Udikteta wa Akili Ndogo: Taifa Linalosherehekea Upumbavu na Kusaliti Mwelekeo wa Ukombozi wa Kifkra

Udikteta wa Akili Ndogo: Taifa Linalosherehekea Upumbavu na Kusaliti Mwelekeo wa Ukombozi wa Kifkra

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Ni jambo la kusikitisha mno na linalotia hasira kwamba katika karne ya 21, bado tunashuhudia watu wanaojiona wasomi wakishabikia mfumo wa utawala wa kijinga, wa kisultani, wa kibeberu uliovaa joho la kidemokrasia lakini ndani yake ukificha kiini cha udhalimu, uonevu, upumbavu na utekaji wa haki za kikatiba. Kuna baadhi ya watu hapa nchini na kwenye majukwaa ya kijamii kama Jamii Forums ambao aidha kwa ujinga wa kupindukia au kwa utumwa wa kiakili uliokithiri wameamua kuwa wasemaji wa watawala, si kwa hoja bali kwa kupiga magoti kwa mabavu ya propaganda zisizo na msingi wala dira.

Mtu mzima, mwenye akili timamu, mwenye chembe ya uelewa wa kikatiba, hawezi kusherehekea mfumo unaoua watu kwa njaa, unaowafanya vijana kuwa intellectual refugees kwenye nchi yao wenyewe, unaogeuza bunge kuwa uwanja wa maigizo badala ya kuwa taasisi madhubuti ya uwakilishi, usimamizi na utungaji wa sheria kwa maslahi ya wananchi. Bunge limetekwa! Leo ukimuondoa Mpina kwa sababu ya ukakamavu wa kukemea ovyoovyo na Gwajima kwa sababu ya matamshi ya kiroho yenye hisia kuliko hoja, nani mwenye akili timamu aliyebaki kule? Ni watu ambao wakifungua mdomo unashindwa kutofautisha kama ni wabunge wa taifa au class monitors wa darasa la sita waliotumwa na mwalimu kuandika majina ya wasiofanya kazi.

Mnatetea nini? Serikali inayochukua fedha za walipa kodi na kuzitumbukiza kwenye miradi ya kifisadi? Serikali inayoweka vipaumbele vya kifahari wakati wananchi wake wanazama kwenye bahari ya umaskini uliokithiri? Serikali ambayo vyombo vyake vya usalama vimegeuka kuwa zana za kuwanyamazisha wanaosema ukweli badala ya kulinda raia na mali zao? Serikali ambayo imelemaa kifikra kiasi kwamba inadhani kuwa ukosoaji ni uhaini na ushauri ni uasi? Huu si utawala wa kikatiba bali ni mfumo wa psychological enslavement—unaofinyanga fikra za watu kuwa passive recipients of state oppression badala ya kuwa active participants wa mabadiliko ya kijamii.

Na kwa wale wanaojitia kujibu hoja kwa kejeli au mzaha, ni wazi kuwa aidha mnateseka na cognitive dissonance au mnafungwa na utumwa wa kutotaka kuona ukweli unaowachoma. Hoja zangu hazihitaji baraka zenu. Na kama unajitambua kuwa IQ yako iko chini ya room temperature, tafadhali heshimu nafasi yako kwa kunyamaza. Tupo kwenye vita ya kimfumo—vita ya utambuzi dhidi ya ujinga, vita ya maarifa dhidi ya ujinga wa kusifiwa kama kigezo cha uhai wa kisiasa. Taifa haliwezi kujengwa kwa mashangilio ya kipumbavu yanayotolewa na watu wasio na maono, waliojaa woga wa kupoteza nafasi walizopewa kwa upendeleo na si kwa weledi.

Utawala huu hautadumu kwa sifa bali kwa haki. Na kwa kuwa hauna haki, unaendeleza uongo, unaendeleza vitisho, unaendeleza unafiki wa kihistoria. Lakini kumbukeni: historia huwaandikia wapumbavu ukurasa wa aibu, na huwasahau watu wa busara kwa kuwa walinyamaza mbele ya uovu. Utawala huu utawatafuna ninyi mnaoushangilia kama miungu wa kisiasa, na mkumbuke maneno haya: You will regret it, not in whispers, but in screams.
 
IMG-20241007-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom