Udhalilishaji katika Usaili unaofanyika na Sekretarieti ya ajira

Aisee nakuunga mkono kabisa alafu sikunizi wana katabia mfano unaweza ukawa shortlisted ukifikanpale udom wana kuchomoa wana kwambia hauna sifa ....
 
Yaani unatafuta mtu mmoja mwenye qualification unazotaka kwenye watu 752, haupo serious labda kama huna imani na ubora wa elimu inayotolewa kwenye vyuo wanakotoka.......
Nakubaliana na wewe na pia wangetumia njia nyingine za kufanya shortlisting, wanaweza kuandaa online aptitude test hii inasaidia kupunguza watu. Kuliko kuwaita watu mia 7 kwa nafasi moja, naamini ndani ya watu kumi tu watakuwa wamepata mtu mwenye sifa zote wanazotaka, kwa maana ya qualification, experience, skills, physical appearence na behaviour.
Ni imani yangu kuwa usaili kwa usahihi unaweza kufanyika kwa watu 10 wa mwanzo peke yake.
Wanafuata utakuta panel inechoka na imeanza kuboreka.
 
Unaweza kukuta ni sehemu ya ulaji wanapoita utitiri wa watu......
 
Unawezaje ku shortlist watu 752 kwa nafasi moja ya ajira? hii nchi imejaa majitu ya hovyo sana....
Ungekuwa ni wewe unasimamia kazi hiyo na endapo wote wana sifa ungefanyaje kuwaacha wengine na kuwachukua wengine? Bursara ya hali ya juu ni kuwaita kwa haki na kuwashindanisha.
lakini pia, hao jamaa wana kanzidata na unaweza kufanya usaili huo mmoja ukapangwa kazi sehemu nyingine na hili ushahidi upo mwingi tu.

Tupambane na tusijikite kulaumu
 
Nakubaliana na mawazo yako
 
Ukishaona mtu mlalamishi-mlalamishi, ujue huyo moja kwa moja ha-qualify! wala usihangaike naye!
 
Sana sana pia wanaosimamia usaili huwa wananuniana maana kila mtu ana mtu wake halafu anatafutwa mmoja
Wangeingiatu utumishi portal wakawapa wanaoona watawafaa kama wanavyofanya kwa baadhi ya kada
 
Hiyo kanzidata wanatumia utaratibu na vigezo gani kuhifadhi jina huko?
Ni alama anazopata katika Oral, au nini?, Na ni alama kuanzia ngapi, na wadau yani watu wanaohusika kuomba na kufanya hizo interview wanajua Kwa namna ipi kuwa ni kweli jina limewekwa kwa kanzidata mana wanaofanya hizo oral hawapewi maelekezo.

Mnatumia miongozo ipi rasmi huko sekretarieti ya ajira?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…