Udhamini wa Bima kwa wachezaji NBC Premier League

Udhamini wa Bima kwa wachezaji NBC Premier League

Makonyeza

Member
Joined
Feb 2, 2020
Posts
72
Reaction score
261
Naaaam, sasa hii ndio maana halisi ya Udhamini
Maana halisi ya usimamizi wa Soka letu
Maana halisi ya kujali vipaji vya vijana wetu.

Kuna wazee wengi nilishuhudia hasa nikiwa Zanzibar ambako binafsi ninaamini ndiko kilipo kisima cha vipaji vya hali ya juu vya soka, mzee mmoja alimzuia kijana wake mwenye kipaji kikubwa sana kucheza Mpira kwa kuhofia kuumia uwanjani na kupoteza future yake.

Mzee alikuwa mkali sana kiasi cha kumuwekea watu kufuatilia kijana ili mradi kuhakikisha hainui mguu wake na kuuhatarisha uwanjani.
Ninaamini kama Udhamini huu wa kipekee ungekuwepo kipindi kile, kipaji cha bwana mdogo yule (namkumbuka tulikuwa tikimuita Owen) kisingepotea.

Hongera sana TFF

Hongera saaana Rais Maria.

Hongera na shukrani sana NBC, walau mmeleta kiungo kizuri kitakachonogesha Soka letu [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]

FB_IMG_1648540913332.jpg
 
Gharama za matibabu kwa mchezaji akiwa klabuni huwa ni za timu yake, sasa sijajua hiyo bima inatolewa kwa mchezaji pekee au mpaka wategemezi wake?.
 
Gharama za matibabu kwa mchezaji akiwa klabuni huwa ni za timu yake, sasa sijajua hiyo bima inatolewa kwa mchezaji pekee au mpaka wategemezi wake?.
Ni pamoja na mke na watoto wawili. Binafsi nimefurahishwa pia na udhamini wa aina hii.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ni pamoja na mke na watoto wawili. Binafsi nimefurahishwa pia na udhamini wa aina hii.
Imekaa vizuri, lakini wangeongeza wigo wa nafasi japo 2 za wazazi/walezi hakika ingefaa sana.
 
Gharama za matibabu kwa mchezaji akiwa klabuni huwa ni za timu yake, sasa sijajua hiyo bima inatolewa kwa mchezaji pekee au mpaka wategemezi wake?.
Timu nyingi hazina msuli huo wa kutibia mchezaji ...hasa majeraha/maradhi ya muda mrefu.
 
Back
Top Bottom