Udhaifu wa marais unawapa umwamba sampuli za akina Mwigulu Nchemba

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
762
Reaction score
1,236
Mfano mzuri ni tabia ya Mwigulu ambayo ilivumiliwa na marafiki kama akina Kikwete kwa sababu zao za kiharibifu hadi kupewa nafasi kubwa ktk CCM. JPM akamuondoa ktk uwaziri. Sasa ameingia rais ambaye wengi tunaamini anashauriwa. Bahati mbaya wanaomshauri ni wale wale wenye akili ya kiharibifu, Mwigulu kaonekana tena eti anafaa sana kupewa wizara! Naye karudia upuuzi wake kwa kasi zaidi.

Anajivunia Ph.D ambayo hajawahi hata kuonesha kipya kilichomo ndani ya kabrasha lake. Hajawahi kuandika chapisho lolote ili kuonesha kwamba amegundua jipya. Yeye kila leo ni kusema ana Ph.D. na katuonesha njia ya kwenda Burundi kwenye unafuu wa maisha. Inasikitisha kwamba mafanikio ya watu kama akina Nchemba ni matokeo ya udhaifu wa marais wanaokua madarakani.
 
Huyo jamaa nikisikia tu jina lake nataman nimnye usoni tena ule muharisho yan simpend simpend kibur kimemja km hii tanzania ni ya kwake viongoz wengin ni km muharisho tu
 
Kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa hapa nchini, Rais wetu Mama SSH itampasa afanye mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Huku bado kuna janga la kukabiliana na wimbi la tatu la UVIKO 19, huku shinikizo la madai ya katiba mpya, huku vilio nchi nzima kutokana na tozo mpya za kodi katika miamala ya simu, na huku bado kuna mengine mengi ambayo yanayofukuta chini kwa chini.

Inampasa asimame thabiti katika nafasi yake kama kiongozi wa nchi, akwepe ushauri wenye chuki za kiitikadi kutoka kwa wahafidhina waliopo katika chama chake ambao baadhi yao ni wenye ushawishi wa nguvu kwake aliowarithi kutoka kwa mwendazake. Atekeleze nia yake njema ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani ili kupunguza fukuto la kisiasa linaloendelea hivi sasa hapa nchini ili aweze kujielekeza zaidi katika kufanya siasa za maridhiano ya kitaifa.
 
Kafanye kongamano tuu la Katiba utajua Mwamba ni Mwigulu au Rais
Sehemu kubwa ya watu hawa wanaegemea kwenye urafiki binafsi badakla ya uwezo wao ktk nafasi.
Angalia Mwigulu wa Kikwete alivyokuwa mwamba, akawa mnyonge enzi za Magufuli, sasa tena kawa mwamba.
Angalia Kabudi wa leo na yule wa enzi ya Magufuli.
Angalia Jafo wa leo na yule wa enzi ya Magufuli
Angalia Gwajima wa afya na enzi za Magufuli

Kwa hili la Nchemba hadi atukane wa-TZ hivi, shida iko kwa rais. Yeye anaona kapata jembe la kisiasa, kumbe jembe linadeka.
 
Mambo mengine yanafikirisha sana, nilidhani wamejifunza kwa yule aliyekuwa anatamba na digrii zake nne kwa wajumbe.
 
Leo imetimia miezi minne na siku kadhaa toka Mama SSH, Rais wa JMT alipochukua madaraka yake rasmi katika nafasi hii nyeti ya kuliongoza taifa letu. Nachelea kusema ya kuwa kuna shida sehemu fulani kutoka kwa wasaidizi na washauri wake.

Toka alifofikisha siku 100 za utawale na hatimaye kufanya mahojiano na wahariri wa vyombo vya habari, naona majibu aliyoyatoa kwao yameanza kuleta fukuto na mihemuko mipya ya kisiasa nchini. Kuna misimamo ambayo anaweza kuishikilia yeye binafsi na kuelekeza ifanyike ili kuepuka matumizi ya nguvu ya polisi hapa nchini.

Hoja za kisiasa hupaswa kujibiwa kisiasa na kupitia wanasiasa endapo tu kama zipo kisheria na zinakubalika kikatiba. Kuanza mapema hivi kuruhusu wakuu wa mikoa na wilaya, polisi na hata maafisa vipenyo kudhibiti shughuli halali za kisiasa zinazofanywa na wapinzani wako zinaanza kutia doa matumaini makubwa wananchi na jumuiya ya kimataifa waliyoyaweka kwako.
 
Mwigulu nahisi kafanya makusudi kabisa, kamtega mama, ana watu wake wamemtuma aharibu uchumi na sifa za mama, lazima, haiwezekani atoe maneno ya kashfa kwa raia baada ya kuwatia hasira kwa makato ya kuwatia umaskini zaidi wananchi..
 
Mfano mzuri ni tabia ya Mwigulu ambayo ilivumiliwa na marafiki kama akina Kikwete kwa sababu zao za kiharibifu hadi kupewa nafasi kubwa ktk CCM. JPM akamuondoa ktk uwaziri. Sasa ameingia rais ambaye wengi tunaamini anashauriwa. Bahati mbaya wanaomshauri ni wale wale wenye akili ya kiharibifu, Mwigulu kaonekana tena eti anafaa sana kupewa wizara! Naye karudia upuuzi wake kwa kasi zaidi.

Anajivunia Ph.D ambayo hajawahi hata kuonesha kipya kilichomo ndani ya kabrasha lake. Hajawahi kuandika chapisho lolote ili kuonesha kwamba amegundua jipya. Yeye kila leo ni kusema ana Ph.D. na katuonesha njia ya kwenda Burundi kwenye unafuu wa maisha. Inasikitisha kwamba mafanikio ya watu kama akina Nchemba ni matokeo ya udhaifu wa marais wanaokua madarakani.
Nadhani tatizo linaanzia ndani ya chama chake 'Ccm' kulea watu aina yake na kuwaruhusu kugombea uongozi.
 
Mfano mzuri ni tabia ya Mwigulu ambayo ilivumiliwa na marafiki kama akina Kikwete kwa sababu zao za kiharibifu hadi kupewa nafasi kubwa ktk CCM. JPM akamuondoa ktk uwaziri. Sasa ameingia rais ambaye wengi tunaamini anashauriwa. Bahati mbaya wanaomshauri ni wale wale wenye akili ya kiharibifu, Mwigulu kaonekana tena eti anafaa sana kupewa wizara! Naye karudia upuuzi wake kwa kasi zaidi.

Anajivunia Ph.D ambayo hajawahi hata kuonesha kipya kilichomo ndani ya kabrasha lake. Hajawahi kuandika chapisho lolote ili kuonesha kwamba amegundua jipya. Yeye kila leo ni kusema ana Ph.D. na katuonesha njia ya kwenda Burundi kwenye unafuu wa maisha. Inasikitisha kwamba mafanikio ya watu kama akina Nchemba ni matokeo ya udhaifu wa marais wanaokua madarakani.
Yaani ile ni takataka tupu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Leo imetimia miezi minne na siku kadhaa toka Mama SSH, Rais wa JMT alipochukua madaraka yake rasmi katika nafasi hii nyeti ya kuliongoza taifa letu. Nachelea kusema ya kuwa kuna shida sehemu fulani kutoka kwa wasaidizi na washauri wake.

Toka alifofikisha siku 100 za utawale na hatimaye kufanya mahojiano na wahariri wa vyombo vya habari, naona majibu aliyoyatoa kwao yameanza kuleta fukuto na mihemuko mipya ya kisiasa nchini. Kuna misimamo ambayo anaweza kuishikilia yeye binafsi na kuelekeza ifanyike ili kuepuka matumizi ya nguvu ya polisi hapa nchini.

Hoja za kisiasa hupaswa kujibiwa kisiasa na kupitia wanasiasa endapo tu kama zipo kisheria na zinakubalika kikatiba. Kuanza mapema hivi kuruhusu wakuu wa mikoa na wilaya, polisi na hata maafisa vipenyo kudhibiti shughuli halali za kisiasa zinazofanywa na wapinzani wako zinaanza kutia doa matumaini makubwa wananchi na jumuiya ya kimataifa waliyoyaweka kwako.
Lakini tatizo pia ni aina ya wanasiasa tulio nao.
Hebu fikiria kiongozi anamsimamisha kijana toka gerezani, halafu anasema huyu naye NITAMNYOA KWA WEMBE ule niliomnyolea mwenzake,. Unategemea nini?

Hebu waza rais ameachia uhuru wote wa kufanya mikutana na vyombo vya habari, halafu ansema nipeni muda juu ya KATIBA halafu kiongozi hata wiki haijaisha anatokea na kusema ATAKE ASITAKE . Unategemea nini?

Ukiweka kidole kwenye moto utaungua.
Sisi tulio nje na siasa tunangalia na kusema ngoja tuone. Je vijana wetu kwenye siasa WAMEPANDIKIZWA? kwa lengo la ku create chaos?
 
Sehemu kubwa ya watu hawa wanaegemea kwenye urafiki binafsi badakla ya uwezo wao ktk nafasi.
Angalia Mwigulu wa Kikwete alivyokuwa mwamba, akawa mnyonge enzi za Magufuli, sasa tena kawa mwamba.
Angalia Kabudi wa leo na yule wa enzi ya Magufuli.
Angalia Jafo wa leo na yule wa enzi ya Magufuli
Angalia Gwajima wa afya na enzi za Magufuli

Kwa hili la Nchemba hadi atukane wa-TZ hivi, shida iko kwa rais. Yeye anaona kapata jembe la kisiasa, kumbe jembe linadeka.
Lipa kodi wewe Acha porojo za kitoto
 
Back
Top Bottom