Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Professa wa sheria Issa Shivji wa Tanzania anayeheshimiwa duniani na aliyefundisha na kutafiti na kuandika vitabu vingi vya masuala ya ardhi anawakumbusha Watanzania: nchi inauzwa kwa kasi na "Wamawakala wapya wa mabeberu." ambao anasema sifa zao ni "Watawala hawaoni mbali. Siasa zao ni za muda mfupi. Maono yao ni finyu." Na anamalizia kwa kuandika jukumu la kulinda ardhi ya nchi ni la nani.
=========
’TULIPO. TUNAKOELEKEA’ 2 TAFAKURI YA KILA WIKI UPORAJI WA MALIASILI MAMA – ARDHI
PROF. ISSASHIVJI
Jul 7, 2024
Tangu wakoloni wavamie nchi yetu mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, uporaji wa ardhi umeendelea. Katika miongo takriban saba hivi wakoloni walitwaa ardhi ya wenyeji kwa ajili ya makampuni ya nje na walowezi ingawa Tanganyika haikuwa ukoloni ambako walowezi wa kizungu walipora maeneo makubwa ya ardhi kama Kenya au nchi za Kusini mwa Bara kama Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.
Katika miaka takriban sitini baada ya uhuru tena wazalishaji wadogo hususan wakulima na wafugaji wakajikuta ardhi yao inachukuliwa kwa visingizio mbalimbali. Hata nyakati ya awamu ya kwanza ardhi ya wazalishaji haikuwa salama. Taasisi za serikali kama jeshi, magereza n.k walivamia na kuchukua ardhi ya wenyeji na kuzaa migogoro ya ardhi isiyoisha. Kila mara mipaka ya hifadhi inapopanuliwa ardhi ya wakulima na hasa wafugaji inamezwa. Taasisi zingine ambazo zilichukua ardhi ya wanakijiji ni mashirika ya umma. Mifano hai ni ya mashamba ya ngano huko Basotu. Wako pia vibwanyenye kutoka mijini na viongozi wa serikali walichukua ardhi ya wazalishaji – mifano mingi ilitolewa katika juzuu ya pili ya Taarifa Ya Tume ya ardhi.
Pamoja na ukweli kwamba katika awamu zote ardhi ya wenyeji haikuwa salama, katika awamu ya sita uporaji wa ardhi unafanyika kwa kasi kubwa kwa visingizio mbalimbali vya kisasa.
Kisingizio kimojawapo ambacho kimezungumziwa sana na kuathiri hasa jamii za Kimaasai ni upanuaji wa hifadhi. Sakata la Ngorongoro na Loliondo bado lipo. Ingawa habari kutoka eneo lile linakandamizwa, bado mara moja moja taarifa za uaji na mateso ya waMaasai zinavuja. Hata hivyo, vyombo vya habari hawatakikuzigusa na wanaharakati wakishachoka kupiga kelele.
***
Inasemekana serikali ya awamu ya sita ina mpango wa kuongeza maeneo ya hifadhi kutoka asilimia 30 ya ardhi yote ya nchi mpaka asilimia 50, yaani nusu ya ardhi yote ya nchi itageuzwa kuwa hifadhi ili watalii-matajiri na makampuni ya uwindaji waje bila kubughudhiwa na wenyeji. Nchi kama Ujerumani, Umoja wa Kifalme wa Kiaarabu (United Arab Emirates), Benki ya Dunia wanawekeza mabilioni ya dola katika miradi hii.
Vijiji vya KiMaasai pamoja na majengo yao ya shule na zahanati zinabomolewa kwa kisingizio cha kuhifadhi mazingira. Papo hapo wawekezaji wanaruhusiwa kujenga mahoteli na viwanja vya ndege ili wanawafalme kutoka Uarabuni waweze kuja na ndege zao kukaa katika mahoteli ya kianasa na kuwinda wanyamapori! Yaani nchini kwetu wanyamapori na wanawafalme kutoka nje wanathaminiwa zaidi kuliko wananchi wetu wenyewe. Kama kweli nusu ya ardhi ya nchi itageuzwa kuwa hifadhi kwa ajili ya uwindaji na utalii basi tunaelekea kuwa Jamhuri ya Hifadhi ( Republic of National Parks).
Jambo lingine la kusababisha uporaji wa ardhi ni uwekezaji katika maeneo makubwa ya misitu, eti kuhifadhi misitu na kupanda miti ili kuweza kuingia katika biashara ya kaboni. Mwaka jana Tanzania ilisaini mkataba wa maelewano na kampuni ya Dubai Blue Carbon. Chini ya mkataba huu Blue Carbon imepewa eneo la misitu lenye ukubwa wa hekta milioni 8 kuhifadhi misitu na kupanda miti kwa lengo la kushiriki katika biashara ya kaboni. Kampuni hii ya Dubai itauza carbon credits kwa nchi zinazozalisha mafuta na hewa chafuzi inayosababisha tatizo la mabadiliko ya tabianchi. Nchi mojawapo ambayo ni mchafuzi mkubwa wa hewa ni nchi za UAE zenyewe! Kwa hivyo, kampuni ya Dubai itauzia nchi za Kiaarabu carbon credit kusafisha jina lao kama mchafuzi wakati wakiendelea kuzalisha mafuta sambamba na hewa chafuzi! Na hayo yote kwa gharama ya watu wa Tanzania watakao poteza udhibiti na matumizi ya maliasili yao – misitu.
Kwenye hafla ya utiaji saini na Blue Carbon Mhe Waziri na watendaji wengine wa Serikali walisisitiza kwamba miradi ya hewa ukaa ni uchumi mbadala na inatoa fursa kwa Watanzania kukuza uchumi wao kwa kushiriki katika miradi ya biashara ya kaboni. Kwa maana nyingine, wazalishaji mazao ya chakula na mazao mengine yenye soko la ndani wanashawishiwa kudandia biashara ya hewa ukaa na kuachana na uzalishaji chakula. Ni rudio ya uchumi wa kikoloni unaofungamana na soko la kimataifa na kufanya wananchi kuwa wategemezi badala ya kujenga uchumi wa kitaifa unaosukumwa na mahitaji ya ndani. Tunarudia dhambi zilezile za uchumi tegemezi safari hii tukirubuniwa na mawakala wapya wa mabeberu. Wamawakala wapya wa mabeberu.
Mipango inayosukumwa kwa kisingizio cha hifadhi ya misitu na wanyapori ni mbinu mpya wa uporaji maliasili zetu, msingi wake ukiwa mama ardhi.
Suala la ardhi ni nyeti na lilikuwa nyuma ya mapambano na vita ya ukombozi kusini mwa Afrika. Hata mapambano ya mashuja wa Kenya wakiitwa eti MauMau yalikita kwenye uporaji wa ardhi na walowezi. (Wao wenyewe walijiita Jeshi la Kukomboa Ardhi, The Land Freedom Army). Suala la ardhi bado linaendelea kusumbua nchi za Namibia na Afrika Kusini. Sisi kwa sababu za kihistoria tuliepukana na tatizo la ardhi. Lakini sasa badala ya kujifunza kutoka historia, tuko mbioni kujitumbukiza katika kınaması (quagmire) ya tatizo la ardhi.
Suala la msingi kama ardhi (na rasilimali zinazopatikana chini na juu ya ardhi) hatuwezi kuliachia serikali. Watawala hawaoni mbali. Siasa zao ni za muda mfupi. Maono yao ni finyu. Matakwa yao ni ya kibanafsi. Hiki ni kizazi kipya cha watawala kilichokuzwa na mfumo wa uliberali mamboleo; sio tena kizazi kile cha kitaifa na kizalendo kilichotanguliza mbele maslahi ya nchi.
Ni juu ya wananchi wenyewe; wavujajasho wenyewe kulinda rasilimali zao na kuchukua hatma ya nchi yao mikononi mwao.
****************