Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 55
- Thread starter
- #41
Tatizo la wizi kazini lina mizizi yake: Nitaorodhesha baadhi kama ifuatavyo
1. Mtu ana utaalamu mzuri sana, na yeye anajua hilo halafu unamlipa mshahara wa laki moja wakati foreigner mbumbumbu anachukua dola 4,000.
2. Kutokuwa na job security kwa wafanyakazi wengi, yaani siku boss akilala na pombe kichwani unasikia anakupa pay-off kazi hakuna, je mtu afanyeje?
3. Gap kati matajiri na masikini limekuwa sana kiasi kwamba kila mtu anahitajia afikie matawi ya juu mapema kabla ya jua halijachwa.
4. Vijana wanaona mfano wa wazee wengi waliolitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa na uaminifu ambao wengi baada ya kustaafu wanaishia kuwa omba omba ambao watu huwacheka kwa nafasi walizokuwa nazo kutozitumia kwa kuwekeza kwenye maisha ya baadae (Lack of comprehensive social security programs)
5. Viongozi wetu nao ni sehemu ya sisi kutokuwa waaminifu, kwani wao wana-collude na wawekezaji na kuwashawishi wawalipe vijana mshahara wa chini kutokana na maisha kuwa chini tofauti na nchi watokazo wawekezaji. Pia viongozi hao hao hujilimbizia mali mpaka inakuwa siyo siri tena, ambazo ni mali za umma bila kuwajibishwa. Je vijana wafanyeje?
6. Wawekezaji wengi na hasa wahindi ni wanyanyasaji wakubwa wa watanzania wanaofanya kazi kwenye makampuni yao, na kuwafanya watu hao kutokuwa na imani na biashara hizo na kuona ni kama vile haziwahusu kwani hawaaminiki, japo wengine ni waaminifu. Dawa ya mtu asiyekuamini muibie, maana usipofanya hivyo siku akipoteza kwa uzembe wake atasema umemuibia na itakuuma sana, ila kama ni kweli utakuwa na ahueni kuwa kweli nimeiba.
My take: Ni kweli kabisa kuwa uaminifu kazini ni jambo muhimu sana katika kutengeneza mazingira mazuri ya kujipatia mkate wa kila siku. Lakini pia na viongozi wetu kama kina Kapuya wawe mstari wambele katika kujitakasa na wizi wa mali za umma. Viongozi wakiwa waaminifu wataweza misingi mizuri ya social security na kufanya vijana kutokuwa na wasi katika maisha yao baada ya kulitumikia taifa. Vinginevyo "Cat and mouse" game katika sehemu za kazi haitaisha
Mkuu,
Kwa mtazamo wangu we can not compromise maadili kwa maovu. Leo hii kuna untold stories nyingi zikiwemo kupotea kwa sadaka katika makanisa na misikiti yetu, kupotea au kutowafikia misaada watoto yatima. Kwahiyo basi tatizo hili ni la kijamii hasa lipo katika jamii yote ya kitanzania kuanzia katika ngazi ya familia hadi kitaifa. Ni vema tukaangalia ni approach gani itafaa katika kuinusuru jamii ya kitanzania kutoka katika tatizo hili.
Wizi umetanda kila mahali kuanzia majumbani mwetu / katika familia zetu, kwenye mashule na taasisi mbalimbali za elimu, ofisi za serikali na mashirika ya umma, mashirika ya binafsi na yale kigeni, taasisi za kidini, vyama vya siasa, nk. Na wizi huu haufanywi na watu wa tabaka moja bali ni wafanyakazi wa matabaka yote yaani kuanzia juu hadi mtu wa chini kabisa.
Iko haja ya kujadili ukweli na kutoka katika tope hili baya.