Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Acha uchochezi wa kidini wewe! wewe ndo umefilisika kifikra.

Na ukitaka kujua kwa kiwango gani unadanganya watu, hebu pitia picha za wafalme wa Zanzibar kutoka mwanzo mpaka mwisho ndo utagundua kuwa umekuwa brain washed. Ikiwa wafalme wenyewe walikuwa ni mixed race utasemaje waarabu waliwabagua na kuwaua watu weusi?
Huyo hapo chini ni Ali Bin Humud (Mfalme wa Zanzibar 1884-1918) na wengine wengi tu!
 
Mkuu Pascal unaonekana kama unaenda na beat vile!

huu uzi ulianza enzi za tawala tofauti huko nyuma ambapo ulionyesha hisia zako za kweli lakini saivi naona kama unaleta comment za funika kombe mwanaharamu apite 😄. Kuwa na msimamo kamanda au omba radhi kama unadhani uliteleza.
 
Baniani mbaya, kiatu chake dawa!, hata utakapohitaji kutumia dawa ya baniani mbaya, kutumia huko dawa hakumfanyi baniani mbaya kugeuka mwema!.

Kafiri akufaaye sii Islamu asiye kufaa, unapokubali kusaidiwa na kafiri, unakuwa ni umepokea msaada wa kafiri na sio msaada wa kikafiri, hivyo huo msaada ni msaada safi kama ile dawa ya baniani mbaya, na huyo kafiri, anaendelea kuwa kafiri!.

Vivyo hivyo kwa Mwarabu!.

P
 
Hakuna cha baniani mbaya kiongozi. Mnachokifanya watanganyika wengi wenye udini ni kusambaza chuki dhidi ya muarabu kwa watanganyika wengine na wazanzibari wachache. Hii ni mbaya sana na mnajua kwa kufanya hivyo mnagusa hisia za wazanzibari walio wengi ila mnafanya kusudi.

Ukweli utabaki palepale, wazanzibari wamechanganyika sana na waarabu na ikiwa nyinyi mnawachukia waarabu basi mnachosema ni kwamba mnawachukia pia wanzanzibari, hili halipendezi hata kidogo ikiwa kweli wewe ni mzalendo wa utanzania wako. Ikiwa kweli waarabaru waliwatesa wanzanzibari basi waachieni wanzanibar wenyewe waseme, sasa iweje mtanganyika awe ndo mjuzi zaidi ya mateso ya mzanzibari kuliko huyo mzanzibari mwenyewe?

Kwa nafasi yako hupaswi kuwa mchochezi wa hisia za kidini na ukabila. Muungwana akiteleza hukiri na kuomba radhi. Wazanibari ni waungwana pia na naamini watakuridhia.
 
Hapa Mada unazungumzia Udhalimu wa Waarabu walioufanya Unguja na Pemba wakati wanavitawala hivyo visiwa.

Ndio maana Serikali Yao ilipinduliwa mwaka 1964.
Kwanza ujue sio Waarabu wote ni Waislamu wengine ni wapagani.

Wakoloni wote na wavamizi waliwafanyia uhalifu wazawa wakati wanawatawala.
Hapa kinachoongelewa ni huo uhalifu na sio Dini wala mahusiano ya familia.

Waarabu walimfanya Muunguja na Mpemba kuwa Mtumwa kama yalivyofanya Mataifa mengine kwa mwafrika.

Waarabu walimfanyia Muunguja na Mpemba suluba nyingi tu hadi akapinduliwa utawala wake.

Hayo ndio yanayosimuliwa hapa na sio Chuki tu dhidi ya Mwarabu.

Muwe munasoma na kuielewa Mada.
 
Tatizo la mtanganyika na mzanzibar akitokea MTU mmoja akakosoa kuhusu Mambo muhimu ya Taifa letu mfano sakata la loliondo na bandari , basi wengine watasema analeta udini na wengine watasema analeta ukabila . Kwahiyo utafika muda Mchele na pumba havitakaa sehemu moja lazima kila kitu kitakaa sehemu yake. Tanzania sehemu ambayo mataifa mengi hapa Africa wanakuja kuomba ushauri kuhusu Amani , umoja na mshikamano kama haitoshi wanajiuliza tuliwezaje watu wote hapa Tanzania kuzungumza lugha moja nchi ya zaidi ya makabila 125 . Kwahiyo sio kila MTU anayepiga odi kwako ni MTU salama ... Subira, uleta heri . Hakuna cha udini wala ukabila Mambo yakibadilika wote tunakuwa victims ..

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Unachokiongea mkuu huna ujuzi nacho!

Hili suala zima la biashara ya utumwa Zanzibar hujui historia yake, hata hiyo inayofundishwa na wazungu. Unguja na Pemba ilikuwa na wakazi kabla ya kuja muarabu na muarabu hakuja kukamata watu Unguja ili wawafanye watumwa. Watumwa walitolewa kutoka maeneo mengine ya bara na hata nchi jirani. Zanzibar ilikuwa ni soko tu la watumwa.

Unaposema sio kila muarabu ni muislamu ni kweli kabisa ila nitajie muarabu mkristo katika utawala wa waarabu Zanzibar. Unajificha sehemu ambayo ipo wazi kabisa.

Swali la msingi kabisa unapaswa kujiuliza, kwanini wazanzibari hawakuwa watumwa wakati wa biashara ya utumwa? (Hili unaonekana ulikuwa hulijui kabisa). Wakaazi wa Unguja (hasa tumbatu) waliomba msaada kwa waarabu waje kuwasaidia kutokana na uvamazimi na udhalimu wa wareno pale Unguja. Unajua kwa nini walimuomba muarabu na sio mzungu? kwasababu Uislamu ulishaingia Zanzibar kabla ya muarabu kuwa mfalme so waliomba msaada kwa waislamu wenzao kuwatoa wareno na kuwapa ulinzi na ndio maana waarabu na waunguja/wapemba waliishi kama ndugu na mwishowe kuzaliana.

Tatizo lenu wengi mna-generalize kama ulivyoingia Ukristo Africa kupitia Missionaries basi na Uislamu pia mnadhani uliingia kwa biashara ya utumwa.

Uislamu uliingia Africa kupitia Ethiopia hata kabla Mtumwe Muhammad (SAW) hajahama Makka kwenda Madina, wakati huo Ethiopia ikiitwa Abysinia chini ya mfalme Najash (aliyekuwa mkristo wakati huo). Baadae ulisambaa kupitia pwani ya Africa mashariki (ni somo pana hili.)

With all due respect ukiamua kuwa mpingaji kuwa mpingaji kwa rangi zako halisi ila kama unataka kujifunza then kuwa interlectual without biasness.
 
Hivi hujui kuwa Waarabu na Wahindi ni watu wenye roho mbaya? Wabinafsi, Wabaguzi n.k, hujui hilo?
Unawaonea wivu tu kwa mafanikio yao. Mbona Makaburu wametesa na kuua Weusi kule Afrika Kusini toka mwaka 1652 hadi 1992 lakini hatuoni mkileta mada za kuwaponda humu.
 
Nimecheka sana watu wanavyosema Sultan hajawahi kuwatesa wazanzibari.

It seems ukiwasema Waarabu, mada inabadilishwa kuonyesha unaisema dini fulani.

Hapa itakuwa vita tu ya udini maana waafrika akili zetu ndivyo zilivyo.
Ili kushinda hoja zao weka tu ushahidi wa mateso ya Sultan kwa Wazanzibari.
 
Kwahiyo unataka kutuambia Mwarabu alimfanyia mema tu Muunguja na Mpemba kwa muda wote alioishi Zanzibar ?
Hakuna baya lolote alilolifanya Mwarabu kwa Mzanzibari hadi Serikali yake kupinduliwa ?

Hapa tunajadili yale mabaya tu ya Mwarabu kwa Mzanzibari kabla na wakati wa Utawala wa Mwarabu huko Zanzibar.
 
Huu ndio wakati Pascal Mayalla alipokuwa ndio yeye kwa nafsi yake.
Mada hii inatupa picha halisi ya hii mikanganyiko inayoendelea kuhusu DP World na waarabu kwa ujumla pamoja na kwa nini Zanzibar na bandari zao wamejiweka pembeni na hili dubwasha linalotaka kumiliki fukwe zetu milele.
Kwa wageni hebu wapitie andiko hili pia challenge alizoleta muislamu huyu kindakindaki Mohamed Said watapicha fulani kujua sehemu ya undani wa kwa nini Watanganyika tunachuuzwa kwenye hili
 

Dp world waje, muhimu tusiumie, na wao wasiumie......haki itendeke.

Halafu wengi wenu mpo na udini udini na kuingiza ubaguzi usio na maana yoyote kisa tu aliepewa bandari hii ni mwarabu/muislamu.

Karibuni dp world, karibuni waarabu kwa ujumla. Kama nilivyosema hapo mwanzo "Dp world waje, muhimu tusiumie, na wao wasiumie......haki itendeke kwa wote"


Tukemee ubaguzi
 
JF tuna watumwa wa Waarabu waliosalia FaizaFoxy THE BIG SHOW a.k.a The Big Choo.
 
Naunga mkono hoja, hili hata mimi katika bandiko hili, hili nimelizungumzia
P
 
Wanalazimisha tuamini uongo na uzushi wao ili tuamini waarabu ni watu wabaya na wakatili, wanakera sana
Qur'an haijaacha kitu, yote mnayoyafanya dhidi ya waislamu yamo katika Qur'an

﴿وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴾
[ البقرة: 120]

Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.
Unawaonea wivu tu kwa mafanikio yao. Mbona Makaburu wametesa na kuua Weusi kule Afrika Kusini toka mwaka 1652 hadi 1992 lakini hatuoni mkileta mada za kuwaponda humu.
Wivu ni mbaya sana, ongezea na chuki dhidi yao
 
Mimi siamini kama kuna Waarabu wema, dharau ya Mwarabu na Mhindi kwa mu Africa ni mara 10 ya dharau ya Mzungu.
Wangese kabisa binafsi nitangaze wazi mwarabu sehemu yoyote nikimuona Huwa napata hisia za chuki na mikanzukanzu na ile mitambara mingine ptuuu[emoji20][emoji20][emoji20][emoji3082]
 
Uislamu umetajwa wapi bwashee?
 
Kwakuwa utumwa ni jambo lisilo pendeza, binafsi nategemea kuona mtu anapomuongelea muarabu na utumwa asiache kumtaja mzungu. Hii imenifanya niwe curious kujua kwani ni kwa kiasi gani hawa waarabu walikuwa wabaya zaidi katika hili kuwashinda wazungu! (hii haihalalishi matendo yoyote ya dhuluma ya utu wa mtu, regarless nani alikuwa mbaya zaidi ama alikuwa na nafuu). Hamu yangu ni kutaka kujua tu kiundani kwanini mzungu haongelewi katika hili?

Siku hizi kuna chatGPT so i tried to ask the robot this question "How did the treatment of slaves differ from Europeans and Arabs"

Brother Pascal Mayalla hebu pitia pitia kidogo kisha uje kutuambia wazungu walikuwa wema kwa kiwango gani kuwashinda hawa waarabu wala tende.
 
Kaka Pascal Mayalla njoo usome uzi wako tena. Na unasema DPW waje ti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…