Udhalimu kwenye huduma za Afya, watoa huduma wengi Matapeli // Sakata la Mwakinyo

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Nina mada mbili leo acha niziseme tu maana binafsi zinanikwaza sana na kunifanya nione dunia imejaa maadui na watu wabaya.

Tumekuwa na kawaida ya kutoa lawama na kashfa kwa serikali, lakini Watanzania naomba tukumbuke kuwa waliokaa kwenye uwongozi ni sisi hao hao Watanzania

Tamaa ya fedha inatufanya tusiwe na utu hata kidogo,

Chukizo la kwanza:
Binafsi mbali na kazi zangu binafsi, nina ujuzi nimesome, ni Tabibu (Clinician)
Nimepita kwenye vituo vya afya vingi tofauti tofauti vya private, nimegombana na maboss wengi tofauti na sababu kubwa ni kwamba nakuwa sitengenezi mazingira mazuri ya pesa kuingia katika Zahanati,

Iko hivi niseme..

Mgonjwa anapokuja hospital, akionana na mganga akisha ongea matatizo yake anaandikiwa vipi, upigaji unaanzia hapo kwenye vipimo boss anataka kuona vipimo vingi bila kujali condition ya mgonjwa,

Akitoka kupima, Boss anataka aone positive nyingi kusudi mgonjwa apatiwe madawa, wakilenga mauzo yawe juu.

Tunakosa utu watanzania, ukiligeuza jambo hili kwa upande wako nini kinatokea ?? utapenda kufanyiwa jambo kama hili ??

Nina ushuhuda wa kumpiga ngumi Mtu wa maabara kwa ujinga wa tamaa za hela na kunijazia majibu ya uwongo.

Can you imagine
Anakuja dada wa watu ni mjamzito, mimba hata haijafika miezi mitatu, mimi nampokea kwa uaminifu wote, namuandikia vipimo, then mtu wa maabara kwa tamaa ya pesa anaandika kwamba Patient wako kipimo cha Malaria kinaonesha ana Malaria...
Kisa tamaa ya hela, dada wa watu anakwenda kunywa midawa bila kuwa na tatizo, umemkosea mjamzito, umekikosea na kiumbe kilicho tumboni.

Hizi laana Kwa wenye hizi Tabia nasemaje, haziwezi kuwaacha salama.
Na kinachonikela mgonjwa akipewa huduma mbaya lawama atapewa aliyetibu kwa kuandika dawa.
Niishie hapa tu na madaktari wahongo wamejaa kila kona, jamani tuweni Makini.

Mwakinyo:
Niseme jambo kwenye Sakata la Mwakinyo kiukweli mimi nasimama na kumtetea Hassan Mwakinyo ana haki ya kuchagua mtu wa kufanya nae kazi,
Asilazimishwe kufanya kazi na mtu yeyote kisa kaweka pesa zake.

Ubondia ni kipaji chache na ana haki ya kutafuta hela kwa haki na amtakaye bila kulazimishwa.

Tamaa ya fedha wewe boss isikufanye kumlazimisha mfanyakazi akiuke maadili yake kisa wewe unaangalia pesa imeingia.

Maboss Acheni Tamaa Mtapata Laana Mbaya.
 
Attachments

  • az_recorder_20230930_115608_edited.mp4
    15.6 MB
Mwakinyo ana hoja asikilizwe, sema watanzania kwakuwa uelewa ni mdogo hawawezi kuelewa
 
Na ukiongea ukweli sehemu km hizo unaonekana mnoko
Kabisa yani,
Dunia ya sasa usimwamini hata rafik yako kwenye hela, zinagombanisha wengi
 
Back
Top Bottom