Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 422
- 893
Mara nyingi mabasi mengi kama sio yote yana stika pembeni zikionesha huduma wanazotoa ni FREE WI-FI na FULL AC lakini ukiingia hakuna hata kimoja.
Inawezekana wakati likiwa jipya lilikuwa na huduma hizo (kwa Wi-Fi) sina uhakika sana maana sijawahi kutumia hata siku moja hata kwenye basi jipya, angalau AC huwa wanajaribu basi linapokuwa jipya.
Kwa mfano nikakata tiketi kwa sababu nimeona kuna Wi-Fi na AC halafu nisivikute ndani yake, swali ni je naweza kuishitaki kampuni husika kwa kunisababishia usumbufu.
Na kama hivyo vitu havipo kwa nini wasibandue hizo stika. Au kumdanganya abiria ni njia inayokubalika kisheria? Maana mabasi mengi yana stika hizo na LATRA sijui SUMTRA hawachukui hatua yoyote kuzuia udanganyifu huo.