UDOM kuna hatari ya waalimu kugomea mitihani, UTAWALA unafanya nini!

Joined
Feb 9, 2012
Posts
65
Reaction score
15
Kuna fununu kwamba waalimu wa COLLEGE YA HUMANITIES AND SOCIAL SCIENCES wamepanga kugomea kusimamia mitihani yetu tunayoanza kesho kutokana na malimbikizo ya miaka mingi ya malipo yao yanayohusiana na usimamizi wa mitihani na mengineyo.

Hivi UDOM kuna nini kila siku sisi tu?? Wiki iliyopita wanafunzi tulizuiwa na Utawala kufanya mitihani kisa hatujalipa ada mpaka waziri mkuu alipotoa tamko Bungeni.

Wiki hii waalimu nao, Hivi sisi wanafunzi tumekosa nini??
 
kuchagua chuo cha kata na kuiamini ii serikali dhaifu ndo kosa lenu
 
Wewe unaesoma chuo cha tarafa unafaida gani kwa jamii na taifa hadi sasa? Kutwa kujisifia chuo ukimaanisha wewe umesoma chuo gani bora hapa nchini ambacho hakina changamoto? Kama Udsm ndicho kimezalisha wasomi feki hadi sasa wanasumbua taifa, wanaitwa mizigo na Kinana kila siku! Sasa faida ni nini kuwa na chuo kinacho zalisha wasomi wasiojielewa! Ungekuwa na busara na elimu bora na si bora elimu unayolingia unge changia mchango wenye mashiko kuwashauri wadogo zetu wa Udom wafanye nini ili wapewe haki yao, pia wahadhiri wafanyeje katika kipindi hiki cha mitihani,wewe unaleta mashindano ya vyuo! Mambo ya kishamba kabisa, tena bora urudi kijijini ukalime mihogo hufai kuitwa msomi wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…