Udhalilishaji katika Usaili unaofanyika na Sekretarieti ya ajira

Udhalilishaji katika Usaili unaofanyika na Sekretarieti ya ajira

Wanaita watu wengi Sana katika usaili hii nilifanikiwa kuifatilia ni fani ya ICT Officer (System Administrator) wanaitaji nafasi moja lakini wameita watu 752.

Vijana waliohudhuria pale wamezuiliwa kuingia kwenye usaili ni wengi sababu ya kuzuia mfano mwingine alikua anashiriki hizo interview mara kwa mara na vyeti vyake ni hivyo leo amekuja wanamzuia wanadai majina katika cheti yametofautiana sasa hapo awali walikua wanamruhusu vipi na vyeti ni hivyo hivyo, mwingine anazuiwa sababu amekuja na namba ya Nida wao wanahitaji kitambulisho lakini mwafahamu Nida bado hawajatoa vitambulisho kwa wengi hapo wao hawakubali kupokea na kuthibitisha Ile namba ya Nida kwani si iko kwa system lakini wanazuia tu. Mtu amesafiri umbali mrefu kuja Dodoma kumzuia bila sababu ya msingi si kumtendea haki.

Hawa vijana hawatendewi haki sababu hata wanapojaribu kujieleza wanaitiwa askari ili kuwafukuza eneo la tukio.
Huu ni udhalilishaji unafanyika hapo.
Mchakato huu nimefatilia kidogo tu nimegundua hauko sawa.

Vijana hawa kwa hakika wanadhalilishwa tu.
Aisee nakuunga mkono kabisa alafu sikunizi wana katabia mfano unaweza ukawa shortlisted ukifikanpale udom wana kuchomoa wana kwambia hauna sifa ....
 
Yaani unatafuta mtu mmoja mwenye qualification unazotaka kwenye watu 752, haupo serious labda kama huna imani na ubora wa elimu inayotolewa kwenye vyuo wanakotoka.......
Nakubaliana na wewe na pia wangetumia njia nyingine za kufanya shortlisting, wanaweza kuandaa online aptitude test hii inasaidia kupunguza watu. Kuliko kuwaita watu mia 7 kwa nafasi moja, naamini ndani ya watu kumi tu watakuwa wamepata mtu mwenye sifa zote wanazotaka, kwa maana ya qualification, experience, skills, physical appearence na behaviour.
Ni imani yangu kuwa usaili kwa usahihi unaweza kufanyika kwa watu 10 wa mwanzo peke yake.
Wanafuata utakuta panel inechoka na imeanza kuboreka.
 
Unaweza kukuta ni sehemu ya ulaji wanapoita utitiri wa watu......
 
Unawezaje ku shortlist watu 752 kwa nafasi moja ya ajira? hii nchi imejaa majitu ya hovyo sana....
Ungekuwa ni wewe unasimamia kazi hiyo na endapo wote wana sifa ungefanyaje kuwaacha wengine na kuwachukua wengine? Bursara ya hali ya juu ni kuwaita kwa haki na kuwashindanisha.
lakini pia, hao jamaa wana kanzidata na unaweza kufanya usaili huo mmoja ukapangwa kazi sehemu nyingine na hili ushahidi upo mwingi tu.

Tupambane na tusijikite kulaumu
 
Nakubaliana na wewe na pia wangetumia njia nyingine za kufanya shortlisting, wanaweza kuandaa online aptitude test hii inasaidia kupunguza watu. Kuliko kuwaita watu mia 7 kwa nafasi moja, naamini ndani ya watu kumi tu watakuwa wamepata mtu mwenye sifa zote wanazotaka, kwa maana ya qualification, experience, skills, physical appearence na behaviour.
Ni imani yangu kuwa usaili kwa usahihi unaweza kufanyika kwa watu 10 wa mwanzo peke yake.
Wanafuata utakuta panel inechoka na imeanza kuboreka.
Nakubaliana na mawazo yako
 
Ukishaona mtu mlalamishi-mlalamishi, ujue huyo moja kwa moja ha-qualify! wala usihangaike naye!
 
Serikali haitaki lawama kama umeomba na ukafit vigezo mnaitwa hata mfike 1500 na nafasi ni moja ili kutoa lawama kwamba watu wanaajiliwa kwa kujuana mkuu,hizo nafasi wanazotoa kweli lazima mzitafute kwa ushindani na ukipata ni halali yako.

Sasa hivi ile ya kujuana haipo maana shelia zinawabana mkuu.
Sana sana pia wanaosimamia usaili huwa wananuniana maana kila mtu ana mtu wake halafu anatafutwa mmoja
Wangeingiatu utumishi portal wakawapa wanaoona watawafaa kama wanavyofanya kwa baadhi ya kada
 
Ungekuwa ni wewe unasimamia kazi hiyo na endapo wote wana sifa ungefanyaje kuwaacha wengine na kuwachukua wengine? Bursara ya hali ya juu ni kuwaita kwa haki na kuwashindanisha.
lakini pia, hao jamaa wana kanzidata na unaweza kufanya usaili huo mmoja ukapangwa kazi sehemu nyingine na hili ushahidi upo mwingi tu.

Tupambane na tusijikite kulaumu
Hiyo kanzidata wanatumia utaratibu na vigezo gani kuhifadhi jina huko?
Ni alama anazopata katika Oral, au nini?, Na ni alama kuanzia ngapi, na wadau yani watu wanaohusika kuomba na kufanya hizo interview wanajua Kwa namna ipi kuwa ni kweli jina limewekwa kwa kanzidata mana wanaofanya hizo oral hawapewi maelekezo.

Mnatumia miongozo ipi rasmi huko sekretarieti ya ajira?
 
Back
Top Bottom