Captain kanyau
New Member
- Jul 26, 2022
- 3
- 1
Bunge letu bado ni dhaifu katika maamuzi
Leo naomba nizungumzie bunge hasa nikizungumzia kazi zinazohusu bunge na wajibu wa muhimili huu mkuu wa nchi katika ile mihimili mitatu mikuu nchini. Katika nchi zenye demokrasia kama zetu bunge ndio chombo kinachofanya maamuzi ya mwisho yote hiyo ni kwa sababu ndio chombo pekee kilichopewa dhamana ya kutunga sheria zitakazotumika katika nchi husika. Pia ndio chombo kinachoshughulika na maswala yote ya katiba katika nchi. Ukiacha hizo sababu zote bunge ndio chombo cha mwisho kujadili na kupitisha katiba ya nchi tayari kwa matumizi katika nchi.
Sababu za kuzungumzia bunge letu ni kwa sababu kwa mujibu wa utafiti wangu nimekuja kugundua wananchi wengi ndani ya nchi yangu hawana imani kabisa na bunge letu. Bunge kama chombo kinachotunga sheria na kupitisha katiba katika nchi yetu lakini limekua halina nguvu kimaamuzi hasa katika kuwawajibisha baadhi ya viongozi ambao wanakwenda kinyume na miiko ya kiuongozi.
Wengi wa wananchi wakisema bunge linafanya kazi kinyume na matarajio yao. Bunge limeshindwa kuwawajibisha viongozi wanaoiba fedha za umma kwa kujinufaisha kwa maslahi yao binfsi. Pia baadhi ya viongozi kufanya maamuzi au kufanya vitu kwa kutumia weledi wao bila kushirikisha bunge ambalo ndio lenye ruksa ya kuamua na kujadili jambo linalohusu taifa kwa ujumla.
Kwa mfano kesi kubwa za uhujumu uchumi kwenye nchi yetu ambazo zilihusisha viongozi wetu wakubwa katika nchi hii. Kesi ya ufisadi kama ya ununuzi wa rada au escrow ni mifano ya kuonyesha bunge letu halina nguvu yoyote kimaamuzi katika kuwawajibisha viongozi wanachukua fedha za umma kwa maslahi yao binafsi huku fedha hizo zikiwa ni kodi ambazo wanalipa wanachi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Pamoja na viongozi hao waliohusika katika ufisadi huo kukutwa na hatia bado haikutosha kwa wao kuwajibishwa kwa namna yoyote zaidi kujiuzuru nafasi zao za kiuongozi na kuachwa waendelee na maisha yao wakiwa na fedha au kodi walizoibia wananchi.
Pia bunge limekua halina sauti wala mamlaka hasa kwa kumpa mamlaka makubwa raisi wa nchi kufanya maamuzi makubwa ya nchi bila kushirikisha bunge. Mwaka 2011 iliundwa tume kwa ajili ya kuchukua maoni kwa wananchi ili kuundwa kwa katiba mpya.
Tume hiyo ikiongozwa na jaji WARIOBA ambae alishawahi kua waziri mkuu wa zaamani wa nchi. Pamoja na kupita nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi lakini bado haikufanya katiba hiyo kujadiliwa wala kupitishwa.
Ingawa ilitumika gharama kubwa ambazo ni kodi za wanachi kwa tume hiyo kuchukua na kukusanya maoni hayo. Lakini pamoja na hayo bunge halikuweza kujadili wala kutoa maamuzi ya hasara iliyopata serekali kupitia mchakato huo wa kukusanya maoni kwa ajili ya katiba mpya na isipitishwe.
Na tokea mchakato huo usimamishwe hakuna nguvu yoyote kisheria ambayo inataka mchakato huo uendelee pale ulipoishia. Wananchi wanasema kama bunge letu limeshindwa kuona umuhimu katika jambo nyeti kama hilo ambalo ni kwa faida ya nchi je majambo mangapi ya maana yanashindwa kupitishwa pasina wao kujua.
Mwaka 2017 mwanasiasa maarufu wa hapa nchini kwetu na aliyekua mbunge wa singida mashariki na mwanasheria mkuu wa chama kikuu cha upinzani tanzania chadema alipigwa risasi kumi na moja na watu wasiojulikana wakati akiingia kwenye makazi yake mkoani dodoma.
Pamoja na kukutwa na kadhia hiyo ambayo ingepelekea kukatisha maisha ya kiongozi huyo bado haikutosha kuundwa kwa tume ya kuchunguza tukio hilo na hata bunge halikuwahi kutilia mkazo tukio hilo ambalo lilimuhusu mbunge mwenzao.
Wala Bunge halikuwahi kupiga kelele kuundwa kwa tume ili kuchunguza tukio lile la mbunge mwezao kupigwa risasi kwenye makazi ya viongozi ambayo kisheria maeneo hayo ambayo wanakaa viongozi na ulinzi mkali lakini kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari inasemekana siku hiyo wakati tukio hilo likitokea hakukua na ulinzi wowote.
Katika miaka kumi ama kumi na tano iliyopita wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali (CAG) wamekua wakitoa takwimu za matumizi ya fedha katika miradi mbali mbali na wizara mbalimbali nchini na kuonyesha kwamba kuna viashiria ama matumizi mabaya ya fedha za umma. Huku akiainisha baadhi ya miradi na wizara ambazo zimeleta hasara kwa nchi aidha kwa fedha za umma kupotea ama miradi husika kutokuisha kwa wakati na kuisababishia serikali hasara.
Pamoja na taarifa hizo zinazotolewa na wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali bado haikotosha kwa bunge kuchukua hatua yoyote kwenye taarifa hizo za kupata hasara kwa nchi nyingine zikionesha kuna ufisadi wa fedha za umma kwa mtu mmoja kuchukua fedha kwa maslahi yake binafsi. Na kumekua hakuna kesi zozote za wahujumu uchumi ambazo zimewasilishwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.
Hii ikimaanisha kwamba takwimu ama taarifa za wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali hazina faida yoyote ya kutangazwa kwa maana hakuna hatua yoyote ya kisheria inayochukuliwa ama kufanyiwa kazi kwenye taarifa hiyo.
Kwa minajili hiyo wananchi wengi hawana imani na bunge lao. Na kusema bunge letu halina nguvu ya kikatiba kama inavyotakiwa kufanya kazi yake na kwamba bunge hilo linaendeshwa kimazoea ama limebaki ni kama jengo tu linalotumika kwa wabunge kukutana.
Mwisho kabisa wananchi wanahitaji katiba mpya ambayo italipa nguvu bunge letu tukufu na serikali ya muungano wa Tanzania kuamua maswala makubwa yanayohusu nchi.
Imeandikwa na abasi issa au captain kanyau
Email: captainkanyau@gmail.com
Tel.+255718554586.

Attachments
Upvote
0