Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Jamii nyingi zilizoendelea Duniani huwa na aina Fulani ya demokrasia. Na jamii nyingi maskini Duniani hujawa na mfumo wa kidikteta.
Mifumo ya kidikteta huzaa viongozi walafi, katili na wasiowekeza kwenye jamii zao zaidi ya kuwekeza kwenye familia zao.
Marekani kwa sasa wana kiongozi dikteta kwenye mfumo wa kidemokrasia. Hivyo ingawa ni dikteta lakini mfumo wa kidemokrasia wa Marekani unawapa fursa wamarekani kupambana na udikteta wake.
Ogopa sana uwe kwenye mfumo wa kidikteta chini ya dikteta kwenye jamii ya watu waliokata tamaa na waliofunzwa kuwa kiongozi ni sawa na Mungu hivyo huwa hakosei.
NI HATARI KUWA SAHIHI WAKATI SERIKALI YA KIDKTETA INAPOKOSEA.
Kumbe 90% ya watanzania hawana ufahamu!!Hauwezi ukasema hawa watanzania wa Leo ambao 90% hawana ufahamu mzuri ambao wanacheza kila mdundo ndo wachague kiongozi .
Mfumo sahihi ni Kama marekaniKumbe 90% ya watanzania hawana ufahamu!!
Sasa mbona mnasheherekea watu wenu kuchaguliwa kama mnajua wachaguaji hawana uwezo wa kuchangua?
Tufanye tunakubaliana kuwa huu mfumo hautufai. Sasa mfumo upi ndiyo unaotufaa?
Marekani "direct vote" zipo. Huo mfumo wa watu wachache kuchagua kiongozi Marekani uliwahi kufanyika lini na wapi?Mfumo sahihi ni Kama marekani
Watu wachache mnakaa mnachagua kiongozi kwa niaba ya watu wengi