Hii scene ilipangwa tu
1. Kwanza unakamatwa kwa purukushani na inadondoka begi lenye vitambulisho wala si simu wala kingine! Ni ili watu watambue katekwa Nani
2. Millard Ayo anafanya coverage ya masaa 24 ku report kinachoendelea wakati siyo tabia yake
3. Inatoka report ya polis aina ya plate number wanazotaja ni tofauti na Plate number zinazotajwa na wananchi japo zote feki,
4. Gari lililomteka likaonekana limepaki sehemu kabisa baada ya tukio tofauti na matukio ya utekaji yaliyopita! Yaan wazi wazi ili sign ionekane liko polisi Gogoni
5. Anapatikana usiku anaomba boda boda imfikishe kwenye makao makuu ya chama kwanini hakuna hata shahidi Aloona anatupwa pale usiku?
6. Je kwanini viongozi wa chama wawe ofisi usiku kabisa wakisubiria atakapo rejeshwa akodi piki piki ndo wampokee? Au walioteshwa?
7. kabisa Taarifa za anayesema aliletwa na bajaji Lakin Polisi wanasema ni boda boda ilimpeleka makao ya chama !
Any away utekaji si mzuri tuzuie kwa namna yeyote ile
Polisi wameendelea kusisitiza kupitia kila taarifa waliyoitoa kwamba Amekamatwa kwa nguvu.
Kwa sisi wamachinga tunaoffanya shughuli zetu hapa Magufuli bust stand tunajua vizuri sana kwamba eneo hili lia ulinzi madhubuti. Hapa mtu hawezi akatekwa, kama ilivyofanyika halafu watekaji waka get awaywith it.
Polisi wapo sahihi, wanaposema alikamatwa kwa nguvu na watu wasiojulikana" inawezekana ilikuwa ni Taskforce Operation (With Police Stand-Down), hivyo Polisi walitaarifiwa lakini hawakutakiwa kuingilia.
Ndiyo maana kila walipotoa taarifa yao waliendelea kuuhabarisha umma kwamba "Amekamatwa kwa nguvu"
ingawa hawajui mkamataji ni nani. Kuna wakati Polisi hulazimika kupokea maagizo na kuyatekeleza pasipo kuhoji.
Kuna level Askari ni mpelelezi, anauliza maswali, anaumiza kichwa kufikiri ili kupata majibu, kuna levels askari akitaka kuchangia ku comment na kufanya reasoning na ku make sense huambiwa "a soldier is hired to act not to think"
Kwenye hoja ya kupangwa kwa hii scene. Hili ni mbaya sana, huku ni kujaribu kuizoesha jamii ikubalianena mambo ya hovyo. Kuna watu wametekwa na wameenda mazima, hadi leo hatujui walipo. Kuna waliotekwa wakapatikana wakiwa na hali mbaya, na kuna waliotekwa wakaja kupatikana wamepoteza maisha.
Sasa kinapojitokeza kikundi kutaka kuizoesha nchi ione matukio haya ni ya kawaida, hawa jakika siyo watu wanaostahili heshima, heri wala jema lolote