwili, mali na watu. Hivi inakuwaje mali ya taifa hili inauzwa Rais wa nchi akiwa hajui.
Shirika kama UDA kwa nchi masikini kama yetu limekula kodi za watu sana.
Ndiyo mali ya masikini, leo tunaambiwa mawaziri na wabunge wananyosheana vidole Rais akiwa kimya kana kwamba hakuna kinachotokea.

Acheni kulumbana, huu ni muda wa kumuuliza aliyeapa kulinda mali zetu Mh Rais, UDA imeuzwaje, kwa utaratibu gani, nani walihusika na kwasababu zipi.

Itakuwa ni kituko Ofisi ya Rais ikisema haikuhusika. Itakuwa haikuhusika vipi wakati ndiyo inayolinda mali zetu.
Nani mwenyekiti wa cabinet, na kwanini wabunge na mawaziri walumbane wakati mwenyekiti wa baraza la mawaziri yupo kimya.

Hivi kesi ile serikali iliyoshindwa, haikutosha kumwambia mwenyekiti wa baraza la mawaziri kuwa kuna tatizo.
Leo, Takukukuru, Polisi na intelligence ya nchi zinafanya kazi kulinda watu na si mali za watu. Nani mkubwa wa vyombo hivyo. Kwanini mlumbane wakati mwenye ngoma kakaa kimya ! mnacheza ngoma gani ikiwa manju hataki kupiga fiilimbi.
 
Ukweli huwa unasimama wenyewe; hauitaji kusimamishwa; unahitaji kuoneshwa tu. Wabunge na wote wanaozungumzia suala la UDA kwa kiasi kikubwa wanakwepa kusema ule ukweli... wanazunguka mbuyu..
 
Ukweli huwa unasimama wenyewe; hauitaji kusimamishwa; unahitaji kuoneshwa tu. Wabunge na wote wanaozungumzia suala la UDA kwa kiasi kikubwa wanakwepa kusema ule ukweli... wanazunguka mbuyu..
Ndio maana hapo juu nimesema, hakuna sababu za mawaziri na wabunge kulumbana.
Wanachokifanya ni kucheza ngoma, kitu cha ajabu mpiga ngoma ambaye pia ni mpiga zumari kakaa kimyaa, sijui wanacheza mirindimo gani. Unachezaje ngoma isiyopigwa!

Hili ni suala la Rais kueleza umma, mali aliyoahidi kuilinda kwa katiba, tena akisema na watu wake imekuwaje?
Wabunge hawana chombo chochote cha dola, kikubwa wanachokifanya ni kusotana madole ya macho.
Ni sawa na akina dada pale mtaani wakiwa wamefunga vibwebwe wanatishiana, utaona! utaona!

Mwenye ngoma ni Rais Kikwete, kakaa kimya mnaulizana wenyewe kwa wenyewe.
Watu wanataka kuuziwa mafuta ya gari kutoka wodi ya Mwaisela, wakijua fika kituo cha mafuta wamekiacha faya
 
Rekodi yangu juu ya utawala wa kifisadi bado inasimama. Tuliandika hili miaka minne iliyopita. Yametimia.
Unajua Mzee Mwanakijiji, msimamo wangu toka siku ile nilipojiunga rasmi na JF, haujayumba...nilidhani naungana na watu wenye uchungu wa kweli na taifa hili na wanakerwa haswa na tunakoelekea. How wrong I was! Siku hizi kuna posts humu nikizisoma natokwa na machozi ingawa hizo ni posts tu kwenye mtandao. Lakini linalofunga mwaka ni kwamba nimebahatika kukutana uso kwa uso na baadhi ya wachangiaji...oh my God, huwezi kuamini wanayoyatetea kuhusu hatma yetu kitaifa! We are but zombies, the walking dead I see in movies. We Tanzanians are not real, just a fake specie that ought to be extinct!
 
Last edited by a moderator:

Mzee mwenzangu; bila ya shaka naweza kuwahesabu watu wachache tu humu ambao hawaatetereka katika mapambano haya. Ukijua ni jinsi gani angalia jinsi gani watu wanazungumzia CCM na wagombea wake as if wana legitimacy ya kupewa hata siku moja ya ziada kuongoza. Yaani watu wameona madudu yote na wanaua ni nani kaliingiza taifa hapa lakini bado tunazungumza kana kwamba labda tujaribu tena.. miaka hamsini na ushee hatujachoka tu...
 
Niliwahi kufikiri kama nikichaguliwa kuongoza Tanzania nitaweza? Nilikuwa nawaangalia watu wa zama hizo. Siku hizi ndoto hizo hazipo maana najua ninaweza, tatizo kubwa linalonisumbua ni pale ninapofikiri aina ya suti zitakazonipendeza

Watanzania ni watu wasahaulifu, wanaongelea matukio na wanaoshangilia hata jogoo kuchi wakipigana.

Leo wanasema fulani anafaa kuwa Rais, kesho wanasema shilingi inaanguka thamani.

Yaani wanadhani shilingi inapanda thamani kama kishada, na kuanguka kama tunda damu.

Leo unawaibia kesho wanakuita mjasirilia mali tena wanakualika katika harambee

Leo wanasema wanapigika kicuhumi, kesho wanakwambi 'huyu' anafaa ataleta lile kontena la ubuyu a.k.a maendeleo

Hawajishughulishi kabisa kufikiri tatizo ni kitu gani
 

Oh Nguruvi; you couldn't have said it better. Ni watu hawa hawa ambao wanalia umaskini na ndio hao hao wanashangilia kuwaingiza wale wale waliowafikisha kwenye umaskini huo. Angalia mikoa inayoitwa "iko nyuma kiuchumi" utaona ndio hiyo hiyo inayochagua kwa wingi CCM. Go figure.
 
Jenerali alilisema hili vizuri sana katika toleo moja la Raia Mwema, nanukuu;
Jenerali Ulimwengu said:
Tunachagua kama vipofu, kisha tunalalama kama vichaa. Sasa tuamue: ama tuchague viongozi wetu kwa makini, au tukae kimya wakati wakitunyanyasa. Wachagua hovyo wasiwe wasema hovyo wakitendewa hovyo.
 
Kizazi chetu hiki hakiko tayari kwa mabadiliko, labda kizazi kijacho cha watoto wetu!
 
Hivi hawa viongozi wetu kuna kitu wanafanya kwa manufaa ya taifa lao kweli?? Yaani inchi imekuwa kama haina watu wa kuingoza kila sehemu ni ufisadi, ufisadi. Hakuna tunachoweza kujivunia si shule tumeshindwa, si hopital tumeshindwa, viwanda tumeshinda, barabara tumeshindwa. umeme ni kero tu.. yaani kila sekta sisi ni zero.. Halafu kuna watu wanatafuta ndani mwa watu wale wale waliofeli kila kitu kupata kiongozi bora..

Hivi sisi watanzania tumelogwa? mtu yuko serikali miaka 20, 30 hakuna alilolifanya la maana halafu leo huyu mtu ndo tumpe uongozi na kutegemea miujiza!!.. Hivi kweli kweli kwa akili za kawaida tunaweza kupata kitu kipya kwa watu wale wale, wenye mitizamo ile ile na mawazo yale yale?
 
Alinda, naomba nitofautiane nawe kuhusu viwanda.
Viwanda hatujashindwa, tumegawa zawadi na vingine kugeuza maghala ya chumvi.

Kuna kiongozi kasema nchi hii ipo katika auto-pilot, nadhani ni kweli.
Sidhani kama Tanzania inahitaji viongozi, inaweza kwenda kwa solar energy

Watanzania ni watu wa ajabu sana. Wanafanya jambo lile lile kwa miaka 50 bila matokeo tofauti na wanategemea kufanya namna ile ile kwa mara nyingine wapate matokeo tofauti.

Watanzania wanaamini kwa dhati kabisa '' unaweza kupata malaika kutoka miongoni genge la wahalifu''

Tena watanzania wapo busy wakiwakatasa majambazi kwa ''kuwavisha nguo nyeupe na mabawa ili wawe malaika''
 
Miaka nane nyuma.. haki inaweza kuchelewa lakini inaweza kufika
 
How times change, how time flies fast, how time and tide waits for no man...kweli hujafa hujaumbika!
 
Miaka nane nyuma.. haki inaweza kuchelewa lakini inaweza kufika
Exactly tulichosema ndicho kinachoonekana

Kuna somo hapa, si yale yaliyosemwa bali waliosema. Waliolieleza hili kwa uchungu kwa bahati nzuri hawakuitwa wasaliti! Walipuuzwa tu pengine kwa kuitwa wapuuzi

Watu hao hao wakisema yale yale siku hizi wanaitwa wasaliti

Somo la pili, uzalendo si tukio la msimu na wala haupandikizwi. Uzalendo ni kitu 'intrinsic'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…