UDOM kushirikiana na madaktari bingwa nchini kutafuta suluhu ya magonjwa ya ndani

UDOM kushirikiana na madaktari bingwa nchini kutafuta suluhu ya magonjwa ya ndani

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
WhatsApp Image 2026-05-29 at 22.33.00.jpeg


Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Hospitali yake imeshiriki katika Kongamano la Mwaka lililoandaliwa na Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Tanzania (APHYTA), lililofanyika leo tarehe 29 Mei 2026 katika ukumbi wa Dodoma City Hotel jijini Dodoma.

Lengo la kongamano hilo ni kujikita zaidi katika kuzuia magonjwa na kuhamasisha kinga ili kupunguza ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayotokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Akizungumza katika kongamano hilo, Dkt. Alfred Miremo ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi, Daktari Bingwa wa Figo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya UDOM, amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kama taasisi ya elimu na tafiti kina wajibu wa kushirikiana na wataalamu wa afya kutafuta suluhu ya changamoto za kiafya zinazoikabili jamii.

WhatsApp Image 2026-05-29 at 22.33.01.jpeg


Amesema mkakati mkubwa utaelekezwa zaidi katika utoaji wa elimu kwa jamii, hususani kwa vijana, ili kuwahamasisha kubadili mitindo hatarishi ya maisha ikiwemo matumizi ya pombe kupita kiasi, kutofanya mazoezi pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya vyakula vinavyochangia magonjwa ya ndani.

Katika kongamano hilo, UDOM kwa kushirikiana na wataalamu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma wametoa huduma za upimaji na utambuzi wa magonjwa mbalimbali bila malipo kwa washiriki wote wa mkutano huo.

Aidha, Chuo kimetumia fursa hiyo kuunga mkono kampeni ya kuwahamasisha Watanzania kujua viwango vya afya zao ikiwemo sukari, shinikizo la damu, uzito na urefu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhimiza wananchi kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.

WhatsApp Image 2026-05-29 at 22.33.00 (2).jpeg


Sambamba na hilo, gari la wagonjwa la UDOM lilikuwa sehemu ya huduma za dharura kuhakikisha usalama wa washiriki wote wa kongamano hilo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Tanzania, Dkt. Kajiru Kilonzo, amewataka madaktari kuweka mkazo zaidi katika kinga na elimu kwa jamii badala ya kusubiri kutoa matibabu pekee.

UDOM ni miongoni mwa vyuo vinavyoendelea kutoa mafunzo ya udaktari bingwa nchini kupitia programu zake za Shahada za Uzamili chini ya Shule ya Tiba na Afya ya Kinywa (SoNPH).

WhatsApp Image 2026-05-29 at 22.33.00 (1).jpeg
 
Back
Top Bottom