UDOM kutowapatia vyeti wanafunzi wa sayansi walio maliza chuo mwaka jana 2012

Zestach

Member
Joined
Sep 3, 2011
Posts
17
Reaction score
5
Kuna taarifa zilizonisikitisha kidogo hivyo naomba kwa mwenye maelezo zaidi anielimishe.Wanafunzi wa shahada za sayansi waliosoma UDOM na kuhitimu mwaka jana wanapata shida wanapohitaji vyeti vyao,hii imetokea baada ya kuambiwa wanatakiwa kulipa kiasi cha shillingi milioni moja.Kwa maelezo niliyoyapata toka kwa mmoja wa wanafunzi hao anadai kuwa wao walidhaminiwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu(HESLB) na chuo kikatuma taarifa za madai ya ada kwa mwaka wa pili na watatu kama shillingi laki saba kila mwaka.HESLB wakalipa fedha hizo kama chuo kilivyo elekeza,baadae chuo wakawaambia bodi kuwa walikosea ada sahihi ilikuwa sh.milioni moja na laki mbili kwa mwaka,HESLB wakakana madai hayo na wanafunzi wakaendelea na masomo bila kusumbuliwa.Sasa imefika wakati huu ambapo wahitimu hao wanahitaji vyeti vyao,chakushangaza eti wanaambiwa wanatakiwa kulipa hiyo sh.millioni moja,vinginevyo hawapewi vyeti hivyo.Je unashauri nini kifanyike kuwasaidia wahitimu hawa maana kwa mtazamo wangu nadhani wao chuo wanatakiwa kumalizana na HESLB.Miliioni moja kwa Mtanzania wa kawaida si kiasi cha kukipata kilahisi,maana mfanyakazi wa serikari tuu wa daraja la TGS D ambalo ndo wahitimu wa vyuo wanaanzia anahitaji miezi mitatu ili aweze kupata hicho kiasi.
 
udom rabish university kabisa,ukubwa nauzuri wamajengo tu lkn utendaji kazi,taaluma,uwajibikaji wawatendaji hakuna kitu.majitu yapo tu ofisini legelege sana!poleni!
 
hiyo bachelor of science ipo kichwani au kwenye cheti?? nenda kaombe kazi waambie ukweli mtupu kuwa hujapewa cheti ila elimu ipo kichwani na uionyeshe kwa vitendo!
 
tatzo watz tunapimana kwa makaratas yan m2 ujuz anao kisa hana chet ndo haiwez kaz...cjui lin tutaelimika
 
shahada ya sayansi gani?
Mbona taarifa yako haijakamilika?
Mi nina jamaa zangu wamesoma shahada ya sayansi ya comp na mwingine ya biology mbona wote wameshapata vyeti vyao?
 
Tujifunze kuandika kitu kilichokamilika sio unapata taarifa kwenye kibanda cha gongo unakuja hapa unazani na sisi tunakunywa gongo,nyie ndo munaotoa taarifa za kupotosha umma kwa ujinga wako wa kushindwa kufikiri,kama umepata taaharifa hizo ingia kwenye tovuti yao uchukue mawasiliano yao uhulize ili kupata taharifa kamili. Na ujue ni wanafunzi wangapi wanadaiwa unaweza ukakuta ni jamaa yako tu!ukakuta umepotosha umma kwa kutokuwa makini wewe kama mtanzania una haki ya kupata habari sehemu yoyote ni vema ukachukua hatua stahiki
 
UDOM ni chuo cha kata,kimejengwa kisiasa,UDSM ndo kila kitu "the home of intellectuals"
 
Udsm ndio habari ya Africa,kaUdom ni sawa na 2le 2vyuo twa Mkabala na Tra,ghorofa ya 0713
 
Walewale,kwaiyo na wewe tukuite intellectual????????
kumbe na ww bado mshamba,dogo tulia Udsm ndo mpango mzima,njoo usome hapa afu kama utakumbana na adha hiyo ya chuo chako cha kata
 
mkuu wa chuo - pro. wa kiswa
hayo yanawezekana kabisa
 
hallow! mi nafkir c inshu ya kuzungumzia how UDOM is, coz no wher is perfect except heaven. cha msing 2jue ukwel halis wa jambo hilo na kuwasaidia hao wapate vyet vyao hata kwa mawazo n.k
 
kumbe na ww bado mshamba,dogo tulia Udsm ndo mpango mzima,njoo usome hapa afu kama utakumbana na adha hiyo ya chuo chako cha kata

Mshamba kivipi??????????chuo cha kata kwa vigezo vipi?????????kusoma Udsm ndo ujanja?????????lol to my ribs

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…