SoC04 Udhibiti na kuimarisha utawala bora, mifumo ya kiserikali kulinda rasilimali na maslahi ya taifa

SoC04 Udhibiti na kuimarisha utawala bora, mifumo ya kiserikali kulinda rasilimali na maslahi ya taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Bahir

New Member
Joined
Jun 5, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Imewahi kunukuliwa kwa viongozi waliopita wa Taifa letu na kitu ambacho ni ukweli ya kwamba nchi yetu ni tajiri, Na utajiri wetu unajidhihirisha katika rasilimali zetu za asili kwa maana ya madini, mbuga za wanyama (utalii), maziwa, mito na bahari, ardhi na watu. Kwa maana nyingine tuna kila tunachokihitaji ili kujitegemea katika kulijenga Taifa letu kiuchumi, teknolojia na uzalishaji kwa maana ya viwanda

Watu imara wanakuja na kuondoka
kama Taifa lenye kiu ya kujikomboa katika umasikini na utegemezi tunapaswa kuchagua ama kutengeneza mifumo imara ili kufikia utawala bora ambao ndio chachu ya maendeleo ya Taifa lolote ili pindi ambapo watu imara wamepita basi mifumo madhubuti ipo kwaajil ya kumsaidia kiongozi yeyote kulifikisha Taifa mahali ambapo sote tuna nia ya kufika.

Tuangazie maana ya utawala bora kama ilivyotafsiriwa katika Wikipedia

*Utawala bora ni mchakato wa kupima jinsi taasisi za umma zinavyoendesha shughuli za umma na kudhibiti rasilmali za umma na kuhakikisha utekelezwaji wa haki za binadamu katika njia ambayo kimsingi haina matumizi mabaya na ufisadi na kwa kuzingatia sheria. Utawala ni "mchakato wa kufanya maamuzi na mchakato ambao maamuzi hutekelezwa (au kutotekelezwa)".[1] Utawala katika muktadha huu unaweza kutumika kwa utawala wa shirika, kimataifa, kitaifa au wa ndani[1] pamoja na mwingiliano kati ya sekta nyingine za jamii.

Dhana ya "utawala bora" kwa hivyo inaibuka kama kielelezo cha kulinganisha uchumi usio na ufanisi au mashirika ya kisiasa yenye uchumi na vyombo vya kisiasa vinavyofaa.

[2] Dhana hiyo inazingatia wajibu wa serikali na mashirika tawala kukidhi mahitaji ya watu wengi tofauti na makundi yaliyochaguliwa katikajamii. Kwa sababu nchi ambazo mara nyingi hufafanuliwa kuwa "mafanikio zaidi" ni mataifa ya huria ya kidemokrasia, yaliyojikita zaidi Ulaya na Amerika, viwango vya utawala bora mara nyingi hupima taasisi nyingine za serikali dhidi ya mataifa haya.[2] Mashirika ya misaada na mamlaka ya nchi zilizo endelea mara nyingi yatazingatia maana ya "utawala bora" kwa seti ya mahitaji ambayo yanapatana na ajenda ya shirika, kufanya "utawala bora" kumaanisha mambo mengi tofauti katika miktadha mingi tofauti.

-Ufafanuzi huo umejitosheleza kutuangazia ni vipi tunaweza kujielekeza na kujizatiti kufikia mafanikio makubwa na pengine kuwa Taifa lililoendelea na lenye demokrasia huria, Bila shaka huwezi kizungumzia utawala bora bila kuangazia udhibiti wa vitendo vya rushwa.

Hapa nchini kwetu unapozungumzia utawala bora kuna vyombo viwili hutoacha kuvitaja navyo ni Usalama wa Taifa ambao wamejikita kwenye intelijensia na TAKUKURU ambao wamejikita kwenye suala zima la uchunguzi wa makosa ya rushwa.

Tunapozungumzia utawala bora kwa muktadha wa tafsiri ilivyo hapo juu ni lazima tuyaguse maisha ya wananchi katika utoaji huduma bora kwenye nyanja zote, iwe elimu, afya, miundombinu, ulinzi na usalama lakini pia ukusanyaji wa mapato na mgawanyo wa mapato na matumizi yatokanayo na rasilimali zetu.
Haitokuwepo maana ya kukopa mikopo nje kutoka nchi wahisani au kujikusanyia mapato ya ndani ikiwa hatuna udhibiti na usimamizi wa mapato yetu ili kuzuia upotevu wa mapato, vinginevyo watu wachache watajinufaisha kwa mapato hayo na kupelekea mzigo mzito kwa mlipa Kodi ambaye ni mwananchi wa kawaida hivyo kudhoofisha jitihada za wananchi kushiriki kikamilifu katika kujikomboa kutoka kwenye umasikini na kulijenga Taifa.

Kwa mtazamo huu; Kama Taifa tutajizatiti kudhibiti kile tulicho nacho basi ni dhahiri tunaweza kuondokana na utegemezi lakini kama hatuna utayari wa kusimamia rasilimali zetu basi hatutaweza kujitosheleza hata tuwe na Pato kubwa kiasi gani la Taifa kama hatujaweza kusimamia vyema hatutaweza kuathiri maisha ya mwananchi mmoja mmoja kwa namna chanya

Hivyo basi katika kufikia uhuru wa kiuchumi na kuboresha maisha ya mwananchi mmoja mmoja ni vema kuboresha taasisi hizi mbili ili ziweze kutoa matokeo ambayo yataakisi utawala bora kwa mujibu wa Sheria, Lakini pia sheria zetu ziboreshwe ili kuvipa vyombo hivi nguvu stahiki kwani vyombo hivi kwa muda sasa vinatazamwa kama viongozi kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwahiyo kushindwa kwao kutoa matokeo yanayotarajiwa kunadhoofisha jitihada za vyombo vingine vya ulinzi na usalama lakini pia idara nyingine za kiserikali na sekta binafsi na kufanya serikali kuwa na mzigo mzito kujiendesha.

Badala ya kuwa na utitiri wa vyombo vingi vya law enforcement tuviboreshe tulivyonavyo ili vitupe matokeo tunayotarajia , mfano wa maboresho ambayo yangeweza kutoa matokeo ni pamoja na makosa ya utakatishaji fedha na ugaidi , haya yakiongezwa kwenye majukumu ya TAKUKURU yataboresha ufanisi wake, ugaidi ni kampeni zisizo rasmi za kushinikiza kutaka kuwajibisha serikali kwa njia isiyo rasmi kwa maana ya kuchagua kutumia madhara na mara nyingi jambo hili hutegemea ufadhili ambao ukitazama undani wake kuna viini vya rushwa lakini pia uwepo wa cartels kama ile ya sukari ni tishio kwa uchumi wa nchi na usalama wa Taifa linalotaka kujikomboa kiuchumi.

Kama eneo hili litaangaziwa kwa upana litachagiza Ari ya wananchi kuchangia Pato la Taifa kwa kuwa na usawa katika uzalishaji na masoko na kupelekea kuwa na uchumi imara usiotegemea mikopo ama misaada kutoka kwa mabepari ama nchi wahisani yenye masharti yanayoleta ukakasi.

Lugha ya mawasiliano serikalini iwe kiswahili katiba na Sheria zetu ziandikwe kwa kiswahili mipango/mikakati ya utekelezaji wa kujikomboa haziwezi kuwa habari njema kwa mataifa ambayo hayana nia njema na ukuaji wa taifa letu, hasa mataifa yenye nia ya kuendelea kututawala, hatupaswi kujisifu kwa mikakati bora ya kujikomboa maana kwa kufanya hivyo ni kuwataarifu maadui mbinu za kufanya ili kutudhoofisha

Utawala bora ni ule unaojiendesha kwa kuzingatia Sheria na uwazi na kwa kusema hivyo namaanisha ushirikishwaji wa wananchi katika mambo muhimu yahusuyo maendeleo katika nchi yao wenyewe, tunao mhimili wa bunge ambao lengo ni kupata uwakilishi wa wananchi katika kuishauri na kusimamia serikali yao, kitendo cha kumteuwa mheshimiwa mbunge kuwa waziri tafsiri yake ni kumfanya kuwa msemaji wa serikali katika sekta husika ambayo alipaswa kuwa mwangalizi kwa niaba ya wananchi, yaani kwa wakati mmoja anawezaje kuwa msemaji wa serikali na msemaji wa wananchi lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi, huko ni kuwanyima sauti na nguvu wananchi kuishauri na kusimamia serikali yao, napendekeza sifa za kuwapata mawaziri zibadilishwe ili kutoa nafasi ya wabunge kutimiza wajibu wao wa msingi kofia moja kwa mtu mmoja itasaidia.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom