[/QUOT
Tatizo mbona liko wazi hapa. Nafasi nyingi kati ya hizi ulizozitolea mfano ni za KITAALUMA zaidi. Hapewi mtu kwa sababu ya dini yake, nafasi hizi zinapatikana kutokana na sifa za TAALUMA. Tumieni nguvu nyingi sana kuwapeleka watoto wenu shule ili wapate elimu na kujinasua kwenye ujinga unaoendelea kuitafuna jamii yenu. Angalia mfano huu hapa: Kwa kipindi cha miaka saba nilipokuwa shule ya msingi sikufundishwa na mwalimu yeyote MUISLAM, nakumbuka kwenye eneo lote la kata ile yenye shule za msingi tisa hakukuwa na mwalimu hata mmoja MUISLAM. Nilipokwenda shule ya sekondari ambayo ilikuwa na walimu 47 alikuwepo mwalimu mmoja tu MUISLAM. Kwa bahati nzuri nilifauru mtihani wa kidato cha nne na kuendelea na masomo ya high school katika shule ile ile, tulikuwa wanafunzi 46 wa (PGM) tuliochaguliwa kuingia kidato cha tano, katika darasa letu hakuwemo MUISLAM hata mmoja. Nilipokwenda chuo kikuu nilisoma na wanafunzi wachache sana WAISLAM. Kwa mtiririko huu usitegemee kuwaona WAISLAM kwenye nafasi za kiataaluma. Acheni tabia ya kulalalamika tu, jengeni shule, wapelekeni watoto wenu shule, wahimize watoto wenu wasome kwa bidii na acheni tabia ya kuwajaza fikra za kibaguzi watoto wenu.