Udaktari: Kwa mwenye uzoefu na ujuzi naomba anipe muongozo

Miaka 14-15 sio mchezo, ila nipo kwenye nafasi kama yake lakini kwangu ni 5 tu.

Asivunjike moyo tu kuna raha sana ya kufanya kitu unachokipenda.

Wewe 5years utafananisha na 15?? Unampa moyo mwenzio eeh 😁😁😁 haya bwana
 
Umesema ulishindwa kusoma pcb kwasabab hukuwa na hela...duh.au uliona hutoweza hiyo kombi kwa kuwa ni ngumu!

HAPANA.pesa za kujikimu tu ilikuwa shda..sasa ukifikiria safar za kwenda dar na hakuna wa kukupokea kama mwenyeji ikawa shida..ama hakika haikuwa ngumu. kila somo ni gumu kwa kadiri ulipangavyo,..huwez amini nafeli kiswahili mpaka kesho
 
JUMLA YA MIAKA:3DIP+5MD+1INTERN+3MMED+2SUPER-SPECIAL=14 YEARS
NOTE:HIYO MIAKA HAPO HAUJAFANYA KAZI HATA MWAKA MMOJA.[/QUOTE]

Asante mkuu kwa mchanganuo mzuri...
 

Najua kuna competitions kubwa sana za kuingia kwenye course ya Medicine (na hata kozi za Engineering) kwa vyuo vizuri duniani. Ila kwa Tanzania ni tofauti, kila mtu akipenda kusomea udaktari au engineering anaweza akafanikiwa. Nadhani tuna vyuo vitatu tu ambavyo walau viko strict katika kuchagua wanafunzi wa kusomea udaktari kwa hapa Tanzania - Muhimbili, Bugando, KCMC; lakini bado wanafunzi wanaoteuliwa na walimu wa kufundisha wenye sifa ni tatizo kuwapata.
Mwanzisha thread katika mazingira yetu yasiyokuwa strict, waweza timiza ndoto zako; lakini ungekuwa nchi za watu ningekwambia sahau. Kama bado wataka usomee udaktari wa binadamu labda nenda kasomee Physics, Chemistry na Biology ili uwe na sifa upate nafasi ya moja kwa moja kwenye vyuo hivyo vitatu juu.
Lakini kuna vyuo kama Kairuki na IMTU ambavyo si vigumu. Unaweza kwenda kuuliza mwenyewe kujua pre medical courses zao zahitaji sifa gani. Pia una option ya kusomea course ya "Clinical Officer", lakini wahitaji ufaulu sana ili baadaye uweze kupata nafasi ya kusomea udaktari.
Pia waweza kujaribu kuangalia uwezekano wa kwenda nchi za Ulaya ya Mashariki, kama Ukraine na pia Russia ambako ni rahisi sana kusomea 'udaktari' ingawa wengi wa wanafunzi wetu wanaoenda huko hurudi wakiwa "mabomu".
Kwa yote. Udaktari ni course ngumu na inayohitaji mwanafunzi kuwa na akili sana. Kupenda tu hakutoshi.Tanzania tuna changamoto ya kuwa na wanafunzi wachache wenye sifa stahili za kusomea Udaktari. Hili hata Prof. Mtabaji wa Bugando (Principal wa zamani wa Muhimbili) kalitaja sana. Upungufu huu umesababisha tupeleke hata mazezeta kusomea Udaktari. Shida tupatazo wote twaziona. Ila wanafunzi wengi hawastahili kusomea udaktari.
 
ndugu OZZIE,..kama ni suala la kusoma na kutendea kazi kile nachosoma(practical) nakuahidi ntawafurahisha mpaka wakufunzi wangu...ila cjawa geneous,huwa najisomea kwa uhakika
 
ndugu OZZIE,..kama ni suala la kusoma na kutendea kazi kile nachosoma(practical) nakuahidi ntawafurahisha mpaka wakufunzi wangu...ila cjawa geneous,huwa najisomea kwa uhakika
Mungu akusaidie. Ila issue si kuahidi, issue ni kuwa na sifa. Maana siamini kwamba kukosa kwako tuition ndio kulisababisha ukasome EGM. Hata wanaosoma EGM huenda tuition. Tutaongea saaana humu, utakuwa unapoteza muda.
Nashangaa kama kweli unaweza ukawa na passmarks hizo za form IV na bado ukashindwa kujua sifa za mtu kwenda kusomea udaktari!!! Naona kama unasumbua watu.
Lakini pia ukumbuke si kila ndoto au kiu ya moyo hutimia. Na si kila unachotamani lazima kiwe sehemu ya maisha yako. Unaweza penda kuwa Rais, lakini si rahisi kuwa Rais. Waweza penda kuwa engineer, lakini kama ulifanya wrong choices au hukufaulu mwanzoni unakuwa na wakati mgumu ku switch. Maisha ndiyo yanaenda. Sio ukiingia chuo kusomea udaktari ndio ushakuwa daktari, unakuwa umeingia angalau miaka mitano ya stress na kashikashi za ku disco. Kama umefaulu EGM vizuri, endelea upande huohuo, usipoteze muda.
 
ndugu OZZIE,kukaa vijijini kabisa kuna hasara zake..we sikia tu,usiombe...hakuna wa kukupa mwanga...na hata kamwanga kakionekana kwa kpindi hcho unakuta hakuna wa kukushka mkono kiuchumi akufikishe hatua fulani.....na mengi nisiyaseme. ila nimepambana na naanza safar rasmi...nimejaribu kutembelea NACTE,nmeona tangazo,asanteni...ngoja nitupe karata baadae nikishalipitia tangazo kwa makini...jamani umasikini wa pesa ni kikwazo kikubwa kutimiza ndoto za sisi vijana kitaaluma. siwafichi..
 
Mkuu usivunjike moyo kwamba siju kitu gani,ukweli upo hivi,udaktari ni commitment na wala sio kuwa na akili sana wala nini hata mtu mwenye ziro anaweza kuwa daktari mzuri kuliko wewe mwenye one ya saba,.............kiukweli nondo za udaktari ni nzito balaa,lakini uhitaji kuwa geneous kuzimaster,kuna watu kibao wana akili balaa kwenye medical school,lakini:
-wavivu
-hawana moyo wa kutibu
-hawana huruma
-wanaogopa vitu kama damu,vinyesi
etc
kwa sababu hizo hapo juu utakuta mtu amefaulu vizuri darasani lakini ni daktari mbovu,ukienda hospitali nyingi za wilaya utakuta wanaofaya operesheni ni wafagizi wa theatre,so kigezo cha mtu sijui kupiga one mi kwangu ni last option,knowledge ya kawaida tu ya kuelewa unachofundishwa inaweza kukufanya kuwa daktari.
Na ndio maana kwa nchi kama marekani ili uweze kusoma udaktrari huwa wanahitaji COMMITMENT & ANY UNDERGRADUATE DEGREE tu kama factor kubwa.
so kama una-COMMITMENT utakuwa daktari wa level unayoitaka.
 

Bonge la point bro, cku hz kusoma md imekua ka' sifa tu.
 
Mkuu udaktari ni abstract thinking. Unaanza na akili, wito baadaye. Huwezi ukaanza na wito halafu thinking ifuate baadaye. Utakuwa daktari bomu... Unaweza fanya kazi nyiiingi sana, lakini kwa makosa. Na unaweza ukafanya kazi chache sana, lakini kwa uhakika. Bahati mbaya huruhusiwi kufanya makosa kwenye udaktari, maana makosa humaanisha madhara makubwa au kifo kwa mgonjwa...
 

Naomba kusahihisha, si lazima kusoma MMED then Masters of Science in particular field. Waweza kusoma Superspecialization straight away, yaani kusomea Cardiology au Nephrology mara baada ya MD(nikimaanisha mtu aka by pass MMed Int. Medicine) tofauti na sisi wa zamani. Ingawa changamoto ni kukubalika among madaktari wenzio.
 

Well said.
 
Unakijua unachokiongea au unachangia tu mkuu ili mradi kwa ufaulu wake wa o level anaweza kabisa kwenda somea clinical medicine tena kwenye chuo kizuri kwani ufaulu wake ni mzuri sana so acheni kumkatisha tamaa ata ingekuwa wapi angeweza tu kusomea clinical medicine mpaka kuja kufikia malengo yake ingawa itamchukua muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…