Mama yangu mzazi (70) anasumbuliwa sana na maumivu ya mgongo,miguu kuwaka moto na kuvimba ,mkono upande wa kushoto ,pamoja na kusumbuliwa na shinikizo la juu la damu(si muda waote) Jana tumeenda REGENCY na ampimwa vipimo kadhaa kama damu,mkojo,moyo na x ray .Leo daktari katupa majibu kuwa mama hana tatizo lolote! Moyo uko sawa,figo ok nk.
Pamoja na ukweli kuwa ukiambiwa huna tatizo ni jambo la heri lakini kama una maumivu yanayokusumbua ni jambo lingine tofauti !Kimsingi imemshangaza hadi akasema kwa utani kuwa sasa mnirudishe kijijini ...! au mnipeleke kwa BABU!
Naomba ushauri kwenu najua mengine ni saikolojia kwani alimpoteza mwenza wake wa miaka hamsini + miaka miwili nyuma!