UDHAURI-Mama mgonjwa Lakini VIPIMO VIANONYESHAHANA TATIZO!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Mama yangu mzazi (70) anasumbuliwa sana na maumivu ya mgongo,miguu kuwaka moto na kuvimba ,mkono upande wa kushoto ,pamoja na kusumbuliwa na shinikizo la juu la damu(si muda waote) Jana tumeenda REGENCY na ampimwa vipimo kadhaa kama damu,mkojo,moyo na x ray .Leo daktari katupa majibu kuwa mama hana tatizo lolote! Moyo uko sawa,figo ok nk.
Pamoja na ukweli kuwa ukiambiwa huna tatizo ni jambo la heri lakini kama una maumivu yanayokusumbua ni jambo lingine tofauti !Kimsingi imemshangaza hadi akasema kwa utani kuwa sasa mnirudishe kijijini ...! au mnipeleke kwa BABU!
Naomba ushauri kwenu najua mengine ni saikolojia kwani alimpoteza mwenza wake wa miaka hamsini + miaka miwili nyuma!
 
Hapo ni ushauri kidole kimedunda!
 

Ndugu, pole sana.
Tafuta uponyaji wa MUNGU
Mpeleke akaombewe na watumishi wa MUNGU.
Jenga imani katika maombi hayo, na atapona.

MUNGU akutangulie
 
Pole sana Madamu kama kapimwa hana maradhi basi atakuwa ana maradhi ya kiswahili mambo ya uchawi na mashetani nitafute kwa njia hii hapa bonyeza hapa.Mawasiliano
 
Ushauri mwingine niwakishirikina na ugombanishaji. Bibi mwenye umri huo alogwe ili iweje?
Mmesahau ya kwamba umri umeenda anaundergo retardation na misuli imechoka kucirculate damu.
Hakikisha unampeleka kwenye vipimo vya kisasa zaidi huko pia atapata dawa za tiba mbadala kusawazisha mwili wake.
 
•Mkuu bila shaka wewe ni Mkenya; kiswahili sanifu ni USHAURI si UDHAURI
 
Pia kama kuna mwangalizi mzuri jaribu kumchua mwili mzima kila siku asbuhi na jioni kwa mchanganyiko wa asali tangawizi na mizizi ya tulatula(unga wa magome yake) fanya hivyo kwa wiki mbili.
Kuhusu shinikizo la damu mpatie atleast punje tatu za vitunguu saumu kila siku.
Usisahau kuleta mrejesho hapa.
CC @KYLOSANGI
 
6¦1Mkuu bila shaka wewe ni Mkenya; kiswahili sanifu ni USHAURI si UDHAURI

Ndugu angalia keyboard zote za simu, Ipad, Computer, typewriter ets zinafanana mtaalamu kama mimi wa keyboard nikiona mtu kaandika D badala ya S sishangau sababu zinakaribiana kifupi maina key ni asdf na jkl; so sio ukenya hapa tunaita typing error na hapo juu nimekuonyesha u na i zipo karibu mtu huweza kosea nimeandika sishangau badala sishangai
 
Tumsaidie huyu mwenye tatizo jamani,tuache kufundishana namna ya kufunga tai.
Jaribu pia mazoezi mepesi mfano kutembea eneo la nyumbani pia mtengenezee juisi ya {asali+limao+kitunguu saumu} 3X5/7. (kijiko cha chai).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…