hao wenye phd ndio wanatuletea tozo zisizo na kichwa wala miguuLakin pia tukisema wagombea wawe na degree ......bado mtaanza kulalamika kwamba elimu sio kigezo cha kuwa uongozi
Waafrika ....tushazoea kulalamika
Asante sana umeeleza vizuriMatatizo wanayajua vizuri sana tena wengine wamefanyia tafiti ngazi ya master, PhD na katika mashirika ya ndani na nje kama UNICEF,twaweza, UNIDA Universities nk.
Uwezo wa kutatua matatizo unategemea uwezo wa uzalishaji mali.
Uzalishaji wa Africa soko lipo ulaya ambao wazungu wachina,wahindi hupanga bei ya kununua bei wanayoitaka wao kisha kutuuzia vifaa vya kutatua matatizo kwa bei kubwa sana.
Jiulize gari mpya ya halmashauri inanunuliwa shilingi ngapi, je ili ulinunue hilo gari inakubidi uuze tani ngapi za pamba au kahawa au gesi.
Viongizi wa Africa wamezidiwa akili/ujanja na wazungu katika fair/win win bussiness, hivyo wanakosa pesa za kuweza kutatua matatizo sio kwamba hawana akili au uwezo au hawatatambui matatizo bali wazungu ni wajanja kuwazidi.
Jambo lingine ni kuendeleza rushwa ndogo ndogo kwa manufaa yao binafsi na kujali vyama kuliko wananchi.Jambo lolote nje ya chama kinachotawala Africa halipokelewi.
Hata hivyo mimi naona kuna mabadiriko kiasi kwa viongozi wetu kuanza kutatua matatizo sugu japo kasi ni ndogo. Mfano sasa hivi vijiji vingi vina umeme, maji, zahanati mitandao ya simu.
Tukumbuke Africa ina natatizo mengi na sugu,wananchi nao wamelala kwani husubiri mpaka serikali ije itatue matatizo wanayoweza kuyatatua mfano kujenga zahanati, darasa,vyoo ipo katika uwezo wa wananchi ila kuajiri watumishi hawawezi. Hivyo LAWAMA ziende kote kote.
Kaeleweka kimuria kabisa.Asante sana umeeleza vizuri
Changamoto ni kwamba serikali inakusanya kodi nyingi, vitu vinapanda bei sana kiasi kwamba hata wananchi wanakuwa busy kutafuta mahitaji muhimu tu pia wakitaka kufanya project kwa mfano kuna baadhi ya maeneo wananchi huamua kujenga barabara lakini mwisho wa siku serikali hai support wakati inawakamua kodi kila kukicha.Napenda sana mada positivr kama hizi aisee.
Na mimi naomba nichangie kwa kusema kwamba suala la changamoto kutokutatuliwa kunachangiwa na mambo mengi sana na mawili ndio umetaja ila nyuma ya pazia yapo mengi.
Kuna upande wa serikali ama vipngozi kuna mapungufu yao miongoni mwayo umeyataja hayo.
Alafu kuna upande wa wananchi ambako nako hali ni mbaya,hawajaamka na kuchukua majukumu yao kisawasawa,wanashabikia vyama badala ya maendeleo,wanasubiri kila kitu kitoke serikalini n.k
Wananchi wanao wajibu wa kuandaa mipango mbalimbali ya kujinasuua katika matatizo yanayowakumba,wananchi waandae mipango mikakati waandae programs ambazo zinaelezea plan zao juu ya kutatua changamoto za maji,waandae program zenye plan za kutatua changamoto za umeme,sio wanakuja watu wanafanya mambo bila kuwashirikisha wananchi wa eneo husika mwishowe mipango inakuwa sio endelevu kabisa.
Wananchi wanakosa maji je wananchi wameandaa mpango gani kuhakikisha wanaliendea suala hili na kutatua changamoto ?
Wananchi na sisi tunao wajibu pia wa kuhakikisha tunapiga hatua fulani kutatua changamoto kisha serikali inaaendelea na hatua kadhaa kumaliza changamoto hizo.
Mabadiliko yanahitajika kwetu sisi na viongozi,kila mmoja anao wajibu