Udadavuzi huru: Kuna ukakasi kwenye Taarifa ya Polisi juu ukamatwaji wa nondo, ama Nondo au Polisi kuna muongo

Wamesema katupwa akiwa katika hali mbaya, sasa kwa nini wasamalia wema walimpeleka kwanza makao makuu ya chama badala ya kumpeleka hospitali?
haya wangempeleka hospitali wangeambiwa PF 3 ya polisi..au hujui utaratibu wa nchi hii watu wanakosa huduma hospitali tena kwa majeraha madogo kisa PF3
 
niliona taarifa ya kibwengo moja mitandaoni eti muungwana hajiwezi kwa chochote na anaongea kwa tabu sana...

nikajiuliza, hivi kulikoni hasa uache kusema ukweli na ung'ang'ane na ukweli na uzushi?🐒
 
Reactions: Tui
Labda tuulize niyapi mazingira ambayo japo yanahisiwa kuwa sababu inayoweza kuwa ilipelekea kutoweka kwake?
 
Pia katika yote hadi huko Aga Khan hakuna cha picha wala video. Hii inaacha maswali. Kwamba kuna aliyewazuia wasipige picha?
Nenda pale Agha Khan kampige picha halafu njoo u-upload hapa. Kabla huja weka hapa tuage kabisa.
 
Na wewe umafuata mkumbo wa Nyumbu...
Tusubiri atapi jitokeza. Tutathaminisha muonekano wake...
 
Kuna kikundi behind the scene chenye uchu wa madaraka ndicho kinachoratibu mipango yote hii.. Kiliwahi kuisumbua sn hata awamu ya tano sasa kinadili na Kizimkazi Empire mpaka aachie ngazi .. lengo kupigania madaraka ili kumege keki ya taifa.
Ni sanaa ambazo zinawaumiza wanaotekwa lakini hazina uwezo wa kumuondoa Rais Samia katika kile kiti alichokalia muda huu.
 
Samia na Serikali yake hawahusiki...Kuna kitu kinaendelea,Nondo anajua vzr Sana.
 
Coco beach.imejaa.askari mida.wote hawa.wanaovaa.kiraia na.wale.wa.tigo mpaka kwenye vichaka vile.
 
Umechambua vizuri .Maana mimi naona NONDO na Act wazalendo wake wametengeneza igizo lisilo ingia akilini kabisa .Uchambuzi wako ungefaa kila mtu asome ili kupanua wigo wa mjadala huu wenye lengo la kutaka kuichafua serikali
 
Umechambua vizuri .Maana mimi naona NONDO na Act wazalendo wake wametengeneza igizo lisilo ingia akilini kabisa .Uchambuzi wako ungefaa kila mtu asome ili kupanua wigo wa mjadala huu wenye lengo la kutaka kuichafua serikali
Kama lile la Mama wa BAWACHA umesikia kelele tena?.Mmoja wa viongozi Maharage akihojiwa amedai kwamba Nondo alizungushwa siku nzima ndani ya Land Cruiser bila ya kuteremshwa.
Zitto kadai kwamba Land Cruiser wameiona imepakiwa Gogoni Police Station kabla ya Nondo kupatikana.Ni detail ndogo lakini inatia shaka kwenye "historia" nzima.
 
Wamemwachia baada wazee wa kigoma kusema waliomteka mtoto wetu mmemteka ila kitakacho wakuta tusilaumiane .na unajua kigoma wanapenda mambo ya ndumba uchawi mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…