UDOM, Korea Kusini na UNICEF waimarisha ufundishaji wa Sayansi Tanzania kupitia mafunzo ya kisasa ya STEM

UDOM, Korea Kusini na UNICEF waimarisha ufundishaji wa Sayansi Tanzania kupitia mafunzo ya kisasa ya STEM

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kikiwa na ufadhili wa Serikali ya Korea ya Kusini kupitia KOICA na uratibu wa UNICEF, kimetoa mafunzo maalum ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kwa walimu wa shule za sekondari kutoka mikoa ya Dodoma na Simiyu.

6695a7ce-e588-47e6-9b38-fce4ec3074ad.jpeg


Mafunzo hayo ya siku saba yalilenga kuimarisha mbinu za ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na mbinu shirikishi zinazochochea ubunifu na kuongeza uelewa wa wanafunzi darasani.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Shule ya Sekondari St. Pio, Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa, kuanzia Machi 26 hadi Aprili 1, 2026.

d495f52e-2aa2-48ed-b8a0-71f7006f0742.jpeg


Akifunga mafunzo hayo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Mwl. Kiduma Mageni, aliwataka walimu kuyatumia maarifa waliyopata kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na matumizi ya TEHAMA darasani, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa chachu ya ubora hata kwa walimu wa masomo mengine.

Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo kutoka UDOM, Dkt. Rose Matete, aliwapongeza wawezeshaji na washiriki kwa ushirikiano wao, akibainisha kuwa mafunzo hayo ni jukwaa muhimu la kuboresha mbinu za ufundishaji na kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika masomo ya sayansi.

Baadhi ya walimu walioshiriki walisema mafunzo hayo yamewapa mbinu za kisasa na za vitendo zitakazosaidia kuongeza ushiriki wa wanafunzi darasani na kuboresha matokeo ya kitaaluma.

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za pamoja za serikali na wadau wa maendeleo katika kuimarisha elimu ya STEM nchini, kwa lengo la kukuza kizazi chenye ujuzi wa kisasa na kinachoweza kushindana kimataifa.

7bf3a205-c784-42b7-becf-1ee06d1a784a.jpeg
 
Back
Top Bottom